TPATZ Main functions of TPA is to promote the use, development & management of Ports and their hinterlands.

The Tanzania Ports Authority (TPA) was established by the Ports Act No. 17 of 2004 as landlord port authority. It operates a system of ports serving the Tanzania hinterland and the land-linked countries of Zambia, Democratic Republic of Congo (DRC), Burundi, Rwanda, Malawi, Uganda and Zimbabwe. The Authority performs the role of landlord and operator with the main functions of promoting the use, d

evelopment and management of the ports and their hinterlands, entering contracts for the purpose of delegating the powers of the Authority through licensing and concessions for port services. The TPA manages a diverse system of sea and inland waterways on Tanzania's Mainland. Dar es Salaam, Tanga, and Mtwara are the major seaports; Kilwa, Lindi, Mafia, Pangani, and Bagamoyo are the smaller seaports; and Lake Victoria, Tanganyika, and Nyasa are the lake ports.

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema ujenzi wa Gati Jipya la Abiria katika Bandari ya Kigoma utakuwa chachu...
16/08/2026

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema ujenzi wa Gati Jipya la Abiria katika Bandari ya Kigoma utakuwa chachu ya kukuza biashara na kuimarisha usafiri kwa njka ya maji katika ukanda wa Ziwa Tanganyika

Prof. Mbarawa ameyasema hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa gati hilo, ambalo linajengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan kupitia ruzuku, huku ujenzi wake ukiwa umeanza tangu Juni,2025

Amesema mradi huo wenye thamani ya Shilingi bil. 53, utakapokamilika utaimarisha usafirishaji wa abiria na mizigo, kuongeza usalama wa huduma za usafiri kwa njia ya maji na kuchochea shughuli za kiuchumi katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa, pamoja na nchi jirani

“Tunajenga meli, tunakabati bandari na tunajenga reli ili kuhakikisha mifumo yote ya uchukuzi inaunganishwa na kuleta tija kiuchumi,” amesema Prof. Mbarawa

Gati hilo litakuwa na urefu wa mita 130, upana mita 50, Mradi huo pia utahusisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa mita 481 kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma hadi eneo la gati

Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya uchukuzi ili kuifanya Kigoma kuwa lango muhimu la biashara na shughuli za kiuchumi katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika na Ukanda wa Maziwa Makuu

Kwa upande wake, Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Bw. Ernest Mabula, amesema kukamilika kwa gati hilo kutaboresha ufanisi na usalama wa huduma za usafiri kwa njia ya maji, kuongeza usafirishaji wa abiria na mizigo na kukuza biashara katika ukanda huo

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dkt. Rashid Chuachua, ameishukuru Serikali kwa uwekezaji huo, akisema gati hilo litachochea ukuaji wa uchumi, kuongeza fursa za biashara na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi.

Meneja wa Bandari, Bw. Salehe Mbega amesema kuwa, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania itaendelea kufanya maboresho ...
15/08/2026

Meneja wa Bandari, Bw. Salehe Mbega amesema kuwa, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania itaendelea kufanya maboresho katika Bandari ya Tanga ili kuweza kuhudumia meli nyingi na shehena kubwa zaidi.

Mbega amesema hayo wakati wa Kikao cha Wadau wa Bandari ya Tanga (PIC). Meneja huyo amesema maboresho hayo ni pamoja na ujenzi gati moja yenye urefu wa mita 300 nambalo litakuwa maalum kwa ajili ya meli za makasha.

Pia katika maboresho hayo TPA itanunua vifaa mbalimbali vya kuhudumia shehena za mizigo. Lengo ni kuongeza ufanisi wa huduma na uwezo wa bandari kuhudumia wateja wake kwa tija zaidi.

Aidha Mbega amewashukuru Wadau wa Bandari ya Tanga kwa ushirikiano na umoja katika kuwahudumia wateja. Amesema hali hiyo imeijengea taswira bora bandari na kuifanya bandari hiyo kuendelea kuwavutia wateja.

Kamati ya Maboresho ya Bandari ya Tanga hukutanisha wadau wa bandari ambao ni pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali na makampuni ya uwakala wa meli na forodha ili kujadili changamoto zinazokabili bandari na kutafuta suluhisho kwa pamoja.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Dkt. James Peter Mataragio ameipongeza TPA kwa utekelezaji...
15/08/2026

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi Dkt. James Peter Mataragio ameipongeza TPA kwa utekelezaji wa mradi na ameridhika na kasi ya ujenzi wa matanki ya uhifadhi na usambaji wa mafuta uliopo kigamboni.

Amesema hayo leo tarehe 14 Agosti, 2026 wakati wa ziara yake ya siku moja katika mradi wa ujenzi wa matanki 15 ya mafuta uliopo kigamboni jijiniDar es Salaam.

Amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utaenda kuongeza ufanisi wa Bandari katika kuhudumia meli za mafuta na kuongeza wateja na mapato kwa wakati.

Aidha ameitaka TPA kuhakikisha Ujenzi wa matanki hayo kwenda sanjari na Ujenzi wa miundombinu ya uondoshaji wa mafuta ili pale utakapokamilika kazi ya kuhudumia meli kuanza maramoja.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw. Plasduce M. Mbossa ameishukuru Wizara Nishati kwa ushirikiano na TPA katika utekelezaji wa mradi huo ambao unatazamiwa kukamilika ifikapo machi 2027.

Pamoja na shukrani hizo Bw. Galus amemhakikishia kuwa mradi huo utakapokamilika utaenda kuboresha muda wa kuhudumia meli kuingia na kutoka “Turn around Time “ kutoka siku nane (8) mpaka siku mbili (2) kuifanya Bandari ya Dar e salaam kuhudumia meli nne za mafuta ndani ya siku nane.

Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu Dkt. James Mataragio alipata fursa ya kutembelea Mita za kupima mafuta “flow Meter” yanayopakuliwa kutoka Boya la Mafuta la (SPM ) lililopo Mjimwema ,Kigamboni baadae kumalizia ziara yake Kampuni ya ubia inayoifadhi mafuta nchini “Tanzania International Petroleum Reserves Limited” (TIPER ) iliyopo Kigamboni.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepongezwa kwa hatua mbalimbali inazochukua katika kuboresha miundombinu...
15/08/2026

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepongezwa kwa hatua mbalimbali inazochukua katika kuboresha miundombinu na kuongeza ufanisi wa huduma za bandari nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati kutoka Wizara ya Shirikisho ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Joachim Schmitt, alipoongoza ujumbe wa Serikali ya Ujerumani katika kikao na Menejimenti ya TPA kilicholenga kujadili fursa za ushirikiano wa kimaendeleo baina ya Tanzania na Ujerumani.

Bw. Schmitt amesema kuwa anaona maendeleo makubwa katika utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam, akieleza kuwa kasi ya maboresho yaliyofanyika ni ya kuvutia na inastahili pongezi kwa Menejimenti ya TPA.

“Bandari ya Dar es Salaam imekuwa kwa kiwango cha kuvutia, na kwa hilo napenda kuipongeza Menejimenti ya TPA,” alisema Bw. Schmitt.

Akitoa salamu za awali kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mkurugenzi wa Mipango, Ubora na Vihatarishi, Dkt. Boniphace Nobeji, amesema TPA imejipanga kuendelea kuimarisha miundombinu ya bandari zake ili kuongeza uwezo na ufanisi katika kuhudumia shehena.

Dkt. Nobeji amesema maboresho yaliyofanyika katika bandari mbalimbali nchini yamechangia kuongezeka kwa shehena inayohudumiwa, akitolea mfano Bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ambazo zimeendelea kuimarika kiutendaji na kuongeza uwezo wa kuhudumia mahitaji ya wafanyabiashara na watumiaji wa bandari.

Aidha, Dkt. Nobeji ameeleza kuwa TPA inaendelea na maboresho ya Bandari za Kisiwa Mgao, Mbamba Bay na Kigoma, hatua inayotarajiwa kuongeza uwezo wa bandari hizo na kufungua fursa zaidi za biashara na usafirishaji, hususan katika masoko ya ndani na ya kikanda.

Amesema maboresho hayo ni sehemu ya mkakati mpana wa Serikali wa kuimarisha miundombinu ya usafirishaji na kuiwezesha Tanzania kutumia kikamilifu nafasi yake ya kimkakati k**a lango la biashara kwa nchi jirani zisizo na bandari.

Kikao hicho pia kilitoa fursa kwa pande hizo kujadili maeneo ya ushirikiano wa kimaendeleo, hususan katika kuimarisha miundombinu, ufanisi wa huduma za bandari na kuongeza mchango wa sekta ya bandari katika kukuza biashara na uch

          PortLogistics TradeFacilitation MaritimeTransport Logistics SmartPorts PortOfDarEsSalaam TanzaniaPorts Gateway...
14/08/2026

PortLogistics TradeFacilitation MaritimeTransport Logistics SmartPorts PortOfDarEsSalaam TanzaniaPorts GatewayToTrade EfficientPorts MovingTrade ConnectingMarkets TradeGateway Tanzania EastAfrica AfricaTrade

11/08/2026

Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) ameipongeza ...
10/08/2026

Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) ameipongeza TPA kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika Bandari ya Tanga, ambayo yameongeza ufanisi na kuvutia shehena zaidi na meli kubwa za moja kwa moja kutoka masoko ya kimataifa.

Prof. Kabudi ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea Banda la Bandari ya Tanga katika Maonesho ya Nanenane 2026 Kanda ya Mashariki, yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Morogoro.

