03/09/2026
Arusha Septemba 3 2026 Hali ya taharuki imeibuka majira ya mchana katika maeneo ya Viwandani Kata ya Themi jijini Arusha baada ya gari kuwagonga watoto wawili waliokuwa wakitoka shuleni
Inaelezwa kuwa watoto hao walikuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Olorien ambapo mtoto mmoja amefariki dunia papo hapo katika eneo la tukio
Mtoto wa pili ambaye alijeruhiwa katika ajali hiyo alifariki dunia akiwa anapelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu
Baada ya ajali hiyo wananchi wenye hasira kali waliichoma moto gari hilo lililohusika katika ajali hiyo na kuteketea kabisa
Inaelezwa kuwa dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo alikimbia eneo la tukio baada ya ajali hiyo ili kuepuka hasira za wananchi waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo
Tukio hilo limesababisha taharuki katika eneo hilo huku vyombo vya ulinzi na usalama vikifika na kuanza kufuatilia tukio hilo