31/08/2023
HAFLA YA KUFUNGA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO KETUMBEINE.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Marco Ng'umbi amelishukuru Shirika la World Vision Tanzania kwa kutekeleza Miradi mbalimbali ya maendeleo k**a ya Afya, Elimu, Maji na kupeleka vyakula mashuleni kwa muda wa miaka 15 na kuisimamia vizuri kwa mda wote huo, kwa niaba ya Wananchi wa Longido amewasihi Wadau hao kwenda kuangalia maeneo mengine ya Wilaya ili kwenda kutekeleza miradi k**a hiyo baada ya kufunga mradi wao kwenye Tarafa ya Ketumbeine.
"Tunawashukuru sana kwa kazi kubwa mliyoifanya kwenye Wilaya ya Longido kwani hii ni Sadaka kubwa sana mmefanya kwa kuwajali wahitaji. Hakika Watoto na wanufaika wengi wemenufaika sana. Hata hali ya usomaji na kujiunga na shule imefanikiwa kwa asilimia 100%," alimaliza kwa kusema.
Naye Mkurugenzi wa World Vision Tanzania ameshukuru Mungu na Wananchi wanufaika na miradi hiyo kwa kuifikia siku ya leo na kumaliza mradi uliokuwa ukitekelezwa kwa kipindi cha miaka 15 kwenye Tarafa ya Ketumbeine , pi amemshukuru Mgeni rasmi kwa kuweza kutenga muda na kushiriki shghuli hiyo, aidha ameipongeza timu nzima iliyotekeleza na kusimamia mradi wa Ketumbeine AP pamoja na kutoa shukrani za kipekee kwa Wafadhili wote wa ndani na nje wa miradi iliyotekelezwa kwenye Tarafa ya Ketumbeine.
"Hakika namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa mema na baraka hizi zote" alisema.