Mediawireexpress

Mediawireexpress Your News Hub for Uncovering Africa's untold narratives , one video at a time .

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, leo tarehe 15 Agosti, 2026 ameshuhudia zoezi la majaribio ya meli ya MV Liemba...
15/08/2026

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, leo tarehe 15 Agosti, 2026 ameshuhudia zoezi la majaribio ya meli ya MV Liemba katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma baada ya kukamilika kwa ukarabati wake mkubwa uliogharimu Shilingi bil 34

Akizungumza na wanahabari Prof. Mbarawa amesema ukarabati huo ulianza baada ya Serikali kumpata mkandarasi mwaka 2023 na kueleza kuwa kurejea kwa MV Liemba kutasaidia wananchi wa Kigoma, Katavi, Rukwa na maeneo mengine kupata huduma muhimu ya usafiri wa majini

Prof. Mbarawa amesema meli hiyo imefanyiwa maboresho makubwa, ambapo injini mbili, jenereta tatu, chumba cha uendeshaji pamoja na maeneo ya abiria vimefanyiwa maboresho na kuwekwa katika hali mpya

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha ukarabati huo, akisema lengo ni kuhakikisha MV Liemba inaendelea kutoa huduma kwa wananchi kwa miaka 50 na zaidi

Waziri Mbarawa amesema Serikali itaendelea kusimamia majaribio na ukaguzi wa kina, na baada ya kukamilika kwa taratibu zote, MV Liemba inatarajiwa kuanza kutoa huduma kwa wananchi kuanzia Septemba 1, 2026.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TASHICO Bw. Eric Hamissi amesema majaribio hayo ni muhimu katika kuhakikisha mifumo yote ya meli inafanya kazi kwa ufanisi na usalama kabla ya kuanza rasmi kutoa huduma kwa wananchi.

Naye Mha. Elias Kivara anayesimamia ukarabati na majaribio ya MV Liemba amesema majaribio hayo yanahusisha injini, jenereta, mfumo wa uendeshaji, kuongeza na kupunguza kasi pamoja na uwezo wa meli kusimama kwa wakati unaotakiwa.

15/08/2026

Kijana Salim Ali Chambega, maarufu kwa jina la Pacha, amesimulia jinsi alivyonusurika kifo baada ya tukio lililotokea ndani ya eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, wakati yeye na wenzake wawili wakielekea Babati kuhudhuria msiba.

Kwa mujibu wa maelezo yake, vijana hao watatu walikuwa wakisafiri kwa pikipiki moja kabla ya kupotea njia na kujikuta katika barabara inayoelekea Ngorongoro, ambako walikutana na askari wa hifadhi ambao wanadaiwa kuwapa adhabu kali.

Tukio hilo liliwaacha vijana hao na majeraha, huku mmoja wao, Sefu M***a, akipoteza maisha. Pacha alijeruhiwa vibaya na baadaye kupelekwa katika Hospitali ya Lutheran, Karatu, akiwa katika hali mbaya na akiwa amepoteza fahamu.

Madaktari walifanya jitihada za kuokoa maisha yake kwa kumpatia matibabu ya dharura, ikiwemo oksijeni, kabla hali yake kuanza kuimarika.

Mwenzake, Abdallah, pia anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu, huku Sefu akizikwa jana jijini Arusha.

Tukio hilo limeacha simanzi kwa familia, ndugu na marafiki, wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa mazingira ya tukio hilo ili kubaini kilichotokea na kuwachukulia hatua watakaobainika kuhusika.

15/08/2026

Vijana mbalimbali wamejitokeza katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha, kwa ajili ya kumuaga na kumsindikiza katika safari yake ya mwisho kijana mwenzao aliyefariki dunia siku mbili zilizopita katika tukio lililotokea eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Kwa mujibu wa maelezo ya wenzake, kijana huyo alikuwa akisafiri pamoja na wenzake wawili kuelekea Babati kwa ajili ya kuhudhuria msiba, lakini walipoteza njia na kujikuta wakielekea upande wa Ngorongoro. Katika mazingira ambayo bado yanachunguzwa, kijana huyo alipoteza maisha huku wenzake wakijeruhiwa.

