ACT Baraza Kivuli

ACT Baraza Kivuli Official Account of the
ACT Wazalendo Shadow Cabinet Research Office (SCaRO) under the office of the Party Leader
Zitto Kabwe
and Shadow PM Dorothy Semu

MTUTURA:  SERIKALI ISITISHE VIBALI VYA BANDARI KAVUWaziri Kivuli wa Ujenzi, Uchukuzi na Miundombinu wa ACT Wazalendo, Mt...
30/08/2026

MTUTURA: SERIKALI ISITISHE VIBALI VYA BANDARI KAVU

Waziri Kivuli wa Ujenzi, Uchukuzi na Miundombinu wa ACT Wazalendo, Mtutura Abdallah Mtutura, ameitaka Serikali kusitisha mara moja utoaji wa vibali vipya vya Bandari Kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam, huku bandari kavu zilizopo zipatiwe muda wa miezi sita kusitisha huduma zinazofanyika katikati ya jiji, pembezoni mwa barabara na maeneo yanayosababisha usumbufu kwa wananchi.

Akizungumza leo tarehe 30 Agosti 2026 na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo, Mtutura amesema ongezeko la Bandari Kavu katika maeneo ya makazi na pembezoni mwa barabara limekuwa likisababisha madhila kwa wananchi, ikiwemo msongamano wa magari, uharibifu wa miundombinu na changamoto za usalama, huku likidhoofisha uchumi wa Dar es Salaam.

Mtutura amesema Bandari Kavu (ICDs) zimekuwa na uhusiano na wafadhili wa CCM pamoja na baadhi ya vigogo wa Serikali, akidai kuwa mfumo huo umetengeneza mwanya wa watu wenye maslahi binafsi kuunganisha biashara za bandari na kampuni zao za usafirishaji wa mizigo kwa lengo la kujipatia faida.

“Bandari kavu (ICDs) zina mizizi ya wafadhili wa CCM na vigogo wa Serikali ambao wametengeneza mwanya wa Bandari na makampuni yao ya usafirishaji wa mizigo ili kujipatia faida huku wakiacha madhila makubwa kwa wananchi na kudhoofisha uchumi wa Dar es Salaam,” amesema Mtutura.

Mtutura ameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kwa kusitisha utoaji wa vibali vipya vya Bandari Kavu, kufanya mapitio ya maeneo yote yenye ICDs na kuwapa waliopo muda wa miezi sita kuondoa shughuli hizo katika maeneo ya katikati ya jiji, pembezoni mwa barabara na maeneo yasiyokidhi vigezo vya mipango miji.

Chama cha ACT Wazalendo  kupitia Waziri Kivuli wa Habari, Shangwe Ayo  tumelaani kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi kwa...
20/08/2026

Chama cha ACT Wazalendo kupitia Waziri Kivuli wa Habari, Shangwe Ayo tumelaani kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi kwa kipindi cha miezi sita.

Wito wetu
Tumeitaka Serikali isimamishe mara moja adhabu hiyo kwa Mwanahalisi na irudishe leseni yake.

19/08/2026

"Hatutaki Katiba itakayoibeba CCM, tunataka Katiba ya wote kwa maslahi ya wote."

Kiongozi wa ACT Wazalendo
Dorothy Semu

Wito wetu ACT Wazalendo kufuatia kuk**atwa na kushikiliwa kwa Wakili Peter Madeleka.Kuk**atwa kwa wakili akiwa katika ma...
16/08/2026

Wito wetu ACT Wazalendo kufuatia kuk**atwa na kushikiliwa kwa Wakili Peter Madeleka.

Kuk**atwa kwa wakili akiwa katika majukumu yake ni tishio kwa uhuru wa kitaaluma wa mawakili, ukiukwaji wa wazi wa sheria zinazotoa uhuru wa kujieleza na wananchi kupata habari.

Kwa hivyo tumelitaka Jeshi la Polisi kumwachia huru Wakili Madeleka bila masharti yoyote ili aendelee kutekeleza majukumu yake.

TAARIFA KWA UMMA"Tunalitaka Jeshi la Polisi Limuachie huru Wakili Peter Madeleka."Waziri Mkuu Kivuli wa  Isihaka Mchinji...
15/08/2026

TAARIFA KWA UMMA

"Tunalitaka Jeshi la Polisi Limuachie huru Wakili Peter Madeleka."

Waziri Mkuu Kivuli wa
Isihaka Mchinjita

Wasemavyo ACT Wazalendo kufuatia ukatili kwa vijana watatu huko hifadhini Ngorongoro na kupelekea kufariki mmoja wao. Wi...
15/08/2026

Wasemavyo ACT Wazalendo kufuatia ukatili kwa vijana watatu huko hifadhini Ngorongoro na kupelekea kufariki mmoja wao.

