22/04/2024
UBUNGO YAADHIMISHA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANZANIA
Tukielekea katika maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania tarehe 26/4/2024 Ubungo imefanya kongamano la kuliombea taifa katika ukumbi wa Noble hall uliopo Kimara Leo tarehe 22 April,2024
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na kauli mbiu isemayo, "Miaka 60 ya Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania,Tumeshikamana na Tumeimarika, kwa maendeleo ya Taifa letu.
Akifungua kongamano hilo Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ambaye pia ni Katibu Tawala Wilaya hiyo Hassan Mkwawa amesema kuwa, vijana wanajukumu la kuenzi Muungano kwa kuhakikisha wanafata yote ambavyo wazee wetu waliyafanya
Aliendelea kueleza kuwa,toka waasisi wetu walivyosimamia Muungano huu ambao taifa linaenda kusherekea siku hiyo ifikapo tarehe 26/4/2024 ambayo ni siku muhimu ni jukumu la Kila mtanzania kuulinda na kuuenzi Muungano.
Aidha, akitoa historia fupi toka Muungano ulivyofanyika na mpaka Sasa ambapo taifa linaenzi Muungano huo luteni kanali mstaafu Ali Shamte amesema kuwa, watanzania tunapaswa kujivunia Muungano wetu na kuulinda na tunapaswa kushikana kwa pamoja kudumisha Muungano huu
Wazee waliokuwepo kipindi Cha muungano wanaelewa faida zake na moja nikuleta umoja,mshikamano na pia ulinzi.alisema Shamte
Nae, kanali mstaafu Massanja Sunday ambaye ni msemaji Taasisi ya kizalendo Tanzania (TPO) amesema kuwa, Muungano unapaswa kuendelea kulindwa, tunapaswa kujivunia Muungano huu ambao sasaivi watu wote tunaweza kukutana na kukaa pamoja na kila mmoja akawa na amani
Wazanzibar wanakaa bara na sisi tunaenda zanzibar na kila mmoja ana amani katika eneo la mwenzie, amani imetawala baina yetu
"Asitokee mtu akatamani kuuvunja Muungano wetu" amesisitiza