24/06/2017
Uzuri Bandia “
Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.” Zaburi 3:3.
Huku akikumbuka jinsi alivyovunja amri za Mungu, Daudi anaonekana kupooza kimaadili; alikuwa dhaifu na asiye na ujasiri, wakati ambapo kabla ya dhambi yake alikuwa amedhihirisha uthabiti na ujasiri.
Mvuto wake kwa watu ulikuwa umepungua sana. Na yote haya yalichangia kusaidia mipango ya mwanae asiye wa asili . . .
Wakati ambapo mfalme alipendelea zaidi maisha ya kujitenga na faragha, Absalomu alifanya bidii sana kujipendekeza ili akubalike kwa wengi …
Siku kwa siku mtu huyu aliyeonekana mwadilifu alionekana ameketi langoni mwa jiji, mahali ambapo makutano wenye shida mbalimbali walisubiri shida zao kushughulikiwa.
Absalomu alichangamana nao na kusikiliza malalamiko yao, akionesha huruma kwa shida zao na Masikitiko kwa serikali kushindwa kushughulikia kwa ufanisi.
Kwa mwonekano wake wa kupendeza, na tabia inayovutia, na huruma ya kujifanya, kwa ujanja aliteka mioyo ya watu.
Hakuwa na moyo wa ukarimu, lakini alikuwa mwenye kutaka makuu, k**a matendo yake yalivyoonesha alikuwa tayari kujenga fitina na hata kuvunja sheria ili mradi atwae ufalme.
Alikuwa radhi kulipa fadhila ya upendo na huruma ya baba yake kwa kumuua. Alitangazwa na wafuasi wake kuwa mfalme kule Hebron kisha akawaongoza kumtoa baba yake.
unyenyekevu na huzuni Daudi alipita nje ya lango la Yerusalemu, akiwa ameondolewa katika kiti chake cha ufalme, katika ikulu yake, kutoka kwa sanduku la Mungu la agano, kutokana na uasi wa mwanaye aliyempenda sana. Watu walifuata katika misafara mirefu ya huzuni k**a misafara ya maiti.
Wengi wasioona k**a aonavyo Mungu, bali wanaona mambo kwa mtazamo wa kibinadamu, wanaweza kudhani kwamba yawezekana Daudi alikuwa na sababu ya kutoridhika na kwamba kwa jinsi toba yake ilivyokuwa ya dhati miaka kabla ya wakati huu ilitosha kumwondoa katika kupata matokeo (hukumu) ya hapa duniani…
Daudi halalamiki popote. Zaburi fasaha kuliko zote alizowahi kuimba ilikuwa wakati akipanda Mlima wa Mizeituni, bila viatu na akilia, lakini roho yake ikijaa unyenyekevu, mkarimu na asiye na ubinafsi, aliyejisalimisha kwa Mungu na mwenye kuridhika. {CC 181.6}
Nikutakie jumamosi njema Mungu akubariki sana