Aidha, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uwekezaji mkubwa katika uboreshaji wa Bandari ya Tanga, akibainisha kuwa uwekezaji huo umeendelea kuleta matokeo chanya kiuchumi, ikiwemo kuongezeka kwa shehena na mapato ya Bandari na Serikali kwa ujumla.

Akieleza kuhusu ushiriki wa TPA katika maonesho hayo, Bw. Peter Millanzi, kwa niaba ya Meneja wa Bandari, amesema lengo ni kuwaelimisha na kuwahamasisha wakulima kutumia fursa za bandari kuagiza pembejeo na kusafirisha mazao yao kwenda masoko ya nje ya nchi, sambamba na msisitizo wa Serikali wa kukuza kilimo cha biashara.

Milanzi pia amesema Bandari ya Tanga imevuka malengo iliyokuwa imewekewa katika mwaka wa fedha uliopita (2025/26), ikiwa ni miongoni mwa matokeo chanya yanayoendelea kuonekana kutokana na maboresho yaliyofanyika katika bandari hiyo.

Wadau mbalimbali wanaohusika na shughuli za kibandari wametumia ipasavyo ushiriki wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tan...
08/08/2026

Wadau mbalimbali wanaohusika na shughuli za kibandari wametumia ipasavyo ushiriki wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika Maonesho ya 33 ya Kimataifa ya Wakulima yaliyofanyika katika Viwanja vya Dkt.John Malecela jijini Dodoma, kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo sekta hiyo na Uchukuzi kwa ujumla.

Sehemu kubwa ya Wadau hao ni wakuu wa Taasisi, Wafanyabiashara, wafanyabiashara, Wasafirishaji wa mazao, malighafi na zana za kilimo.

TPA imetumia ushiriki wake katika Maonesho haya ya Wakulima kuonyesha namna inavyohudumia shehena mbalimbali na jinsi ilivyojipanga kutekelza Dira 2050 hususani katika kichocheo cha Usafirishaji fungamanishi ambapo Serikali imeeleza dhamira yake ya kuunganisha Bandari na reli za kisasa ili kuongeza ufanisi katika sekta ya Uchukuzi nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, amesema Serikali imejipanga kuhakikisha sehemu kubwa ya mizig...
08/08/2026

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, amesema Serikali imejipanga kuhakikisha sehemu kubwa ya mizigo inayopita katika Bandari za Tanzania inasafirishwa kwa njia ya reli.

Amesema hatua hiyo inalenga kuongeza ufanisi, kupunguza gharama za usafirishaji na kuwawezesha wafanyabiashara pamoja na wakulima kupata huduma bora na nafuu za usafirishaji.

Prof. Kahyarara amesema hayo wakati akihitimisha ziara yake katika mabanda ya Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake yanayoshiriki Maonesho ya Nane Nane 2026 yanayoendelea katika Viwanja vya John Malecela, Dodoma.

Amesema Serikali, kupitia TPA na TRC, inaendelea kuunganisha kwa ufanisi huduma za bandari na reli ili mizigo inayowasili bandarini iweze kusafirishwa kwa haraka na gharama nafuu kwenda maeneo mbalimbali nchini na nchi jirani.

Katika usafiri wa majini, Prof. Kahyarara amesema Serikali imeendelea kuimarisha miundombinu katika Ukanda wa Magharibi, hususan Kigoma, kupitia ujenzi wa miundombinu mipya ya bandari, uzinduzi wa meli mpya za mizigo na ukarabati mkubwa wa MV Liemba, ambayo imeanza majaribio kabla ya kurejea kutoa huduma.

Hatua hizi zinaendelea kuimarisha nafasi ya Tanzania k**a kitovu cha usafirishaji na biashara katika Afrika Mashariki na Kati.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah M***a Mwaipaya,  ameipongeza Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanza...
08/08/2026

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah M***a Mwaipaya, ameipongeza Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) kwa kuimarisha miundombinu ya Bandari ya Mtwara, inayochangia kuongeza uwezo wa Bandari hiyo katika uhudumiaji wa shehena ikiwemo za mazao ya biashara.

Mhe. Mwaipaya amesema hayo alipotembelea banda la TPA katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini ambayo yanafanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Aidha, Mhe. Mwaipaya amesema uwekezaji wa miundombinu ya Bandari na ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kuhudumia shehena ni vitu ambavyo Wilaya ya Mtwara inajivunia kwa kuwa umechangia kuhudumia kwa ufanisi zao la korosho.

TPA inatumia jukwaa la Maonesho ya Nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, katika kuonesha uhusiano uliopo baina ya shughuli za kibandari na Sekta ya Kilimo Nchini.

Address

P. O. Box 9184 DSM
Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TPATZ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share