dcea_tz

dcea_tz Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from dcea_tz, Government Organization, 8 Kivukoni Road, Dar es Salaam.

The Drug Control and Enforcement Authority (DCEA) has the functions of define, promote, coordinate, and implement all measures geared towards control of drugs, drug abuse and trafficking in drugs.

ÌMamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Ziwa imeshiriki katika Mbio za Mwenge wa Uhuru wil...
11/08/2026

Ì

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Ziwa imeshiriki katika Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Ilemela jijini Mwanza Agosti 11, 2026 kwa kutoa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya kwa wananchi waliofika katika Viwanja vya Kabwali ambako pia kunafanyika mkesha wa Mwenge wa Uhuru kabla ya kukabidhiwa Wilaya ya Magu.

Kupitia banda lake DCEA imetoa elimu kuhusu madhara ya matumizi na biashaa ya dawa za kulevya huku wananchi wakihamasishwa kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya tatizo hilo.

Aidha, ujumbe wa dawa za kulevya ni ajenda muhimu katika mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa unaolenga kuhamasisha jamii kujiepusha na matumizi na biashara ya dawa za kulevya pamoja na kushirikiana na Serikali katika kuzuia na kupambana na tatizo hilo.

DCEA Kanda ya Ziwa itaendelea kutumia fursa mbalimbali za kitaifa kuifikia jamii kwa elimu na kuhamasisha wananchi kuwa sehemu ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Ziwa iloshoriki kutoa elimu kwa wananchi waliotembe...
08/08/2026

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Ziwa iloshoriki kutoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lake katika Maonesho ya Kikanda ya Nanenane yanayofanyika Viwanja vya Nyamhongolo mkoani Mwanza.
Ushiriki katika maonesho hayo ni sehemu ya mkakati wa kuifikia jamii moja kwa moja kwa kutoa elimu, kujibu maswali ya wananchi na kuongeza uelewa kuhusu nafasi ya kila mmoja katika mapambano dhidi ya dawa hizo

08/08/2026
*MSAFIRISHAJI WA KILI 26.4 ZA BANGI AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA.* Mahakama ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza, imemhukumu Benj...
07/08/2026

*MSAFIRISHAJI WA KILI 26.4 ZA BANGI AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA.*

Mahakama ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza, imemhukumu Benjamin Robat Ndarahwa (25), mkazi wa Isamilo, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukiri kosa la kusafirisha kilogramu 26.4 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani, Juni 9, 2026 maofisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) walifanya operesheni katika eneo la Isamilo, Wilaya ya Magu na kukamata bangi hiyo pamoja na fedha taslimu TSh 353,500 zinazodaiwa kuwa zilitokana na biashara hiyo haramu. Uchunguzi wa Mkemia Mkuu wa Serikali ulithibitisha kuwa dawa zilizokamatwa zilikuwa bangi.

Kabla ya kutolewa hukumu, mshtakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu akieleza kuwa ni mkosaji wa kwanza na anamlea mtoto wa mwaka mmoja baada ya mke wake kufariki dunia. Hata hivyo, mahakama ilimhukumu kifungo cha miaka 30 jela kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.

DCEA inaendelea kuwakumbusha wananchi kushiriki kutoa taarifa kuhusu vitendo vya uzalishaji, usafirishaji na biashara ya dawa za kulevya ili kulinda afya, usalama na ustawi wa jamii.

Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza, imemhukumu Doto Meshaki Mitanda, mkazi wa Kishiri, Wilaya ya Nyamagana, ...
07/08/2026

Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza, imemhukumu Doto Meshaki Mitanda, mkazi wa Kishiri, Wilaya ya Nyamagana, kifungo cha miaka 10 jela baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa kilogramu 1.05, kinyume na Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Sura ya 95, Toleo Lililorekebishwa la mwaka 2023.

Hukumu hiyo ilitolewa tarehe 3 Agosti 2026 na Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana mbele ya Mheshimiwa Hakimu Mkazi Kubaja katika Shauri la Jinai Na. 1522/2026, Jamhuri dhidi ya Doto Meshaki Mitanda. Kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani, mshtakiwa alikamatwa tarehe 11 Oktoba 2025 akiwa na bangi yenye uzito wa kilogramu 1.05.

Katika kuthibitisha shtaka hilo, upande wa Jamhuri uliwasilisha ushahidi wa mashahidi saba pamoja na vielelezo mbalimbali vilivyoonyesha kuhusika kwa mshtakiwa katika kosa hilo. Kwa upande wa utetezi, mashahidi wanne, akiwemo mshtakiwa mwenyewe, walitoa ushahidi wao bila kuwasilisha kielelezo chochote.

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili, Mahakama iliridhika kuwa upande wa Jamhuri umethibitisha shtaka bila kuacha shaka yoyote ya msingi, ikamtia hatiani mshtakiwa na kumhukumu kifungo cha miaka 10 jela.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inaendelea kutoa elimu kwa wan...
06/08/2026

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika Maadhimisho ya Nanenane yanayofanyika kikanda katika Viwanja vya Nanenane, Uyole mkoani Mbeya.

Kupitia banda la DCEA, wananchi wanapatiwa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya, mbinu za kujikinga, pamoja na huduma za kinga, tiba na urekebishaji kwa watu wenye changamoto za matumizi ya dawa za kulevya.

DCEA inawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lake ili kupata elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka.

06/08/2026

Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda, mapema leo ametembelea banda la Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma.

Akiwa katika banda hilo, Mhe. Pinda ameishauri Mamlaka kuendelea kuweka mkazo katika utoaji wa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya, hususan kwa vijana wa vyuo vya elimu ya juu, ili kuwakinga dhidi ya kujiingiza katika matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Amesisitiza kuwa elimu endelevu ni nyenzo muhimu katika kujenga kizazi chenye afya, maadili na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia kanda zake zinazoshirik...
06/08/2026

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia kanda zake zinazoshiriki Maonesho ya Nanenane 2026 yanayofanyika katika maeneo mbalimbali nchini.

Kanda ya Kusini ilishiriki ufunguzi wa maonesho katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana (Mb.), Dkt. Joel A. Nanauka.

Kwa upande wa Kanda ya Magharibi, DCEA inaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho ya Kikanda ya Nanenane yanayofanyika Viwanja vya Ipuli, Tabora, huku ikihamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kuzuia matumizi, biashara na kilimo cha mazao ya dawa za kulevya.

Nayo Kanda ya Ziwa inaendelea kutoa elimu kupitia banda lake katika Viwanja vya Nyamhongolo, Mwanza, ambapo wananchi wanapata fursa ya kujifunza kuhusu madhara ya dawa za kulevya, namna ya kutambua viashiria vya matumizi yake na wajibu wa kila mmoja katika kuzuia na kupambana na tatizo hilo.

📍Tembelea banda la DCEA katika maonesho ya Nanenane yaliyo karibu nawe upate elimu sahihi kuhusu dawa za kulevya na ushiriki katika kujenga jamii salama.

📞 Toa taarifa kupitia namba ya bure 119.

03/08/2026

Wanakijiji wa Kata ya Kandawale na Kipatimo, Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi waliposhiriki Katika operesheni ya kufyeka mashamba ya bangi

Address

8 Kivukoni Road
Dar Es Salaam
S.L.P80327

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when dcea_tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share