15/08/2026

Familia ya Jason Arday imetoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Profesa wa Chuo Kikuu cha Cambridge baada ya kupatikana amefariki katika nyumba moja jijini London siku ya Ijumaa.

Arday, ambaye aliwahi kuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Cambridge, alikutwa amefariki katika eneo hilo huku taarifa zaidi kuhusu mazingira ya kifo chake zikisubiriwa kutoka kwa mamlaka husika.

Familia yake imetoa salamu za maombolezo, ikimkumbuka kwa mchango wake katika taaluma na jamii.

Taarifa zaidi kuhusu chanzo cha kifo chake na uchunguzi wa polisi zinatarajiwa kutolewa kadiri uchunguzi unavyoendelea.

15/08/2026

China imezindua teknolojia mpya inayotumia mionzi ya laser kulenga na kuangamiza mbu wakiwa angani.

Teknolojia hiyo inalenga kusaidia kudhibiti idadi ya mbu na kupunguza hatari ya magonjwa yanayoenezwa na wadudu hao.

Mfumo huo hutumia teknolojia ya kutambua mbu na kuelekeza mionzi ya laser kwa usahihi, huku ukilenga wadudu hao bila kuhitaji matumizi makubwa ya kemikali.

Teknolojia hiyo inaelezwa kuwa sehemu ya juhudi za kutumia ubunifu wa kiteknolojia katika udhibiti wa wadudu na kulinda afya ya jamii.

15/08/2026

Korea Kaskazini imetishia kutoa jibu “kubwa na la kushtukiza” iwapo Marekani na Korea Kusini vitaendelea na mazoezi yao ya pamoja ya kijeshi, kwa mujibu wa KCNA.

Pyongyang imesema mazoezi hayo yanayotarajiwa kuanza Agosti 17, 2026, si ya kujihami pekee k**a yanavyoelezwa na washirika hao, bali ni ya uchokozi yanayolenga kujiandaa kwa vita dhidi ya Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini imedai kuwa mazoezi hayo yanaiga mazingira ya vita vya kisasa, ikiwemo matumizi ya ndege zisizo na rubani, operesheni za kielektroniki na mashambulizi ya kimtandao.

Pyongyang imeonya kwamba hatua hiyo inaweza kuongeza mvutano katika Rasi ya Korea na kwamba itachukua hatua za kijeshi kujibu kile inachokiona k**a tishio kwa usalama wake.

Marekani na Korea Kusini kwa upande wao zimekuwa zikisema mazoezi yao ya pamoja ni sehemu ya maandalizi ya kijeshi na kuimarisha uwezo wa kujilinda dhidi ya vitisho vinavyoweza kujitokeza kutoka Korea Kaskazini.

Video: Mazoezi ya Pamoja ya Kijeshi ya Marekani na Korea Kusini, Machi 2026

15/08/2026

Wafuasi wa Taliban nchini Afghanistan wamejitokeza kusherehekea miaka mitano tangu kundi hilo lilipochukua tena madaraka nchini humo tarehe 15 Agosti 2021.

Sherehe hizo zimefanyika katika maeneo mbalimbali, huku viongozi wa Taliban wakisifu kile wanachokiita kurejea kwa utulivu na kumalizika kwa miongo kadhaa ya mapigano nchini Afghanistan. Kabul pia imekuwa na matukio ya umma na maandamano ya kuadhimisha siku hiyo.

Hata hivyo, maadhimisho hayo yamefanyika wakati Afghanistan ikiendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za kibinadamu na kiuchumi. Mashirika ya misaada yameonya kuhusu ongezeko la mahitaji ya kibinadamu, huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu vikwazo vinavyoendelea kuwaathiri wanawake na wasichana, wakiwemo kuzuiwa kwa wasichana walio na umri wa zaidi ya miaka 12 kupata elimu.

Taliban ilitwaa Kabul tarehe 15 Agosti 2021 baada ya vikosi vya Marekani na washirika wake kuondoka Afghanistan, na tangu wakati huo imekuwa ikiongoza nchi hiyo k**a mamlaka ya Islamic Emirate of Afghanistan.

