08/08/2023
Nanenane📌
♦️DKT. SAMIA AFUNGA SHEREHE ZA MAONESHO YA WAKULIMA, WAFUGAJI NA WAVUVI (NANENANE)♦️
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 08 Agosti, 2023 amefunga rasmi maonesho ya wakulima (nanenane) yaliyofanyika Kitaifa jijini Mbeya.
Maadhimisho hayo ya siku nane yaliyofanyika katika viwanja vya
John Mwakangale, jijini Mbeya yamefikia kilele chake leo huku yakiwa na kauli mbiu isemayo "vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula".
Wakati akifunga maashimisho hayo, Mheshimiwa Dkt Samia alihitimisha kwa kutoa wito kwa wakulima wa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba ya chakula cha kutosha kwa mwaka mzima ili kuendana na hali ya hewa ya Tanzania.
Shirika la Posta Tanzania ambalo ni mdau mkubwa wa usafirishaji nchini, limepata nafasi ya kushiriki maadhimisho hayo kwa kufanya maonesho ya siku nane ya kutoa huduma na elimu ya huduma kwa wananchi namna shirika hilo linavyoenda sambamba na kusafirisha mizigo ya wakulima na wadau wengine.
Aidha Shirika la Posta Tanzania linajivunia huduma yake ya Post Cargo ambayo ni miongoni mwa huduma zinazolenga kundi la wakulima, wafugaji na wavuvi kwa namna ya kisafirisha mazao yao na kufikia Masoko mbali mbali ya ndani na nje ya nchi.
Shirika limewakilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Bw. Amos Millinga kwa niaba ya Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania aliyeambatana na Meneja wa Posta Mkoa wa Mbeya Bw. Michael Mwanachuo, pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Mkoani humo.