NSSF Tanzania

NSSF Tanzania The National Social Security Fund is a fully funded scheme running under defined benefit principles.

ULIYE JIAJIRI, UMEJIUNGA NA KUJISAJIRI HIFADHI SCHEME?Bofya *152*00 # kisha endelea
03/09/2026

ULIYE JIAJIRI, UMEJIUNGA NA KUJISAJIRI HIFADHI SCHEME?

Bofya *152*00 # kisha endelea

03/09/2026

ULIYE JIAJIRI, UMEJIUNGA NA KUJISAJIRI HIFADHI SCHEME?

Fahamu namna ya kujiunga na kuchangia popote ulipo

Namna ya kujiunga kupitia mitandao ya simu;

1.⁠ ⁠Piga *152*00 #

2.⁠ ⁠Bonyeza 9 Ajira na Utambuzi

3.⁠ ⁠Bonyeza 6 NSSF

4.⁠ ⁠Bonyeza 1 Jisajili kisha fuata maelekezo

Namna ya kuchangia kupitia mitandao ya simu;

1.⁠ ⁠Piga *152*00 #

2.⁠ ⁠Bonyeza 9 Ajira na Utambuzi

3.⁠ ⁠Bonyeza 6 NSSF

4.⁠ ⁠Bonyeza 2 malipo

5.⁠ ⁠Bonyeza 2 mwanachama kisha fuata maelekezo

PUBLIC NOTICE: EXPRESSION OF INTEREST
01/09/2026

PUBLIC NOTICE: EXPRESSION OF INTEREST

PUBLIC NOTICE: SALES OF PARCEL OF LANDS
01/09/2026

PUBLIC NOTICE: SALES OF PARCEL OF LANDS

HONGERA MHE. DEOGRATIUS JOHN NDEJEMBIKwa kuteuliwa na kuapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaTu...
29/08/2026

HONGERA MHE. DEOGRATIUS JOHN NDEJEMBI

Kwa kuteuliwa na kuapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tunaahidi ushirikiano katika kutekeleza majukumu yako

Mawlid Al Nabi Mubarak
25/08/2026

Mawlid Al Nabi Mubarak

RAIS DKT. SAMIA AIKABIDHI NSSF CHETI CHA SHUKRANI KWA MCHANGO WAKE KATIKA TAMASHA LA KIZIMKAZI 2026Rais wa Jamhuri ya Mu...
14/08/2026

RAIS DKT. SAMIA AIKABIDHI NSSF CHETI CHA SHUKRANI KWA MCHANGO WAKE KATIKA TAMASHA LA KIZIMKAZI 2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 14 Agosti 2026, amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba, Cheti cha Shukrani kwa kutambua ushiriki na mchango wa NSSF katika Tamasha la Kizimkazi 2026.

Cheti hicho ni ishara ya kutambua mchango wa NSSF katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza maendeleo ya taifa, kuimarisha ustawi wa wananchi na kuendeleza sekta ya hifadhi ya jamii.

Aidha, ushiriki wa NSSF katika tamasha hilo unaakisi dhamira ya Mfuko ya kuendeleza ujumuishaji wa wananchi waliojiajiri katika Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Hifadhi ya Jamii, fursa za kiuchumi na kijamii, sambamba na utekelezaji wa vipaumbele vya kitaifa vinavyoainishwa katika Dira 2050.

MWISHO

RAIS SAMIA AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA NSSFKizimkazi, Zanzibar.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Sul...
13/08/2026

RAIS SAMIA AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA NSSF

Kizimkazi, Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Tamasha la Kizimkazi, ambapo alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba.

Pamoja na kutembelea banda la Mfuko, Mhe. Rais alitembelea mabanda mengine ya taasisi na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa.

Mhe. Rais amefurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na NSSF hususan katika kuboresha huduma kwa wanachama.

Katika hatua nyingine, NSSF imeendelea kutekeleza wajibu wake kwa jamii katika maeneo ya elimu, afya, michezo, jamii, mahitaji maalum na wadau wa maendeleo. Katika tamasha la Kizimkazi, Mfuko umewajibika kwa jamii kupitia utoaji wa majiko janja (80L Electric Pressure Cooker) yanayotumia umeme kidogo sana wastani wa ‘units’ 2 kwa saa nzima , ni salama na yanajizima yakiivisha ambayo yametolewa kwa shule za sekondari sambamba na kushiriki, pamoja na wadau wengine wa maendeleo, katika Kongamano la Nishati Safi lililofanyika hapa Kizimkazi.