Wito Wetu

1. Tumetaka familia ya marehemu ilipwe fidia na vijana wengine wawili watibiwe kwa gharama za Serikali na wao pia walipwe fidia

2. Tumetaka askari wa hifadhi waliofanya ukatili huu wachukuliwe hatua kali za kisheria

3. Waziri wa Maliasili na utalii Ndg. Ashatu Kijaji (Mb), Kamishna wa Uhifadhi wa Mmalaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Ndg. Abdul Razaq Badru wajiuzulu maramoja au mamlaka za uteuzi zitengue uteuzi wao k**a sehemu ya uwajibikaji kufuatia matukio ya mauaji yanayofanywa na ofisi zao.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AJIUZULU KUFUATIA MAUAJI YA KIJANA YALIYOFANYWA NA ASKARI WA HIFADHI YA TAIFA YA NGORONGOR...
14/08/2026

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AJIUZULU KUFUATIA MAUAJI YA KIJANA YALIYOFANYWA NA ASKARI WA HIFADHI YA TAIFA YA NGORONGORO

ACT Wazalendo tunalaani vikali matukio yaliyoota mizizi ya askari wa hifadhi mbalimbali nchini kufanya vitendo vya kinyama kwa raia na wananchi ikiwa ni pamoja na kuwatesa, kuwadhalilisha na kuwaua kikatili. Tukio la Agosti 12, 2026 katika Hifadhi ya Ngorongoro ni uthibitisho wa matukio mengi ya ukatili ya askari wa Hifadhi kwa raia bila hatua za dhati za uwajibikaji.

Kuk**atwa na kupewa mateso makali kwa vijana watatu, Ndg. Seif M***a ambae ameuawa kikatili kwa mateso ya askari wa Hifadhi ya Ngorongoro na wenzake wawili ambao bado wanapatiwa matibabu Ndg. Salimu Haji na Ndg. Abdallah Nuru, ambao walipotea njia na kwa bahati mbaya wakajikuta kwenye eneo la hifadhi, licha ya kujieleza na kutokutwa na nyara au kiashiria chochote cha uhalifu, walianza kupokea mateso makali yaliyosababisha kifo cha ndg.Seif M***a (25) na majeraha na maumivu kwa wengine.

Taarifa ya Jeshi la Polisi ya Agosti 13, 2025 inaonesha kuwa tayari wameshawak**ata askari waliokuwa zamu eneo hilo kwa uchunguzi zaidi, hatua hiyo ni muhimu lakini haitoshi katika kukomesha matukio haya ya kinyama yanayotokea kila uchao. Ni wazi kuwa askari hawa wanalindwa na viongozi wao au sheria kandamizi zinazoendelea kuumiza wananchi na hivyo ni lazima hatua zaidi za kiuwajibikaji zichukuliwe.

Matukio ya mauaji, mateso, unyanyasaji na ulipishaji fidia usio wa haki kwa wananchi yamekuWa yakiripotiwa kufanywa na askari wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Hifadhi ya Taifa ya Saadani, Hifadhi ya taifa ya ziwa Manyara, Hifadhi ya Misitu Mbarali na maeneo mengine mengi ya hifadhi. Mara zote tumesikia Jeshi la Polisi kuwa linafanya uchunguzi bila majibu ya wazi ya uwajibikaji.

Kufuatia kukithiri kwa matukio ya mauaji yanayofanywa na askari wa Hifadhi mbalimbali hapa nchini, ACT Wazalendo tunataka, Mosi, vijana waliojeruhiwa na kuteswa wapatiwe matibabu stahiki kwa gharama za serikali. Aidha Serikali ilipe fidia kwa ndugu wa kijana aliyeuliwa na kwa wote waliosababishiwa madhara, Pili askari waliohusika na ukatili huu wachukuliwe hatua za kisheria, na tatu Waziri wa Maliasili na utalii Ndg. Ashatu Kijaji (Mb), Kamishna wa Uhifadhi wa Mmalaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Ndg. Abdul Razaq Badru wajiuzulu maramoja au mamlaka za uteuzi zitengue uteuzi wao k**a sehemu ya uwajibikaji kufuatia matukio ya mauaji yanayofanywa na ofisi zao.

Vilevile tunataka utekelezaji wa mapendekezo ya Ripoti ya Tume ya haki jinai ya kufanya mageuzi ya kimfumo ya majeshi nchini na kuiondolea hadhi ya jeshi askari wa hifadhi na kurekebisha mifumo yao ya kiutendaji na uwajibikaji.

Mwisho, Tunatoa pole kwa familia za vijana waliopoteza maisha, tunamtakia kijana aliyejeruhiwa kupona haraka, na tunasimama pamoja na wananchi wote wanaodai haki, uwajibikaji na utawala wa sheria.

Imetolewa na;
Emmanuel Ntobi
Waziri Kivuli wa Maliasili, Utalii, Utamaduni na Michezo.
Agosti 14, 2026.

TAARIFA UMMA"Tunataka Waziri wa Maliasili na Utalii ajiuzulu kufuatia mauaji ya kijana Seif M***a yaliyofanywa na askari...
14/08/2026

TAARIFA UMMA

"Tunataka Waziri wa Maliasili na Utalii ajiuzulu kufuatia mauaji ya kijana Seif M***a yaliyofanywa na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro."

Waziri Kivuli wa Maliasili, Utalii, Utamaduni na Michezo wa ACT Wazalendo
Emmanuel Ntobi

04/08/2026

"Mtaani kuna wahudumu wengi wa afya hawana ajira. ACT Wazalendo tunaitaka Serikali iwaajiri ili kuziba pengo kubwa la upungufu la wahudumu wa afya nchini."

Waziri Kivuli wa Afya wa ACT Wazalendo
Elizabeth Sanga

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ACT Baraza Kivuli posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share