16/03/2023
KIKAO KAZI CHA TATHIMINI YA UTENDAJI KAZI KWA IDARA YA AFYA NUSU MWAKA 2022/2023
Idara ya afya Manispaa ya ubungo imefanya kikao kazi cha tathmini ya utendaji kazi kwa nusu mwaka julai- disemba 2022 ambapo taarifa kutoka vitengo mbalimbali vya idara ya afya, hospitali za umma na binafsi pamoja na zahanati ziliweza kutoa tathmini ya shughuli zilizotekelezwa
Aidha Katika kikao hicho Kuna vituo vya Afya, hospitali na zahanati ambazo zilionekana kufanya vizuri kwa utoaji mzuri wa huduma kwa wananchi na kufanikiwa kupewa vyeti vya pongezi kwa utendaji bora
Akiongea katika kikao hicho Mganga Mkuu Dkt.Tulitweni Mwinuka amesisitiza watumishi wote wa Afya kufanya kazi kwa weledi na kila mmoja katika kituo chake afanye kazi kwa uzalendo ili kuhakikisha Ubungo inaendelea kusimama imara katika utoaji wa huduma za afya
Aidha, Dkt. Tulitweni aliwapongeza wale wote ambao wamepata vyeti vya pongezi kwa kuonyesha utendaji kazi mzuri na kuwaasa waendelee kuwajibika vyema katika kuhakikisha huduma nzuri za afya zinatolewa kwa wananchi
Zoezi la ugawaji wa vyeti vya pongezi kwa hospitali, zahanati na vituo vya Afya pamoja na hospital binafsi zilizofanya vizuri ulifanyika ikiwemo Hositali ya Wilaya ya Ubungo, Sinza, kituo cha Afya Kimara, zahanati ya Kibwegere, zahanati ya Msumi, zahanati ya Mburahati, zahanati ya Kiluvya, zahanati ya Mabibo na zahanati ya Kwembe