15/03/2019
NAAM
SWALA YA IJUMAA KWA MWANAMKE...
Wamekubaliana wanazuoni juu ya swala ya ijumaa sio wajibu kwa mwanamke, na kuwa yeye ataswali nyumbani kwake rakaa nne (adhuhuri) na akiwa safarini ataswali rakaa mbili.
anasema ibn mudhir katika ijmaau "na wamekubaliana kuwa hakuna ijumaa kwa wanawake"
Pia kwa hadithi ya Mtume aliposema " ijumaa ni haki ya kila muislam katika mkusanyiko isipokuwa kwa wanne, mtumwa anayemilikiwa,au mwanamke, au mtoto, au mgonjwa". kapokea Abuu Daudi, kaisahihisha Al-baniy..
Na swala iliyokuwa bora kwa mwanamke ni ile anayoswali nyumbani kwake.
Kwa hadithi aliyopokea Ibn Mas'uud, Mtume anasema "swala ya mwanamke chumbani kwake ni bora kuliko swala yake katika sebule, na swala katika chumba kilichopo ndani ya chumba anacholala ni bora kuliko swala yake katika chumba anacholala". Kaipokea Abuu Daud 570, Tirmidhy 1173.
Na swala hapa zinaingia swala zote ikiwemo Ijumaa.
Mwanamke akiswali Ijumaa msikitini swala yake hukubaliwa kutokana na ijmaa ya wanazuoni, na haitomlazimu kuswali tena adhuhuri, kutokana na kuthibiti wanawake kuswali na Mtume lakini Mtume Swalla ALLAHU alayhi wa Sallam hakuwaambia warudie swala zao. Rejea lajna ddaaim fat'wa 7/337.
Ni vizuri mwanamke anapokwenda msikitini ajistiri vizuri bila kutia manukato wala kudhihiridha mapambo yake ili kuepuka fitna ambayo kwa ajili yake hupendeza aswali nyumbani kwake...
Na ALLAH ni mjuzi zaidi...
Uislamu Dini Yangu