Licha ya sherehe hizo, serikali ya Taliban bado haijatambuliwa rasmi na nchi nyingi duniani, huku Urusi ikiwa nchi pekee iliyotajwa kuwa imetambua rasmi serikali hiyo.

15/08/2026

Marekani na Iran wamekwama katika mzozo wa muda mrefu ambao, kwa mujibu wa Bloomberg, hakuna upande unaoonekana kujua namna ya kupata ushindi wa mwisho.

Baada ya karibu miongo mitano ya uhasama kati ya mataifa hayo mawili, mvutano wao umeingia katika mzozo wa muda mrefu ambao sasa umechukua takribani miezi sita.

Bloomberg imesema kuna dalili chache zinazoonyesha kwamba mzozo huo unakaribia kumalizika, huku pande hizo zikiendelea kukabiliana licha ya gharama kubwa za kisiasa, kiuchumi na kijeshi.

Mzozo huo umeongeza wasiwasi kuhusu uwezekano wa mapigano kuendelea kwa muda mrefu na kusababisha athari zaidi katika Mashariki ya Kati.

Video: CENTCOM

15/08/2026

Mchumi Mkuu wa zamani wa Benki ya Dunia ameeleza kwa nini utandawazi na utegemezi wa kiuchumi kati ya mataifa huenda visiweze kuzuia kutokea kwa Vita vya Tatu vya Dunia.

Amesema kwa muda mrefu kulikuwa na mtazamo uliokubalika na watu wengi kwamba utandawazi, biashara na utegemezi wa kiuchumi kati ya nchi vingefanya vita kuwa jambo ambalo ni karibu kutowezekana.

Kwa mujibu wake, hoja hiyo ilijengwa kwenye dhana kwamba hasara za kiuchumi ambazo nchi zingepata kutokana na vita zingekuwa kubwa kiasi cha kuzifanya nchi kuepuka migogoro, kwa kuwa zingekuwa na manufaa makubwa zaidi kupitia biashara, mauzo na ushirikiano.

Hata hivyo, amesema nadharia hiyo ilikuwepo hata kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia, huku mataifa yakifahamu kwamba vita vingekuwa na madhara makubwa kwa uchumi wao.

Amehoji kwa nini, licha ya dunia kuwa katika kilele cha utandawazi na ushirikiano wa kiuchumi kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia, bado vita vilitokea.

Amesema jambo hilo limekuwa changamoto kwa wachumi kulieleza kwa sababu kwa mtazamo wa kiuchumi, vita havikupaswa kutokea katika mazingira ambayo mataifa yalikuwa yameunganishwa kwa kiwango kikubwa kupitia biashara na ushirikiano.

“Kwa kweli, wachumi hawana maelezo ya kutosha kwa sababu katika ulimwengu wa kiuchumi, hili halikupaswa kutokea,” alisema.

Ameonya kwamba hali ya sasa inaonyesha mfanano fulani na kipindi hicho cha historia. Dunia iko mwishoni mwa kipindi kirefu cha utandawazi, huku uwiano wa biashara dhidi ya Pato la Taifa (GDP) ukifikia kiwango cha juu kabla ya janga la COVID-19.

Wakati huohuo, amesema mazingira ya kisiasa duniani kwa sasa ni mabaya zaidi kuliko kipindi chochote tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia.

“Kwa mtazamo wa kiuchumi, mambo haya mawili hayapaswi kwenda pamoja, lakini katika ulimwengu halisi yanaenda pamoja,” alieleza.

Maelezo hayo yanaibua mjadala kuhusu iwapo utegemezi wa kiuchumi pekee unaweza kuwa kinga ya kutosha dhidi ya migogoro mikubwa ya kimataifa, hasa wakati mvutano wa kisiasa na kijeshi kati ya mataifa makubwa unapoendelea kuongezeka.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba  leo Agosti 15, 2026 ameendelea kutatua  kwa njia ya maridhiano migogoro sugu  inayowak...
15/08/2026

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Agosti 15, 2026 ameendelea kutatua kwa njia ya maridhiano migogoro sugu inayowakabili wananchi na mara hii ametatua mgogoro wa ardhi kati ya Bi. Alia Shariff na Bi Devotha Delfina Elisei uliodumu miaka 28 katika eneo la Goba jijini Dar es salaam .

