07/07/2020
Sehemu ya 3.....
Ndio maana leo vijana wengi suala la kuoa limekuwa mtihani, hawajui nani wamuoe, lini na kwa nini? Ukiwauliza utasikia 'bado nipo nipo kwanza'
Pia mabinti wamekuwa na uhitaji sana wa kuolewa kwa hofu tu ya umri kuwatupa mkono na hofu ya kuonekana vibaya kwa jamii kuwa wana gundu! Hivyo wengine wanajiingiza tu popote ilimradi tu waonekane wameolewa! Yaani ni vurugu tupu!
Kwa hiyo hoja yangu leo ni kuwa, vijana wanapaswa kupunguza 'kutumia akili na utashi wa nafsi' ktk kutafuta mwenzi, bali zaidi wazingatie tija ya 'utu wa ndani wa mtu' ambao kwa lugha nyepesi tunaweza kusema wazingatie 'lengo' 'tabia' na 'mazingira' halisi ya kumtafuta huyo mwenzi!
Kwa mfano, kuna watu tumesoma shule ambazo sio sahihi kwetu kwa sababu tu ndio zilizokuwepo ktk mazingira yetu! Pia kuna aina ya maisha tuliyoishi ktk familia zetu kwa sababu tu hatukuwa na chaguo lingine!
Kuna vijana wengi kwa hakika wameshindwa kupata wenzi bora kwa sababu wamekuwa na vigezo vingi vyenye msukumo wa tamaa za nafsi zaidi! Wamewakataa tena kwa ujasiri kwa sababu tu hawana muonekano wanaoupenda, hasa mabinti!
Kwa hiyo, km vile neno tuliloanza nalo, tusizitegemee sana akili ktk kuchagua mwenzi, tumtegemee Mungu zaidi! Tusitegemee kwa kuwa tumemuomba Mungu, basi atatuletea wenzi kulingana na utashi wetu, mawazo ya Mungu sio k**a yetu, wala njia zake sio k**a zetu! Unaweza kutamani mfupi akakupa mrefu, ukitaka mweupe anakupa mweusi, n.k
Mwenzi akikujia, akakueleza haja ya moyo wake, kabla ya kumjibu 'Ndio' au 'Hapana' pata muda wa kutafakari. Muombe akupe muda wa kutafakari. Funga fikra, fungua moyo. Muulize Mungu, shirikisha Mchungaji wako ndipo utoe jibu!
Naomba kuwasilisha!
Share na vijana wengine tufanye marekebisho!