Tanapa Updates

Tanapa Updates The Official Page for Tanzania National Parks (TANAPA) News and Updates.

05/09/2026

Dkt. Kijaji asema moto uliozuka juzi Septemba 03, 2026 katika eneo la Kikerelwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro umedhibitiwa kwa asilimia 90, huku juhudi mbalimbali zikiendelea kuhakikisha moto huo unazimwa kabisa.

DKT. KIJAJI: MOTO NDANI YA HIFADHI YA TAIFA KILIMANJARO WADHIBITIWA KWA ASILIMIA 90Na. Philipo Paschal Hassan  - Kiliman...
05/09/2026

DKT. KIJAJI: MOTO NDANI YA HIFADHI YA TAIFA KILIMANJARO WADHIBITIWA KWA ASILIMIA 90

Na. Philipo Paschal Hassan - Kilimanjaro

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), leo Septemba 5, 2026, ametembelea eneo ulipozuka moto ndani ya Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kwa lengo la kujionea hali ya eneo hilo na hatua zinazochukuliwa kudhibiti na kuzima moto huo.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo, Dkt. Kijaji alisema kuwa moto huo umedhibitiwa kwa asilimia 90, huku shughuli za utalii zikiendelea vizuri ndani ya hifadhi. Pia alitoa rai kwa wananchi wanaozunguka hifadhi za Taifa kuepuka shughuli zinazoweza kusababisha moto.

“Ninatoa rai kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka hifadhi waepuke shughuli zinazoweza kusababisha moto na kuleta athari kwa mazingira na wanyamapori ndani ya hifadhi. Pia, endeleeni kuzingatia mipaka iliyowekwa kati ya maeneo ya hifadhi na maeneo ya wananchi”, alieleza Dkt. Kijaji.

Kwa upande wake, Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Massana Mwishawa ilibainisha kuwa zoezi la kudhibiti na kuzima moto huo linaendelea vizuri chini ya ushirikiano wa Jeshi la Uhifadhi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wadau mbalimbali wa utalii huku hatua mbalimbali zikiendelea kuchukuliwa kuhakikisha kuwa moto huo unadhibitiwa kikamilifu.

Naye, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TANAPA, Catherine Mbena aliwashukuru wadau wote walioshiriki katika jitihada za kudhibiti moto huo katika Mlima Kilimanjaro, kwa akitambua mchango wao wa hali na mali, ushirikiano na kujitolea kwao katika kulinda rasilimali za hifadhi na kuzuia moto huo kusambaa zaidi.

Ushirikiano wa wananchi wanaozunguka Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, TANAPA na wadau wa utalii ni muhimu katika kuimarisha uhifadhi na kukabiliana kwa pamoja na changamoto za moto, kwa kulinda rasilimali za hifadhi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Conservation thrives when communities thrive. Through continuous dialogue, mutual trust, and active collaboration, TANAP...
05/09/2026

Conservation thrives when communities thrive. Through continuous dialogue, mutual trust, and active collaboration, TANAPA remains committed to strengthening partnerships with neighboring communities by promoting open communication, sharing knowledge on conservation and tourism opportunities, and supporting community development initiatives that improve livelihoods and promote environmental conservation.

Together, we are building a future where people and nature coexist in harmony, ensuring that the benefits of conservation are shared for generations to come.

TAARIFA KWA UMMA
03/09/2026

TAARIFA KWA UMMA

02/09/2026

🎙️ TANAPA PODCAST | S02 EP 03 — Utalii wa ndani na nguvu ya vyombo vya habari katika kuitangaza Serengeti na vivutio vya Tanzania kwa Watanzania na dunia.

📍 Serengeti

🎙️ Catherine Mbena
👥 Rashid Suluhu Hassan & Yusuph Khamis. Ni mwendo wa bandika bandua!

01/09/2026

Every Moment. A Serengeti Story.

Mimi sina dukuduku 😌… lakini napenda kuwajulisha tu kwamba wale wote mliochukua muda wenu kutupigia kura na kutuamini, i...
31/08/2026

Mimi sina dukuduku 😌… lakini napenda kuwajulisha tu kwamba wale wote mliochukua muda wenu kutupigia kura na kutuamini, imani yenu imegeuka kuwa TUZO 6 za World Travel Awards 2026! 🌍

Safari yenu ndiyo ushindi wetu sote. Asanteni sana kwa kuendelea kuchagua, kutembelea Hifadhi za Taifa Tanzania. ❤️🇹🇿

Tuzo tulizoshinda 👇

🏆 HIFADHI YA TAIFA SERENGETI
🥇 Hifadhi Bora Barani Afrika 2026
🥇 Hifadhi Bora Afrika ya Wanyama Watano Wakubwa (Big Five) 2026

🏆 HIFADHI YA TAIFA NYERERE
🥇 Hifadhi Bora kwa Mandhari ya Kuvutia Barani Afrika 2026

🏆 HIFADHI YA TAIFA RUAHA
🥇 Hifadhi Bora kwa Utalii wa Kitamaduni Afrika 2026

🏆 HIFADHI YA TAIFA TARANGIRE
🥇 Hifadhi Bora Afrika kwa Utajiri wa Tembo 2026

🏆 HIFADHI YA TAIFA KILIMANJARO
🥇 Hifadhi Bora Afrika ya Milima 2026

TANAPA, Next Level
TANAPA, Nyumbani kwa Tuzo

KAMISHNA MWISHAWA: “ONGEZENI WIGO WA UTOAJI WA ELIMU YA UHIFADHI KWA WANANCHI”.Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadh...
31/08/2026

KAMISHNA MWISHAWA: “ONGEZENI WIGO WA UTOAJI WA ELIMU YA UHIFADHI KWA WANANCHI”.

Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Massana Mwishawa amekielekeza Kitengo cha Mahusiano ya Jamii kuongeza wigo wa utoaji wa elimu ya uhifadhi kwa wananchi hususan jamii zinazozunguka Hifadhi za Taifa ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi na maendeleo.

Akizungumza katika Kikao Kazi cha Mwaka cha Kitengo cha Mahusiano ya Jamii kinachofanyika jijini Dodoma Kamishna Mwishawa amesisitiza umuhimu wa elimu ya uhifadhi katika kujenga uelewa na mahusiano mazuri kati ya TANAPA na jamii. Elimu hiyo inapaswa kuwafikia wananchi kuhusu namna ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu, athari za mabadiliko ya tabianchi, uhifadhi wa vyanzo vya maji, fursa za uzalishaji mali kupitia utalii pamoja na usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya ujirani mwema.

Uimarishaji katika utoaji wa elimu na ushirikishwaji wa jamii, TANAPA inalenga kujenga jamii yenye uelewa na utayari wa kushiriki katika kuendeleza uhifadhi shirikishi wa maliasili. Ushirikiano huo ni muhimu katika kuimarisha mahusiano kati ya Shirika na jamii zinazozunguka Hifadhi za Taifa, kuongeza ushiriki wa wananchi katika shughuli za uhifadhi na kuhakikisha uhifadhi endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

PUBLIC NOTICECc,Serengeti National Park Tanzania National Parks Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿
31/08/2026

PUBLIC NOTICE

Cc,
Serengeti National Park
Tanzania National Parks
Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿

TAARIFA KWA UMMACc,Serengeti National Park Tanzania National Parks Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿
31/08/2026

TAARIFA KWA UMMA

Cc,
Serengeti National Park
Tanzania National Parks
Ukurasa Rasmi wa Wizara ya Utalii - Tanzania🇹🇿

Address

Majengo
Arusha
23104

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanapa Updates posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share