Bi. Alia Shariff, mkazi wa Dar es Salaam, alimwandikia barua Mheshimiwa Waziri Mkuu tarehe 20 Januari 2026, akiomba amsaidie kutatua mgogoro huo na katika barua hiyo, alieleza kuwa eneo analolalamikia limemilikiwa na wanae tangu mwaka 1998 na kwa muda wote huo ametafuta suluhu ya jambo hilo bila mafanikio.

Waziri Mkuu alituma Timu ya Watalaam kutoka Ofisini kwake ikiongozwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Msaidizi wa Waziri Mkuu – Mahusiano, Asasi za Kiraia na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Bw. Tryphone Mkolokoti, na Katibu wake ambaye pia ni Msaidizi wa Waziri Mkuu – Masuala ya Ardhi, Bw. Senso Magessa ambayo ilishirikiana na Kamishina Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es salaam, Shukuruni Kyando, Watalaam wa Ardhi Manispaa ya Kinondoni pamoja wa viongozi wa Kata na Mtaa wa Goba lilipo eneo lenye mgogoro.

Timu iliitisha vikao vya usuluhishi na kutembelea eneo la mgogoro vilivyowahusisha Watalaam wa masuala ya ardhi Mkoa wa Dar es salaam na wilaya ya Kinondoni, majirani na wazee walioishi miaka mingi pamoja na wapima ardhi ambao walihakiki na kubainisha mipaka halali ya viwanja Namba 202, 203, 204 na 205, vilivyopo Goba, jijini Dar es Salaam vilivyokuwa na mgogoro.

Baada ya uchambuzi wa nyaraka, maelezo ya pande mbili zilizohuka katika mgogoro huo na upimaji uliofanywa imebainika kuwa uamuzi wa Mahak**a umeelekeza kuwa kiwanja Na. 202 chenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 3,000 ambapo Devota anamiliki mita za mraba 1,000 ndicho kiini cha mgogoro.

Pande zote mbili zimekubaliana kuheshimu hukumu, amri na maamuzi halali ya Mahak**a, pamoja na kufuata taratibu zinazotakiwa na mamlaka za ardhi katika kubainisha na kutekeleza haki za kila upande na kuepuka vitendo vinavyoweza kuibua mgogoro tena.

Nayo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imeelekezwa kusimamia na kuhakikisha Ofisi ya Ardhi ya Wilaya ya Kinondoni inakamilisha haraka taratibu za kitaalamu za kugawa kiwanja Na. 202 ambacho ni kiini cha mgogoro kwa mujibu wa maamuzi ya Mahak**a na makubaliano yaliyofikiwa katika maridhiano hayo.

Utiaji saini nyaraka za maridhiano hayo ulifanyika kwenye eneo lililokuwa na mgogoro

Goba jijini dar es salaam na kushuhudiwa na Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Mkoa wa Dar es salaam, Shukuruni Kyando, Watalaam wa Ardhi Manispaa ya Kinondoni na Mkoa wa Dar es salaam, Watalaamu kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Viongozi wa eneo la Goba na wananchi.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dar es salam Shukuruni Kyando alitumia fursa hiyo kutoa elimu ya namna sahihi na ya haraka ya kubatilisha hati miliki ya ardhi na kupata hati mpya na halali katika maeneo yenye migogoro ambayo utatuzi wake ulisababisha kiwanja hicho kugawanywa kwa mmiliki zaidi ya mmoja.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amedhamiria kutatua baadhi ya migogoro inayowakabili wananchi kwa maridhiano yanayoendeshwa na Timu yake ya Watalaam aliyoiagiza kufanya kazi hiyo kwa kuzingatia maamuzi ya vyombo vya sheria, taratibu, kanuni na utu. Hatua hiyo imewafanya wananchi wengi kumwandikia barua za malalamiko yao na kujitokeza kwa wingi kutoa kero zao katika mikutano anayoihutubia.

Address

Samora Avenue
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mediawireexpress posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Mediawireexpress:

Shortcuts

Share