Tanzania Civil Aviation Authority

Tanzania Civil Aviation Authority OUR MISSION

"To ensure safety, security and regularity of civil aviation in Tanzania by providing effective oversight and efficient air navigation service

For more information contact us via [email protected]

21/08/2026



TCAA YASHIRIKI KONGAMANO LA NNE LA KIMATAIFA LA SEKTA YA UCHUKUZI NA USAFIRISHAJIMamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TC...
21/08/2026

TCAA YASHIRIKI KONGAMANO LA NNE LA KIMATAIFA LA SEKTA YA UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepongezwa kwa kuendelea kusimamia sekta ya usafiri wa anga kwa ufanisi na kuimarisha utoaji wa huduma kupitia mifumo ya kisasa ya kidijitali.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Uchukuzi Mh. Prof.Makame Mbarawa aliyekuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Nne la Kimataifa la Sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji, linalofanyika tarehe 20 na 21 Agosti 2026 katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam ambalo TCAA imeshiriki, pindi alipotembelea banda la TCAA.

Awali akiwa katika banda la TCAA, Prof. Mbarawa alipokewa na Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), Aristid Kanje, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Dkt. Jabiri Bakari, ambaye alimweleza kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mamlaka katika kusimamia na kuendeleza sekta ya usafiri wa anga nchini, ikiwemo matumizi ya teknolojia katika kuboresha utoaji wa huduma.

Kanje pia alimweleza Mh. Waziri kuhusu mfumo wa huduma za kielektroniki unaowawezesha wadau wa usafiri wa anga kupata huduma kwa haraka na kwa ufanisi zaidi, pamoja na Dawati la Huduma kwa Wateja linalowezesha kupokea na kufuatilia maoni na changamoto za wadau.

Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na limewakutanisha wadau kutoka sekta ya umma na binafsi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, maarifa na kujadili fursa na changamoto katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji nchini.

Kamati ya  Bunge ya Bajeti imekutana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)...
19/08/2026

Kamati ya Bunge ya Bajeti imekutana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi kwa lengo la Kupokea na kujadili taarifa kuhusu mwenendo wa Sekta ya Usafiri wa anga nchini, mafanikio na changamoto za kikodi.

Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mh. Mashimba Ndaki imepokea ufafanuzi na majibu kutoka kwa taasisi hizo na Pamoja na Wizara ya Uchukuzi ikiongozwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mh. David Kihenzile katika kutoa maelekezo ya kuhakikisha yote yaliyojadiliwa na kuafikiwa katika kikao hicho yanatekelezwa kwa wakati. Kikao hicho kimefanyika Agosti 18, 2026 jijini Dodoma.

TCAA YATIA  SAINI HATI YA MAKUBALIANO NA KAMANDI YA JESHI LA ANGAMamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),  imetia sai...
12/08/2026

TCAA YATIA SAINI HATI YA MAKUBALIANO NA KAMANDI YA JESHI LA ANGA

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imetia saini Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding – MoU) kati ya TCAA na Kamandi ya Anga. Utiaji saini huo umefanyika Agosti 10, 2026 jijini Dar es Salaam.

Hati hiyo ya Makubaliano inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya TCAA na Kamandi ya Anga, hususani katika utafutaji na uokoaji (Search and Rescue – SAR).

Ushirikiano huo unatarajiwa kuimarisha uratibu na uwezo wa pande zote mbili katika kutekeleza majukumu yanayohusiana na usalama wa anga.

Katika hafla hiyo Mamlaka ya Usafiri wa anga iliongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt Jabiri Bakari akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Sheria Bi. Maria Memba na upande wa Kamandi ya Anga iliongozwa na Meja Jenerali Shabani Baraghashi Mani akishuhudiwa na Meja Haika Haule.

Utiaji saini huo unaimarisha ushirikiano wa kitaasisi na ufanisi katika usalama wa anga, sambamba na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kuimarisha na kukuza sekta ya usafiri wa anga.



11/08/2026

Kwanini Ndege inaweza kuwa na viti vya abiria vilivyo wazi lakini ikaelezwa kwamba Ndege Imejaa?

Umewahi kusafiri na ndege ya abiria halafu ukakuta baadhi ya viti vipo wazi bila abiria lakini ukaambiwa ndege imejaa?

Leo Tunakuletea Ufafanuzi na elimu ya kutosha kuhusu Hali hiyo.


DKT. JABIRI KUWE BAKARI ATUNUKIWA TUZO YA MCHANGO WA MAISHA KATIKA TEHAMAMkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga T...
11/08/2026

DKT. JABIRI KUWE BAKARI ATUNUKIWA TUZO YA MCHANGO WA MAISHA KATIKA TEHAMA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dkt. Jabiri Kuwe Bakari, ametunukiwa Tuzo ya Mchango wa Maisha katika TEHAMA (TEHAMA Lifetime Achievement Award) 2026 katika hafla ya TEHAMA Awards 2026 iliyofanyika tarehe 9 Agosti 2026 jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo ni sehemu ya Tuzo za Utambuzi Maalum (Special Recognition Awards) zinazolenga kutambua watu waliotoa mchango wa kipekee na wa muda mrefu katika maendeleo ya sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) nchini Tanzania.

Dkt. Bakari ametunukiwa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake wa muda mrefu katika uongozi wa sekta ya TEHAMA, maendeleo na usimamizi wa mifumo ya kidijitali, ujenzi wa uwezo wa kitaalamu pamoja na kuendeleza matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za umma.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwake na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Kairuki.

Tuzo ya Mchango wa Maisha katika TEHAMA hutolewa kwa mtu binafsi aliyetoa mchango wa kudumu katika ukuaji wa sekta hiyo kupitia uongozi, ujenzi wa mifumo na miundombinu ya kidijitali, maendeleo ya sera, kukuza vipaji au kuanzisha na kuimarisha taasisi na huduma za TEHAMA.



09/08/2026

Je, Unaijua Tofauti Kati ya Waongozaji wa Ndege na Waegeshaji wa Ndege?

Hivi karibuni, tulijifunza kuhusu majukumu ya Waongozaji wa Ndege (Air Traffic Controllers) na jinsi jinsi walivyoanza kufuatia kuanzishwa kwa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga(ICAO), kufuatia Mkataba wa Chicago wa mwaka 1944 namna ulivyoweka misingi ya usalama katika uendeshaji wa usafiri wa anga duniani. Leo tuone tofauti yao na waegesha ndege yaani Aircraft Mashallers.

KUFAHAMU YOTE HAYA.

Ungana na Ben Mwanantala katika simulizi hii


07/08/2026

JE UNAJUA MTU ANAYEKUHUDUMIA CHAI AU KAHAWA NDANI YA NDEGE AMEPEWA MAFUNZO YA KUOKOA MAISHA YAKO?

Watu wengi hudhani kwamba kazi ya Cabin Crew ndani ya ndege ni kusambaza Chakula kwa abiria,ukweli ni kwamba hiyo ni sehemu ndogo sana ya majukumu yao.

Ungana na Ben Mwanantala katika Simulizi hii nzuri ya kuvutia.



31/07/2026



Address

Kitunda Road Junction, Banana Ukonga Area
Dar Es Salaam
255

Opening Hours

Monday 09:00 - 15:30
Tuesday 09:00 - 15:30
Wednesday 09:00 - 15:30
Thursday 09:00 - 15:30
Friday 09:00 - 15:30

Telephone

+255222198196

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Civil Aviation Authority posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tanzania Civil Aviation Authority:

Shortcuts

Share