04/09/2026
๐๐๐๐ ๐ฌ๐๐๐๐ ๐๐ง๐ ๐ ๐๐๐๐๐ฆ๐ ๐ช๐๐ก๐ก๐ ๐๐ช๐ ๐๐จ๐ฃ๐ข๐๐๐ ๐๐ข๐ก๐๐ข
Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imewakamata maafisa wanne wa umma katika operesheni tofauti katika ๐ธ๐ฎ๐๐ป๐๐ถ ๐๐ฎ ๐๐๐ฎ๐น๐ฒ ๐ป๐ฎ ๐๐๐ป๐ด๐ผ๐บ๐ฎ,kwa madai ya kuitisha na kupokea hongo kutoka kwa wananchi.
Waliokamatwa ni maafisa wawili wa usalama wa Kampuni ya Kenya Power mjini Diani, Kaunti ya Kwale, na maafisa wawili wa Uzingatiaji wa Sheria na Utekelezaji wa Kanuni katika Serikali ya Kaunti ya Bungoma, mjini Kimilili.
๐๐๐ธ๐ผ ๐๐๐ฎ๐น๐ฒ, maafisa wa EACC kutoka Ofisi ya Kanda ya Pwani ya Chini, Mombasa, waliwakamata maafisa hao wa Kenya Power Joseph Dena na Fredrick Odhiambo baada ya kudaiwa kuitisha hongo ya Sh100,000 kutoka kwa mlalamishi.
Maafisa hao wanadaiwa kumshutumu mlalamishi kwa kutumia umeme kinyume cha sheria na kumtaka awape fedha hizo ili wamsaidie kuachiliwa na kuhakikisha kuwa hachukuliwi hatua za kisheria.
Baada ya kupokea malalamishi hayo, Tume iliendesha operesheni iliyosababisha kukamatwa kwa washukiwa hao walipokuwa wakipokea Sh50,000.
Walifikishwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mombasa kuandisha taarifa na baadaye wakaachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu ya Sh20,000 kila mmoja, huku uchunguzi ukiendelea.
๐๐๐ธ๐ผ ๐๐๐ป๐ด๐ผ๐บ๐ฎ, Tume iliwakamata askari wa Serikali ya Kaunti, Victoria Mala Nafula na Elizabeth Nafuna Lukhale, baada ya kudaiwa kuitisha na kupokea hongo kutoka kwa mhudumu wa cyber cafรฉ katika Manispaa ya Kimilili.
Maafisa hao wanadaiwa kumtaka mfanyibiashara huyo awape fedha hizo ili amruhusu kuendelea kuendesha biashara yake bila leseni. Pia wanadaiwa kumtishia kufunga biashara hiyo iwapo hangewapa hongo hiyo.
Baada ya uchunguzi wa awali, EACC iliendesha operesheni na kuwakamata maafisa hao walipokuwa wakipokea pesa kutoka kwa mlalamishi.
Washukiwa hao walipelekwa katika Ofisi ya EACC, Kanda ya Magharibi mjini Bungoma kuandikisha taarifa, na baadaye wakapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Bungoma, ambako walilala usiku mmoja. Waliachiliwa asubuhi kwa dhamana ya pesa taslimu ya Sh20,000 kila mmoja huku uchunguzi ukiendelea.
Kukamatwa kwa maafisa hao kunajiri wakati Tume inaongeza juhudi za kukabiliana na hongo na aina nyingine za ufisadi katika vituo vya utoaji wa huduma, ambako wananchi hukutana moja kwa moja na maafisa wa umma.
๐๐๐๐ ๐ถ๐ป๐ฎ๐๐ฎ๐ต๐ถ๐บ๐ถ๐๐ฎ ๐๐ฎ๐ป๐ฎ๐ป๐ฐ๐ต๐ถ ๐ธ๐๐ฟ๐ถ๐ฝ๐ผ๐๐ถ ๐๐ถ๐๐ฎ ๐๐๐ฎ ๐ธ๐๐ถ๐๐ถ๐๐ต๐๐ฎ ๐ต๐ผ๐ป๐ด๐ผ ๐ป๐ฎ ๐๐ถ๐๐ฒ๐ป๐ฑ๐ผ ๐๐ถ๐ป๐ด๐ถ๐ป๐ฒ ๐๐๐ฎ ๐๐ณ๐ถ๐๐ฎ๐ฑ๐ถ ๐๐ถ๐ป๐ฎ๐๐๐ผ๐ณ๐ฎ๐ป๐๐๐ฎ ๐ป๐ฎ ๐บ๐ฎ๐ฎ๐ณ๐ถ๐๐ฎ ๐๐ฎ ๐๐บ๐บ๐ฎ. Tume inawahakikishia wananchi kuwa malalamishi yao yatashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.