Meru District Council

Meru District Council Meru DC
Ukurasa rasmi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru
www.merudc.go.tz

Halmashauri ya Wilaya ya Meru kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii Leo Tarehe 22 Mei , 2026 imetoa Mikopo ya Asilimia 10 ...
22/05/2026

Halmashauri ya Wilaya ya Meru kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii Leo Tarehe 22 Mei , 2026 imetoa Mikopo ya Asilimia 10 ya Mapato ya ndani kwa vikundi vya wanawake , Vijana na walemavu yenye Thamani ya shilingi za Kitanzania Milioni Mia Sita Sabini na Tatu ( 673,000,000.00) kwa Robo ya Nne ya Mwaka wa Fedha 2025/2026.

‎Kwa mara ya katika Ugawaji wa Mikopo katika Halmashauri ya wilaya ya Meru Vijana wamepata Fedha nyingi kuliko Kundi lolote Kiasi cha shilingi Milioni Mia Tatu Hamsini na Saba (357,000,000.00) huku wanawake wakipata shilingi Milioni Mia Mbili Themanini na Mbili (282,000,000.00) na watu wenye ulemavu Milioni Thelathini na Nne ( 34,000,000.00).

‎katika hafla hiyo ya ugawaji mikopo mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe.Joshua Nassari amewataka wananchi kutumia mikopo hiyo k**a fursa ya kukuza uchumi huku Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Lucas Kaaya amesema Halmashauri ya wilaya ya Meru imeandaa mpango wa kuwawezesha vikundi viinavyopata mikopo kushinda zabuni mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri.

‎Halmashauri ya wilaya ya Meru kwa Mwaka wa fedha wa 2025/26 imetoa jumla ya shilingi Bilioni Moja , Milioni Mia Tatu Kumi na Nane na Laki Nane ( 1,318,800,000.000) , huku Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Frola Msilu amesema Halmashauri itaendelea kuwawezesha wananchi wake kwa kutoa mikopo pamoja na elimu ya matumizi ya fedha.


https://www.instagram.com/reel/DYpXEpbM_7J/?igsh=MXR5cWs4bm11eHpvYQ==

20/05/2026
20/05/2026

Address

Arusha

Opening Hours

Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Meru District Council posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share