08/06/2022
WILAYA YA CHAKE CHAKE
SABRINA KHAMIS JUMA
AFISA HABARI
WILAYA YA CHAKE CHAKE
Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Bw. Abdalla Rashid Ali amekabidhi Nyumba za makaazi kwa watu wenye Mahitaji Malumu katika Maeneo tofauti ndani ya Wilaya hiyo
Nyumba hizo zimwjengwa kupitia Taasisi ya IFRAJ ZANZIBAR FOUNDATION kwa lengo la kuwasaidia Jamii ambazo zinahitaji msaada.Waliokabidhiwa nyumba hizo Bw.Ali Khamis Kombo Mkaazi wa Mfikiwa na Bi Rehema Mzee Bakari mkaazi wa Chanjamjawiri.
Mkuu huyo amezitaka Familia kuzitunza na kuziboresha ilo ziweze kudumu muda mrefu ili lengo la kujengwa nyumba kufaidika kizazi na kizazi
Aidha katibu Tawala wa wilawa hiyo Bw. Suleiman Hamadi Suleiman amewashukuru tasisi ya IFRAJI ZANZIBAR FOUNDATION kwa kuiunga mkono serekali na kujenga nyumba hizo kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum
Kwa pamoja Familia hizo zilizokabidhiwa Nyumba huzo wameishukuru serekali pamoja na Tasisi ya IFRAJ ZANZIBAR FOUNDATION kwa msaada huo na wameahidi kuzitunza na kuzienzi nyumba hizo
.....MWISHO......