10/04/2020
Mtunzi : Chris L Kessy
Jina langu naitwa Daudi nina mke ambaye kwa sasa ni mjamzito, Mimba yake ina nipa mashaka sana kwani toka kipindi cha nyuma sikuwa na maelewano mazuri na yeye.
"hivi mke wangu huyo anaye kutumia text kila siku ni nani" Kulikuwa kuna ujumbe umeingia pindi nilipo kuwa nimeketi chumbani na mke wangu majira ya usiku.
'Jamani mume wangu mimi simjui kila siku nakwambia namba hiyo ni ngeni."
"sasa namba ngeni ndiyo kila siku iwe inakutumia ujumbe tu.."
Nilichukua ile simu ya mke wangu kwa lengo la kupiga sema kwa bahati mbaya haikuwa na salio na pia chaji ilikuwa imeisha ikazima ghafla. Nikaamua kulala zangu usingizi.
Siku iliyo fuata sikuweza kukumbuka kupiga hiyo namba kutokana na kuwa busy na mambo yangu.
Nilidamka asubuhi na kisha nikaelekea zangu kazini.
BAADA YA MIEZI 9 MKE WANGU ALIFANIKIWA KUJI FUNGUA SALAMA.
"Hongera sana mkeo amejifungua mtoto wa kiume."
alisema daktari.
"Asante sana" nilimjibu.
Tulitoka pale hospitali nikiwa na mke wangu pamoja na mama yake.
"Mwanangu Daudi mi nafikilia Lilian akakaae kwanza nyumbani na mtoto mpaka itakapo timu 40 ndiyo atarejea kwako ili na wewe upate muda mzuri wa kufanya mambo yako." Aliniambia mama mkwe.
"sawa" nilimkubalia.
Basi mke wangu ilibidi aondoke na mwanangu kwenda kukaa kwa mama yake.
Nilikuwa napeleka pesa za matumizi, pamoja na matunda, kuku wa nyama kwa ajili ya supu ili tu mke wangu arejeshe mwili wake. Nilifurahi sana kupata mtoto wa kiume kwani ndiyo ombi langu la kwanza kwa Mungu.
Kipindi chote icho nilikuwa na amani na mke wangu kwani sikuwa na mikwaruzo yoyote pia ata ile namba ya simu iliyo kuwa inakosea kutuma ujumbe hakuwa ikisumbua tena.
BAADA YA SIKU 40 KUFIKA NILIANDAA SHUGHULI KWA AJILI YA KUTOKA MWANANGU.
Shughuli hiyo ilifanyikia nyumbani kwa mama mkwe wangu, watu walikuwa wengi sana, walikula na kunywa mpaka kusaza.
Ilipo fika usiku nilimchukua mke wangu na kurudi nyumbani.
Nilipo fika nyumbani tuliingia ndani na kuketi sebuleni.
Wakati tulipo keti sebuleni tukipiga stori mbili tatu na mke wangu ghafla ujumbe ukaingia kwenye simu ya mke wangu.
Simu yake ilikuwa ipo mezani nilikuwa wa kwanza kuichukua na kuisoma wakati mke wangu aliniaga mara moja na kwenda chooni. Ujumbe ulikuwa unasema hivi.....
"Hongera sana kwa kuniletea mtoto wa kiume mke wangu.."
Nilishtuka, nilipoitazama ile namba kwa umakini nikaja kukumbuka ni namba ambayo ilikuwa inamsumbua sana mke wangu kipindi cha nyuma. Na ndiyo namba ambayo ilikuwa inafanya nisiwe na maelewano mazuri na mke wangu.
Nikawa najiambia mwenyewe "huyu mtu atakuwa ana mahusiano na mke wangu kwanini ampe hongera ya kujifungua.."
Nilipatwa na hasira nilijikuta na mtazama mwanangu akiwa amelala kwenye sofa, nilimchukua na kisha machozi yakawa yana nitoka... ile mke wangu anarejea kutoka chooni anafika na kunikuta nimembeba mtoto uku nikilia.
"vipi mume wangu una tatizo gani, na mbona unalia..? aliniuliza swali mke wangu.
"Nilicho kifanya nilinyanyua kidole na kumuonyesha mke wangu simu yake, alisogea na kuichua. Baada ya kuchukua kitu cha kwanza kukutana nacho ni ule ujumbe, aliusoma. ile alipo maliza kuusoma akasema...
"Ukweli mume wangu mimi hii namba siijui... Naapa kwa Mungu wangu tena anihadhibu mimi siijui hii namba kweli tena.." kabla hajamaliza kuongea maneno yake nilijikuta nimechukua maamuzi ya kinyama sana kwani nilimnyanyua mtoto wangu juu na kisha nikampigiza chini... kwa kuwa alikuwa bado ni kichanga hivyo ilipelekea kichwa kupasuka, na damu ilitapaka pale sebuleni.. Nilimuua mwanangu..!!
"Mamaaaaa mwananguuuuu...!! mke wangu alipiga mayoe alilia sana alitoka pale na kuukimbilia mwlili wake pale chini.
Mimi nilibaki nimesimama uku mwili ukinitetemeka na jasho jingi likinitoka.
Wakati mke wangu akiwa analia ghafla ile simu yake ikaanza kuita tena... nilitoka na kisha nikaichukua, nilipoitazama ilikuwa ni ile namba ikipiga... Taratibu nikaipokea uku machozi yakinitoka na mafua kwa mbali...
"Unataka nini.." nilimuuliza
"Aisee kaka
Ngoja kwanza nikuambie kitu ambacho kitakusaidia wewe mkuu ambaye unasoma hii.
Hadithi hii inapatikana ndani ya equatorstory.com mwendelezo na hadithi k**a hizi utaipata ndani humo.
Basi twendelee
"Aisee kaka samahani sana unajua hii namba siku zote nilikuwa natuma jumbe nilikuwa najua ni ya mke wangu kumbe sio nilikuwa nakosea namba ya mwisho..." Nisamehe sana bwana... leo ndiyo nimegundua maana amenitafuta baada ya kutoka kujifungua .
"Nini....? nilijikuta nimetoa sauti kubwa ya mshangao...
JE MKE WANGU NITAMWAMBIA NINI MPAKA ANIELEWE..? NA JE UMEJIFUNZA NINI KUHUSIANA NA HII SIMULIZI...?
Kuendelea na hadithi hii tembelea
https://equatorstory.com/story/16/ep/2.
Asante
WRONG NUMBER (Namba ngeni) episode 1 Jina langu naitwa Daudi nina mke ambaye kwa sasa ni mjamzito, Mimba yake ina nipa mashaka sana kwani toka kipindi cha nyuma sikuwa na maelewano mazuri na yeye. "hivi mke wangu huyo anaye kutumia te