Utoaji wa majiko janja na ushiriki wa Mfuko kwenye Kongamano la Nishati safi ni hatua zinazoonesha dhamira ya NSSF ya kuunga mkono Ajenda ya Kitaifa ya Nishati Safi ya Kupikia, inayolenga kuongeza matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kuboresha afya, kulinda mazingira na kuchochea maendeleo endelevu.

NSSF YAKABIDHI MAJIKO JANJA KUUNGA MKONO AJENDA YA NISHATI SAFIMakunduchi, Zanzibar, Agosti 12, 2026 Mfuko wa Taifa wa H...
12/08/2026

NSSF YAKABIDHI MAJIKO JANJA KUUNGA MKONO AJENDA YA NISHATI SAFI

Makunduchi, Zanzibar, Agosti 12, 2026

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekabidhi majiko janja 10 katika Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja, kuunga mkono ajenda ya Serikali ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini.

Majiko hayo yanalenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, kulinda mazingira dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, kuboresha afya za wananchi na kuinua ustawi wa jamii.

Katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makunduchi, Mhe. Wannu Hafidhi Ameir, alipokea majiko hayo ambayo yatakabidhiwa katika shule za sekondari.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mhe. Wannu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF), aliishukuru NSSF na wadau wengine kwa kuunga mkono juhudi za taasisi hiyo katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi.

"Naamini huu ni mwanzo tu. Tutaendelea kushirikiana kuhakikisha kaya nyingi zaidi zinatumia nishati safi. Tunawashukuru NSSF na wadau wengine kwa kutambua umuhimu wa kushirikiana nasi katika kuwahudumia wananchi," alisema Mhe. Wannu.

Alisema msaada na vifaa vilivyotolewa na wadau mbalimbali vitawanufaisha wananchi wa Makunduchi na Wilaya ya Kusini kwa ujumla, ambapo madaftari yatagawiwa katika shule za msingi, vitabu vitapelekwa shule za sekondari, majiko ya gesi yatatolewa kwa vikundi vya wanawake, huku majiko janja yaliyotolewa na NSSF yakitarajiwa kuboresha huduma za upishi katika shule.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, alisema ushiriki wa Mfuko huo ni sehemu ya kuunga mkono ajenda ya Taifa ya matumizi ya nishati safi inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, sambamba na kuendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi, hususan waliojiajiri.

“NSSF inaamini kuwa matumizi ya nishati safi ni uwekezaji katika afya za wananchi, uhifadhi wa mazingira na maendeleo endelevu. Tumekabidhi majiko 10 k**a sehemu ya mchango wetu katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini,” alisema Bw. Mshomba.

Alieleza kuwa, pamoja na kukabidhi majiko hayo, NSSF imeendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi waliojiajiri kujiunga na kuchangia katika Mfuko kupitia Skimu ya Hifadhi, inayowawezesha kupata mafao mbalimbali ikiwemo pensheni ya uzee, pensheni ya ulemavu, pensheni ya urithi, mafao ya uzazi, matibabu na huduma nyingine zinazotolewa na Mfuko huo.

Bw. Mshomba alisema matumizi ya nishati safi yana mchango mkubwa katika kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, kulinda afya za wananchi dhidi ya madhara ya moshi unaotokana na matumizi ya nishati zisizo salama, kuhifadhi mazingira na kuboresha maisha ya jamii.

“Majiko haya ni mwanzo wa ushiriki wetu katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi. Tutaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanafikiwa na elimu pamoja na teknolojia ya nishati safi,” alisema.

Naye, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Reuben Kwagilwa, aliipongeza Taasisi ya MIF kwa kuandaa Tamasha la Kizimkazi, akisema limeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuhamasisha matumizi ya nishati safi na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.

Alisema juhudi hizo zinaendana na dira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuongeza matumizi ya nishati safi nchini na barani Afrika, huku akiwahimiza wananchi kuendelea kutumia teknolojia zinazolinda mazingira na kuboresha afya zao.

Ugawaji wa majiko hayo unaunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kupitia ushirikiano wa Taasisi za Serikali na Binafsi. NSSF na wadau mbalimbali wamekuwa mstari mbele kuunga mkono juhudi hizo huku wananchi wakiendelea kunufaika na elimu kuhusu hifadhi ya jamii na huduma zinazotolewa na Mfuko huo.

Address

P. O. Box 1322, Azikiwe Street
Dar Es Salaam
0255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NSSF Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share