Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA

Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA MTENDAJI MKUU,
MAJENGO YA VETERINARI,
131 BARABARA YA NELSON MANDELA,
S.L.P 9254, DAR ES SALAAM. SIMU Na. +255 22286152
Barua: Pepe.

Mission
To enhance sustainable livestock productivity, food safety through provision of cost effective quality veterinary diagnostic and analytical services, production and marketing of veterinary products and conducting research on animal diseases. [email protected],
Tovuti: www.tvla.go.tz

Matukio mbalimbali katika picha yakimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uv...
28/07/2026

Matukio mbalimbali katika picha yakimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Prof. Mohammed Ali Sheikh, alipotembelea banda la Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kujionea namna wadau wa mifugo wanavyopatiwa elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala, Julai 12, 2026, katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere, Dar es Salaam.

28/07/2026
ENDELEZENI ELIMU YA UTAMBUZI NA MATUMIZI SAHIHI YA CHANJO ZA MIFUGO – PROF. SHEIKHNa Daudi Nyingo, Dar Es SalaamNaibu Ka...
28/07/2026

ENDELEZENI ELIMU YA UTAMBUZI NA MATUMIZI SAHIHI YA CHANJO ZA MIFUGO – PROF. SHEIKH

Na Daudi Nyingo, Dar Es Salaam

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Prof. Mohammed Ali Sheikh, ameitaka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu namna ya kutambua chanjo halisi zinazozalishwa na Wakala pamoja na matumizi yake sahihi ili kuongeza ufanisi wa kinga dhidi ya magonjwa ya mifugo.

Prof. Sheikh ametoa wito huo leo Julai 12, 2026, alipotembelea banda la TVLA katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), kwa lengo la kujionea namna wadau wa mifugo wanavyopatiwa elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala.

Ameipongeza TVLA kwa kuwa na mfumo wa alama maalumu za utambuzi wa chanjo zinazozalishwa na Wakala, akieleza kuwa hatua hiyo itaendelea kuwasaidia wafugaji kutambua chanjo halisi na kujikinga dhidi ya bidhaa bandia zinazoweza kuhatarisha afya ya mifugo na uzalishaji.

*"Ni muhimu TVLA kuendelea kutangaza alama hizi za utambuzi kupitia vyombo mbalimbali vya habari na njia nyingine za mawasiliano ili wafugaji kote nchini wazitambue na wazitumie ipasavyo,"*

*“Ni jukumu letu kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ubora wa chanjo, matumizi sahihi ya chanjo hizo na umuhimu wa kununua kutoka katika vyanzo rasmi na vilivyoidhinishwa, ili kuepusha wafugaji kudanganywa na walaghai wanaouza bidhaa zisizo halali,”* amesema Prof. Sheikh.

Akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa utambuzi wa chanjo za TVLA, Daktari Mtafiti wa Mifugo wa TVLA, Dkt. Chrisostom Kisega, amesema chanjo zote zinazozalishwa na TVLA zina alama maalumu za usalama ambazo haziwezi kughushiwa.

Amesema alama hizo ni pamoja na QR Code, Barcode, sili ya utambuzi, nembo ya TVLA, namba za bechi (Batch Numbers) pamoja na mifumo ya kidijitali ya kuhakiki ubora wa bidhaa, hatua inayowezesha wafugaji na wadau wengine kuthibitisha uhalali wa chanjo kabla ya kuzitumia.

Dkt. Kisega aliongeza kuwa wafugaji wanaotembelea katika banda la TVLA lililopo kwenye Maonesho ya Sabasaba wanapatiwa elimu kuhusu utambuzi wa chanjo za TVLA, matumizi sahihi ya chanjo, huduma za uchunguzi wa magonjwa ya mifugo pamoja na huduma nyingine zinazotolewa na Wakala kwa lengo la kuimarisha afya ya mifugo na kuongeza tija katika sekta ya mifugo nchini.

