14/11/2023
JINSI YA KUJENGA NDOA NA MAHUSIANO BORA💥
Nyumba hujengwa na vitu vingi ikiwemo msamaha na matumizi ya kinywa. Mama anapojua kutumia vizuri kinywa chake anayo nafasi kubwa sana kuiponya na kujenga hata kuimarisha ndoa yake.
MITHALI 9: 13💥 MITHALI 14: 1 - 5💥
Hili hutokana na majibu yake pale anapoongea na mume wake kwa kauli nzuri njema zenye kuvutia na kubembeleza; hulka ya mwanamke ni upole na kauli zake ni za kipole maneno matamu yenye kuvutia na kubembeleza hata k**a mtu kapandisha hasira kwa jibu na kauli yako ya upole
Unamshusha sawa na Neno la Mungu lisemavyo katika MITHALI 15: 1 💥ya kwamba "Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu."
Sio kila jambo unatakiwa kulitolea ufafanuzi ama kuongea, wakati mwingine jishushe tu omba msamaha hata uonapo umekosewa na kuonewa kisha nyamaza kimya maana kazi ya utetezi si yako bali ya Mungu wako yeye atasimama kukutetea kwa njia yake mwenyewe.
Kunyamaza ni hekima, maana maandiko yanasema kwamba "Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na mwenye roho ya utulivu ana busara. Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu." (MITHALI 17:27-28) na AYUBU 13:5 💥inasema kwamba "Laiti mngenyamaza kabisa! Hilo lingekuwa hekima kwenu."
kumbe basi kuna muda inakupasa kunyamaza kimya tu si kwa kiburi au dharau ila kuipisha ghadhabu tu.
Sote twafahamu ya kwamba ulimi ni kiungo kidogo lakini kina madhara makubwa sana kulingana na Neno la Mungu kutoka YAKOBO 3:5-6; 💥hivyo basi k**a mke chunga ulimi wako
▪Jishushe
▪Omba tu msamaha ubebe ubaya
▪Nyenyekea na kujishusha
▪Nyamaza kimya usifumbue mdomo wako kuongea ukiwa na hasira maana hasira haifanyi kazi na hekima hata siku moja.
▪Usiwe mwanamke wa kupiga piga kelele tu na kuongea sana
MITHALI 10:19 💥inasema kwamba "Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili." angalia katika kuongea kwako sana unakwaza na kukosea na WAEFESO 4:31💥 inatuonya ya kwamba "Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya"
Wewe ni mke jenga ndoa yako kwa kutumia kinywa chako na msamaha mwombe Roho wa Mungu akusaidie kujishusha, kuachilia, kusamehe, akupe hekima ya kiMungu ambayo ni safi, yenye amani, upole,iliyo tayari kusikiliza, imejaa rehema (msamaha), yenye kutenda mema isiyo na unafiki wala fitina (YAKOBO 3:17-18💥)
✍🏼 Mtumishi Fahim 0716 822126 Whatsapp 💥
Maombi na ushauri Whatsapp 0716 822126 🙏