UVCCM Tz

UVCCM Tz "KULINDA NA KUJENGA UJAMAA"

05/06/2026

RAIS DKT. SAMIA: TANZANIA HAIPO KWENYE VIKWAZO

Rais wa Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania haijawekewa vikwazo vya kimataifa (sanctions) na inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.



05/06/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika Jijini St. Petersburg nchini Urusi tarehe 05 Juni, 2026. Kongamano hilo limewakutanisha Wafanyabiashara, Wawekezaji pamoja na Taasisi za kukuza Uwekezaji kutoka Tanzania na Urusi.


05/06/2026

VIJANA TUPO TAYARI KUKUPOKEA RAIS DKT. SAMIA, KARIBU SANA

Vijana wa Tanzania wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuandika historia ya kufanya ziara ya kikazi nchini Urusi akiwa Rais wa pili baada ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambayo inatoa nafasi zaidi ya Tanzania kuendelea katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, elimu na uwekezaji.

Vijana hao kutoka mikoa yote ya Tanzania kesho tarehe 06 Juni 2026 watakutana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kumlaki akirejea kutoka nchini Urusi

05/06/2026

Vijana wa Tanzania waamesema ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Urusi imeongeza matumaini kwa vijana, hususan katika fursa za elimu, teknolojia na ushirikiano wa maendeleo.

"Na nikiongelea kuhusu ziara ya Mheshimiwa Rais Samia katika nchi ya Urusi: Kwanza, matarajio ya vijana wengi katika nchi hii, tunafahamu Urusi ni taifa lenye uchumi mkubwa lililoendelea kiteknolojia, kiulinzi, na katika nyanja mbalimbali. Kwa hiyo, vijana wengi wamepata shauku kubwa na wamehamasika baada ya kuona Rais ameenda kwenye nchi hiyo na kuwa na matarajio makubwa"

Aidha, amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Dkt. Samia kesho Juni 06 mara atakaporejea nchini kutoka katika ziara hiyo ya kihistoria.

05/06/2026

Vijana nchini wamempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia ziara yake nchini Urusi, wakieleza kuwa imefungua fursa mpya za maendeleo kwa vijana wa Kitanzania.

Wakizungumza kwa niaba ya wanafunzi na vijana, wamesema ziara hiyo imeweka msingi wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi, hususan katika sekta ya elimu, ambapo nafasi za masomo (scholarships) zinatarajiwa kuongezeka na kutoa fursa kwa vijana wengi kupata maarifa, ujuzi na utaalamu wa kimataifa.



05/06/2026

VIJANA TANZANIA WAMPONGEZA RAIS DKT. SAMIA KUFUNGUA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO URUSI

Vijana wa Tanzania wamempongeza Rais Jamhuri ya Muungano ww Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ziara yake nchini Urusi ambayo imeendelea kufungua milango ya fursa za elimu, mafunzo na ushirikiano wa kimataifa kwa vijana.

Vijana hao wameeleza kuwa hatua hiyo itachochea upatikanaji zaidi wa ufadhili wa masomo, ujuzi wa teknolojia na kuboresha uwezo wa vijana kushindana katika soko la ajira la kimataifa, sambamba na kuimarisha mahusiano ya Tanzania na Urusi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Vijana hao wamesema kuwa kesho tarehe 06 Juni 2026 watashiriki kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Rais wetu kipenzi wa maendeleo, Dkt.
Samia.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Kongamano la Biashara na Uwekez...
05/06/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika Jijini St. Petersburg nchini Urusi tarehe 05 Juni, 2026. Kongamano hilo limewakutanisha Wafanyabiashara, Wawekezaji pamoja na Taasisi za kukuza Uwekezaji kutoka Tanzania na Urusi.


05/06/2026

KARIBU NYUMBANI DKT. SAMIA

Jumamosi ya Tarehe 6 Juni 2026 ni siku ya kipekee kwa vijana na watanzania wenye mapenzi mema na Taifa letu kwenda kumpokea mwana diplomasia ya uchumi, mbeba maono na maslahi mapana ya Tanzania kimataifa.

Karibu nyumbani Rais wetu, kipenzi chetu Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ziara Yako Ina Faida kubwa sana kwa vijana na taifa kwa ujumla.



KATIBU MKUU WA CCM AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA KUJADILI USHIRIKIANO WA MAENDELEO NA DIRA 2050Katibu Mkuu wa CCM akuta...
05/06/2026

KATIBU MKUU WA CCM AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA KUJADILI USHIRIKIANO WA MAENDELEO NA DIRA 2050

Katibu Mkuu wa CCM akutana na Balozi wa Uingereza Kujadili Ushirikiano wa Maendeleo na Dira 2050

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Asha-Rose Migiro, leo Ijumaa Juni 5,2026 amefanya mazungumzo na Mheshimiwa Marianne Young, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, katika Makao Makuu ya CCM, Dodoma.

Mazungumzo hayo yalihusu maeneo ya ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Uingereza, kwa kuzingatia vipaumbele vilivyobainishwa katika Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya mwaka 2025–2030, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Viongozi hao walijadili fursa za kuendeleza ushirikiano kwenye maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hususan katika kuwawezesha vijana na wanawake kupitia elimu, ujuzi, ubunifu na uwekezaji.

CCM inaendelea kuthamini ushirikiano wa kimataifa unaochangia maendeleo endelevu na ustawi wa wananchi wa Tanzania.



Address

Петербургское ш., 64
Saint Petersburg
196140

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UVCCM Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share