HabariLeo

HabariLeo HABARILEO Gwiji la Habari Tanzania| Kwa habari za uhakika na kina | Sehemu ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania
Tanzania Standard Newspapers (TSN)
(2)

Kurasa za mbele HabariLEO Jumatatu  Agosti 17, 2026Soma nakala yako kupitia kiunganishi cha http://epaper.tsn.go.tz
16/08/2026

Kurasa za mbele HabariLEO Jumatatu Agosti 17, 2026
Soma nakala yako kupitia kiunganishi cha http://epaper.tsn.go.tz

KAGERA; Mchezaji wa Simba, Libasse Gueye ameibuka Mchezaji Bora wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Kagera Sugar...
16/08/2026

KAGERA; Mchezaji wa Simba, Libasse Gueye ameibuka Mchezaji Bora wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Kagera Sugar na Simna uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba leo Agosti 16, 2026. Simba ilishinda mabao 0-2.
-

16/08/2026

DAR ES SALAAM: Mtanzania mwenye umri wa miaka 15, Xyleen Mapunda, amekuwa Mtanzania wa kwanza kushiriki katika safari ya kisayansi ya kufika North Pole, kupitia meli ya nyuklia ya kuvunja barafu.
-
Akizungumza wakati wa kumpokea Xyleen, Dickson Mangera, mwakilishi wa Mantra Tanzania Limited, amesema Xyleen alichaguliwa baada ya kushiriki mchakato wa ushindani ulioanza mwezi Mei mwaka huu, uliowahusisha vijana wenye umri wa miaka 14 hadi 16.
-
Amesema zaidi ya Watanzania 50 waliomba kushiriki, huku Xyleleen akiibuka mshindi na kuiwakilisha Tanzania katika safari hiyo ya kimataifa.
-
Katika safari hiyo, Xyleen alipata mafunzo kuhusu sayansi ya nyuklia, mazingira ya Arctic na umuhimu wa sayansi katika maendeleo.
-
Safari hiyo ilishirikisha washiriki kutoka mataifa 22, Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi za Afrika zilizoshiriki.
-

KAGERA; Simba ya Dar es Salaam leo imeibuka na ushindi wa mabao 0-2 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa kwanza Ligi K...
16/08/2026

KAGERA; Simba ya Dar es Salaam leo imeibuka na ushindi wa mabao 0-2 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2026/27, uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Mabao ya Simba yamefungwa na Ismail Toure na Elie Mpanzu.
-

DAR ES SALAAM; MTOTO Mtanzania Xyleen Mapunda (15) amesema amefurahi kujifunza namna madini ya urani yanavyotumika kuten...
16/08/2026

DAR ES SALAAM; MTOTO Mtanzania Xyleen Mapunda (15) amesema amefurahi kujifunza namna madini ya urani yanavyotumika kutengeneza nishati ya nyuklia na faida zake.
-
Xyleen alisema hayo alipowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo Agosti 16, 2026 akitoka nchini Urusi.
-
Alikwenda huko kwa safari ya kielimu na kisayansi baada ya kushinda shindano la kimataifa la Icebreaker of Knowledge 2026 kupitia programu ya kampuni ya Nishati ya Nyuklia ya Urusi, Rosatom.
-
Xyleen ameweka historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kufika Ncha ya Kaskazini (North Pole) katika safari ya siku 10 akiwa na wanafunzi wenzake wenye vipaji kutoka nchi 22 duniani.
-
Katika safari hiyo kutoka mji wa Murmansk kwenda Ncha ya Kaskazini, Franz Josef Land na kurejea Murmansk, wanafunzi hao walitumia meli kubwa zaidi duniani inayotumia nishati ya nyuklia 50 Let Pobedy.
-
“Meli yenyewe inatumia nyuklia, tumejifunza namna madini ya urani yanavyotumika kutengeneza nishati ya nyuklia na namna inavyotumika kwenye masuala mbalimbali… nimejifunza jambo zuri sana ambalo sikuwahi kufikiria,” alisema Xyleen.
-
Isome zaidi kupitia kiunganishi cha http://epaper.tsn.go.tz
Imeandaliwa na Zena Chande

DAR ES SALAAM: DIRA ya 2050 inataka kila mtanzania anaenda kutimiza ndoto aliyoikusudia kwa kuhakikisha mama mjamzito an...
16/08/2026

DAR ES SALAAM: DIRA ya 2050 inataka kila mtanzania anaenda kutimiza ndoto aliyoikusudia kwa kuhakikisha mama mjamzito anajifungua salama, vijana ndoto zao zinakuwa bora, mjasiriamali kuwa mfanyabiashara mkubwa, na kwa mwanafunzi anatimiza ndoto zake kwa kufika chuo kikuu ili Tanzania iwe na wataalamu bora.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amesema hayo jana, Agosti 16, 2026, wakati akihitimisha CRDB Marathon jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, huku akiipongeza CRDB Group kwa uamuzi wa kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema programu ya iMbeju haiwezi kutenganishwa na Dira ya 2050 kwani Tanzania imeingia katika hatua mpya kupitia Dira hiyo na CRDB tayari wameshaanza kuitekeleza kwa vitendo.

