ccm_katayakivukoni

ccm_katayakivukoni Page rasmi ya kuzungumza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa mwaka 2015 - 2020

Mechi ya watani wa jadi kutoka Soko la Kimataifa la Samaki ( Feri ) imelizika kwa Umoja Fc  kuifunga timu ya Kijiwe Sugu...
31/10/2024

Mechi ya watani wa jadi kutoka Soko la Kimataifa la Samaki ( Feri ) imelizika kwa Umoja Fc kuifunga timu ya Kijiwe Sugu Fc bao Moja kwa bila na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya mchezo wa beach soka katika Mashindano ya kombe la Mama Samia Ferry Fish Market.

Mashindano haya yaliyoandaliwa na Uongozi wa Soko Chini ya Meneja wa soko Ndg. Suleman Mfinanga na Mwenyekiti wa wadau Ndg. Mbaraka Kilima.

Akizungumza kocha wa timu ya Umoja Bw. Ronaldo mara baada ya kumalizika mechi amesema , "ushindi huu tuliutegemea kwasababu tulijiandaa vya kutosha kwenye uwanja wa mazoezi na wachezaji wangu wamefanya vizuri licha kupata kadi nyekundu moja ."

Naye Kapteni wa timu ya Umoja Fc Mohamed Hafidh amesema , "tumepata ushindi kwasababu tumefuata maelekezo ya kocha wetu japo kuwa watani wetu walikuwa wagumu lakini tunashukuru tumefanya vizuri na kufanikiwa kutinga hatua inayofuata . "

Mdau wa michezo kutoka Feri Bw. Athumani sanga amesema kuwa wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika mashindano haya kwasababu licha ya zawadi mbali mbali zinazoshindaniwa lakini pia michezo inaleta watu pamoja na kudumisha tamaduni ya kufanya mazoezi.

Mashindano haya bado yapo katika hatua ya makundi huku baadhi ya timu zikiwa zimefuzu hatua ya robo fainali.

CCM YAMJULIA HALI MUASISI WA TANU NA MPIGANIA UHURU MOIJumapili 16 Januari 2022 Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa I...
16/01/2022

CCM YAMJULIA HALI MUASISI WA TANU NA MPIGANIA UHURU MOI

Jumapili 16 Januari 2022 Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amemtembelea na kumjuilia hali ya maendeleo ya afya ya Mzee Rehan B. Waikela aliyelazwa katika taasisi ya mifupa Muhimbili (Moi) akipatiwa matibabu.

"Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake kinathamini na kujali kila mtu aliyejitoa na kujitolea kwa hali, mali, vitu, ujuzi na maarifa kufanikisha uhuru wa Nchi yetu na ukombozi wa Afrika. Mchango wao haupimiki wala hauwezi kuthaminishwa kwa chochote bali kwa kuwatambua, kuwajali na kuwatunza inaweza kuwa namna bora zaidi ya kutambua mchango wao.” Alisema Shaka.

Mzee Waikela amekuwa moja kati ya viongozi wa Chama cha TANU wakati huo ambaye alijitoa na kujitolea kwa hali na mali kuwapa ushirikiano wapigania Uhuru ili kufanikisha lengo hilo.

Historia inamtaja kuwa wakati viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, walipokuwa wakifika mkoani Tabora Mzee Waikela alikuwa akiwalaki kwa malazi, chakula na kuwapa huduma ya usafiri ili kuhamasisha harakati za Uhuru na Ujenzi wa Chama cha TANU wakati huo.

28/12/2021
16/10/2021

Address

Kivukoni
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ccm_katayakivukoni posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share