MWISHO

Matukio mbalimbali katika picha: Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Rashid Kassim Mchatta, akitembelea banda la Wakala ...
28/07/2026

Matukio mbalimbali katika picha: Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Rashid Kassim Mchatta, akitembelea banda la Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 9 Julai, 2026. Katika ziara hiyo alipokea maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na TVLA, ikiwemo uzalishaji wa chanjo za mifugo, uchunguzi wa magonjwa ya mifugo, huduma za maabara, uhakiki wa ubora na usajili wa viuatilifu vya mifugo, pamoja na tafiti zinazolenga kuboresha afya za mifugo nchini.

CHANJO ZA TVLA NI BORA NA ZINA MATOKEO CHANYA – RAS TANGAKatibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Rashid Kassim Mchatta, ames...
28/07/2026

CHANJO ZA TVLA NI BORA NA ZINA MATOKEO CHANYA – RAS TANGA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Rashid Kassim Mchatta, amesema chanjo zinazozalishwa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) zimeendelea kuthibitisha ubora wake kwa kusaidia kudhibiti magonjwa mbalimbali ya mifugo na kuongeza tija kwa wafugaji nchini.

Bw. Mchatta alitoa kauli hiyo tarehe 9 Julai 2026 alipotembelea banda la TVLA katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere, Dar es Salaam, ambapo alipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na TVLA pamoja na kuona aina za chanjo zinazozalishwa kwa ajili ya kuboresha afya ya mifugo.

*"TVLA inaendelea kufanya kazi kubwa ya kulinda afya ya mifugo. Chanjo zake ni bora na zimeonyesha matokeo mazuri kwa wafugaji wengi, hivyo ni muhimu wananchi waendelee kuzitumia ili kuongeza uzalishaji na kuchangia maendeleo ya sekta ya mifugo."*

*“Serikali itaendelea kuhamasisha wafugaji kutumia chanjo zetu za mifugo kwa kuwa zimefanyiwa tafiti za kisayansi, zina ubora unaokidhi viwango na zimekuwa na mchango mkubwa katika kupunguza milipuko ya magonjwa ya mifugo nchini”* amesema Bw. Mchatta.

Akimkaribisha Katibu Tawala katika banda la TVLA, Mtaalamu wa Maabara wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania, Bw. Henry Mlundachuma, alisema TVLA ina jukumu la kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo, kuzalisha na kusambaza chanjo, kufanya tafiti za mifugo, kusajili na kuhakiki ubora wa viuatilifu vya mifugo pamoja na kutoa huduma za ushauri na mafunzo kwa wadau wa sekta hiyo.

Alieleza kuwa katika maonesho hayo, TVLA imekuwa ikitoa elimu kwa wafugaji na wananchi kuhusu matumizi sahihi ya chanjo, umuhimu wa uchunguzi wa magonjwa kabla ya tiba, pamoja na huduma za maabara zinazosaidia kubaini magonjwa mbalimbali ya mifugo kwa wakati.

Bw. Mlundachuma aliongeza kuwa matumizi ya chanjo bora na huduma za kitaalamu za TVLA ni nguzo muhimu katika kuimarisha afya ya mifugo, kuongeza uzalishaji wa nyama, maziwa na mayai, pamoja na kuimarisha usalama wa chakula na uchumi wa wafugaji.

Banda la TVLA limeendelea kuvutia idadi kubwa ya wageni wanaotembelea Maonesho ya Sabasaba, ambapo wamekuwa wakipata elimu kuhusu huduma mbalimbali za Wakala na namna zinavyochangia maendeleo ya sekta ya mifugo nchini.