Nsekela ameeleza kuwa Dira hiyo haiwezi kujengwa na serikali pekee bali inahitahi sekta binafsi, taasisi za fedha, vijana, wajasuriamali, wanamichezo, wasanii na watanzania kwa ujumla, hivyo crdb group wamepokea wajibu huo kwa umakili na watashirikiana na serikali katika utakelezaji huo.

"hatutaki kuwa benki inayofadhili tu matukio au mipango ya Dira bali tunataka kuwa sehemu ya kuijenga Dira ya 2050" amesema Nsekela.


DAR ES SALAAM: TIMU ya wawakilishi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), ikiongozwa na Meneja wa Huduma za Habar...
16/08/2026

DAR ES SALAAM: TIMU ya wawakilishi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), ikiongozwa na Meneja wa Huduma za Habari za Kidijitali, Sylvester Domasa, pamoja na Meneja wa Masoko na Utangazaji wa Bidhaa, Felix Mushi, imeshiriki katika CRDB Marathon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Ushiriki huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za CRDB Group katika kuchangia maendeleo na ustawi wa jamii, hususan kupitia mipango inayolenga kuboresha afya na maisha ya wananchi.


DAR ES SALAAM: ZAIDI ya Sh bilioni tano zilizopatikana kupitia mbio za CRDB Marathon zimekusanywa na kuelekezwa katika s...
16/08/2026

DAR ES SALAAM: ZAIDI ya Sh bilioni tano zilizopatikana kupitia mbio za CRDB Marathon zimekusanywa na kuelekezwa katika sekta ya afya, na kuwezesha watoto zaidi ya 400 wenye matatizo ya moyo kufanyiwa upasuaji pamoja na kuwasaidia wanawake 240 wenye ujauzito hatarishi kupata matibabu na huduma salama za kujifungua.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, ametoa taarifa hiyo leo, Agosti 16, 2026, wakati akizungumza katika bonanza la CRDB International Marathon lililofanyika katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

Bonanza hilo limewakutanisha zaidi ya washiriki 17,000 kutoka ndani na nje ya Tanzania, likihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, huku mgeni Rasmi akiwa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.

Nsekela amesema uwekezaji katika afya ni sehemu muhimu ya maandalizi ya kujenga uchumi imara wa Tanzania kuelekea mwaka 2050, ambapo amesisitiza kuwa maendeleo ya uchumi hayawezi kupimwa kwa fedha na miundombinu pekee bila kuzingatia ubora wa rasilimali watu.

“Uchumi mkubwa wa Tanzania wa 2050 hautajengwa na fedha wala miundombinu pekee, bali na Watanzania wenye afya, ujuzi, ubunifu, vipaji na uwezo wa kuzalisha thamani. Nyuma ya kila takwimu ya uchumi kuna mwanadamu,” amesema Nsekela.

Amesema CRDB Group imeamua kuendelea kuwekeza katika afya, vijana, ubunifu, michezo, utamaduni na fursa za kiuchumi kwa kutambua kuwa maendeleo endelevu yanahitaji watu wenye afya na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji.

“CRDB Group imezingatia na kujikita katika afya, vijana, ubunifu, michezo na utamaduni pamoja na fursa mbalimbali za kiuchumi, kwa sababu hatuwezi kujenga uchumi imara bila kuanza kujenga watu wenye afya, uwezo na maarifa,” amesema.


CRDB Marathon 2026 imehakikisha kila rika linapata afya ya mwili💪.
16/08/2026

CRDB Marathon 2026 imehakikisha kila rika linapata afya ya mwili💪.


CRDB Marathon leo Agosti 16, 2026 imewakutanisha washiriki wa aina zote katika mbio hizo, ikiwa ni ishara ya ushirikishw...
16/08/2026

CRDB Marathon leo Agosti 16, 2026 imewakutanisha washiriki wa aina zote katika mbio hizo, ikiwa ni ishara ya ushirikishwaji na usawa katika michezo. Ushiriki wa pamoja umeonesha kuwa kila mmoja ana nafasi ya kushiriki, kushindana na kuchangia katika shughuli za kijamii bila kujali hali yake ya kiafya au uwezo wa kimwili.


Address

Arusha
255

Opening Hours

Monday 07:30 - 05:30
Tuesday 07:30 - 05:30
Wednesday 07:30 - 05:30
Thursday 07:30 - 05:30
Friday 07:30 - 05:30
Saturday 09:00 - 04:00
Sunday 10:00 - 04:00

Telephone

+255737688205

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HabariLeo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to HabariLeo:

Shortcuts

Share