NemcTanzania

NemcTanzania Karibu katika ukurasa rasmi wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC). Pamoja tulinde na kutunza mazingira kwa maendeleo endelevu.

NKM OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA) DKT. MADUHU KAZI AZURU NEMC šŸ“ŒšŸ“ŒAipongeza Serikali kwa kuthamini Mazingira katika ...
14/08/2026

NKM OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA) DKT. MADUHU KAZI AZURU NEMC


šŸ“ŒšŸ“ŒAipongeza Serikali kwa kuthamini Mazingira katika Dira ya 2050

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Maduhu Kazi, amezuru NEMC kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Kazi ameipongeza Serikali kwa kuthamini masuala ya Mazingira na kuipa kipaumbele ajenda ya mazingira katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, akisema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha maendeleo ya Taifa yanaenda sambamba na uhifadhi endelevu wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, ameipongeza NEMC kwa uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yake na kulitaka Baraza kuendelea kusimamia misingi ya Sheria, huku likiimarisha ufanisi katika uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa manufaa ya Taifa na vizazi vya baadae.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi alipokuwa akizungumza alimweleza Dkt. Kazi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Baraza na hatua zinazochukuliwa katika uhifadhi na usimamizi wa mazingira, huku akiahidi kuendelea kusukuma mbele ajenda ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na miongozo ya Serikali.

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN APANDA MTI KIZIMKAZI, ATOA WITO WA UHIFADHI WA MAZINGIRARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tan...
13/08/2026

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN APANDA MTI KIZIMKAZI, ATOA WITO WA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 13, 2026, amepanda mti aina ya muembe katika Kituo cha Afya Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni miongoni mwa shughuli kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi.

Hatua hiyo inaonesha dhamira ya dhati ya Mhe. Rais katika kuhamasisha uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira, pamoja na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa miti katika kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kupitia tukio hilo, Mhe. Rais ameendelea kutoa mfano wa uongozi katika agenda ya mazingira, akihimiza wananchi, taasisi na wadau mbalimbali kupanda, kutunza na kulinda miti ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira, ukame na athari za mabadiliko ya tabianchi.

NEMC inaunga mkono na kuendeleza wito huu wa Mhe. Rais kupitia elimu kwa umma, uhamasishaji wa jamii, usimamizi wa mazingira na utekelezaji wa programu zinazolenga kuongeza uoto wa asili, kupunguza uharibifu wa mazingira na kujenga Tanzania yenye mazingira salama na endelevu.

*Kupanda mti ni kuwekeza katika maisha, Mazingira na kizazi kijacho.*

USIKOSE KUSIKILIZAšŸ¤
13/08/2026

USIKOSE KUSIKILIZAšŸ¤

13/08/2026

TAZAMA WAKAZI WA MWANANYAMALA KWA MAMA ZAKARIA WAKIZUNGUMZIA KUHUSU MAZINGIRA NI UHAIšŸ¤

KATAA MIFUKO YA PLASTIKI, TUMIA MIFUKO MBADALA šŸ¤
13/08/2026

KATAA MIFUKO YA PLASTIKI, TUMIA MIFUKO MBADALA šŸ¤

12/08/2026

KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELEšŸ¤

KATAA MIFUKO YA PLASTIKI, TUMIA MIFUKO MBADALA AMBAYO NI RAFIKI WA MAZINGIRAšŸ¤
12/08/2026

KATAA MIFUKO YA PLASTIKI, TUMIA MIFUKO MBADALA AMBAYO NI RAFIKI WA MAZINGIRAšŸ¤

NEMC YAONGEZA VYOMBO VYA USAFIRI KUIMARISHA MIUNDOMBINU WEZESHI YA UTEKELEZAJIBaraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa...
11/08/2026

NEMC YAONGEZA VYOMBO VYA USAFIRI KUIMARISHA MIUNDOMBINU WEZESHI YA UTEKELEZAJI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeongeza vyombo vya usafiri kwa kutumia mapato yake ya ndani, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha miundombinu wezeshi ya utekelezaji wa majukumu ya kimazingira, ikiwemo ufuatiliaji, ukaguzi na uzingatiaji wa Sheria ya mazingira nchini.

Akizungumza leo Agosti 11, 2026 wakati wa makabidhiano ya magari mawili kwa baadhi ya viongozi wa Baraza, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi, amesema Baraza limeanza na magari mawili kati ya matano kwa ajili ya viongozi na linatarajia kununua magari mengine 20 ndani ya mwaka huu kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi katika Kanda zote 13 nchini.

ā€œMagari haya tumeyanunua sisi wenyewe kwa kutumia mapato yetu ya ndani na tunaanza na magari 5 kwa ajili ya viongozi, lakini kwa malengo tuliyojiwekea kwa mwaka huu tutanunua magari mengine 20 " amesema Dkt. Semesi.

Ameongeza ā€œHii ni katika kuhakikisha tunaboresha utendaji kazi katika jukumu tulilokasimiwa la usimamizi wa mazingira nchini, sawa na malengo na matakwa ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 pamoja na malengo ya Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,ā€

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Bw. Dickson Mjinja alipozungumza aliahidi utunzwaji wa magari hayo na kutumika kwa malengo kusidiwa huku akisistiza uwajibikaji kufikia malengo chanya.

TUMIA MIFUKO MBADALA, RAFIKI WA MAZINGIRAšŸ¤
11/08/2026

TUMIA MIFUKO MBADALA, RAFIKI WA MAZINGIRAšŸ¤

KATAA MIFUKO YA PLASTIKIšŸ¤
10/08/2026

KATAA MIFUKO YA PLASTIKIšŸ¤

Address

Regent Street
Dar Es Salaam
00000

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 09:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NemcTanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share