MWISHO

28/07/2026
MBUNGE, MADIWANI MBULU WAVUTIWA NA HUDUMA ZA MAABARA ZA TVLAKamati ya Fedha ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ikiongozwa...
28/07/2026

MBUNGE, MADIWANI MBULU WAVUTIWA NA HUDUMA ZA MAABARA ZA TVLA

Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ikiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Mhe. Dkt. Emanuel Qambaji Nuwas, na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Yeconia Deles, tarehe 06 Julai 2026 wametembelea banda la Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Wakiwa katika banda la TVLA lililopo ndani ya banda la pamoja la Wizara ya Mifugo na Uvuvi waliweza kupata elimu kuhusiana na huduma mbalimbali zinazotolewa na TVLA kuhusiana na jinsi ya kuimarisha afya ya mifugo, kupitia udhibiti wa magonjwa ya mifugo pamoja uhakiki wa ubora wa chakula cha mifugo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo, Mhe. Dkt. Nuwas alisema ameridhishwa na kiwango cha huduma zinazotolewa na TVLA, hususan huduma za uchunguzi wa magonjwa ya mifugo, uzalishaji wa chanjo pamoja na matumizi ya teknolojia za maabara katika kudhibiti na kuzuia magonjwa ya mifugo.

Alisema huduma zinazotolewa na TVLA zina mchango mkubwa katika kuongeza tija ya ufugaji na kuinua uchumi wa wafugaji, huku akiitaka TVLA kuendelea kuongeza juhudi za kuwafikia wafugaji wengi zaidi nchini kuwapatia elimu na mafunzo kuhusu umuhimu wa huduma za maabara.

*"TVLA inaendelea kufanya kazi kubwa ya kulinda afya ya mifugo yetu. Nawapongeza kwa huduma hizi muhimu na nitoe rai muendelee kuwafikia wafugaji wengi zaidi muwapatie elimu na huduma za kitaalamu ili sekta ya mifugo ichangie zaidi katika uchumi wa wananchi na Taifa," alisema Mhe. Dkt. Nuwas.*

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mhe. Yeconia Deless Maleyecky, aliwataka madiwani walioambatana naye kutumia elimu waliyoipata katika banda la TVLA kuwahamasisha wananchi katika kata zao kuhusu umuhimu wa kinga na udhibiti wa magonjwa ya mifugo.

Alisema viongozi wa serikali za mitaa wana nafasi kubwa ya kuwaelimisha wafugaji kuhusu matumizi ya chanjo, uchunguzi wa magonjwa na huduma nyingine zinazotolewa na TVLA, hatua itakayosaidia kuongeza uzalishaji wa mifugo na kuboresha vipato vya wananchi.

Akitoa maelezo kwa viongozi hao, Daktari Mtafiti wa Mifugo kutoka TVLA, Dkt. Julius Mwanandota, alisema TVLA ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi yenye jukumu la kulinda afya ya mifugo kupitia huduma za kisasa za maabara, utafiti na uzalishaji wa chanjo.

Dkt. Mwanandota alieleza kuwa TVLA hutoa huduma za uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya mifugo kwa kutumia teknolojia za kisasa za maabara, huzalisha na kusambaza chanjo za mifugo, pamoja na kufanya uchunguzi wa ubora na usalama wa vyakula vitokanavyo na mifugo.

Aidha, alisema Wakala hufanya usajili na uhakiki wa ubora wa viuatilifu vya mifugo kabla ya kuruhusiwa kutumika nchini, kufanya tafiti kuhusu magonjwa ya mifugo, na kutoa huduma za ushauri na mafunzo kwa wanafunzi, wafugaji na wadau wa sekta ya mifugo.

Katika Maonesho hayo, banda la TVLA limeendelea kuwa kivutio kwa wageni mbalimbali wanaotembelea Sabasaba, ambapo hupata elimu kuhusu huduma za uchunguzi wa magonjwa ya mifugo, uzalishaji wa chanjo, usalama wa bidhaa zitokanazo na mifugo na huduma nyingine za kitaalamu zinazolenga kuongeza tija ya ufugaji na kuchangia maendeleo ya sekta ya mifugo nchini.

MWISHO

Address

Nelson Mandela Road, Veterinary Complex In The Ministry Of Livestock And Fisheries Compound
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA:

Shortcuts

Share