24/03/2024
DALILI (7) ZA KUJUA MAISHA YAKO YAMEFUNGWA NA ADUI.
1. Huoni mambo mapya ya kufurahisha na kutia moyo ya kitokea kwenye maisha yako.
Huoni ukipiga hatua chanya kwenye maisha
MFANO
Huoni ukiongezeka. Kuongezeka kimaendeleo.
Kuongezeka kiuchumi, kipato ulichokuwa nacho mwaka juzi ndiyo hicho hicho mpaka leo japo matumizi yameongezeka.
Matokeo yake kuna mambo mengi ya kuondoa pesa kuliko kuingiza ukipata pesa gafla kunatokea tatizo linalodai hiyo pesa itoke,
mtu wamhim anaumwa au kunatokea msiba au tatizo lingine la lazima.
2. Mawasiliano yako yanafungwa, hakuna anae kuletea taarifa njema unaletewa tarifa mbaya tu. AYUBU 1: 16 💥
Hata ikitokea ukapigiwa simu nyingi ni zamatatizo kuliko za Habari njema
MFANO
Unaweza pigiwa cm za kuachishwa kazi.
Kuachwa na mtu umpendae,
au simu za kulaumiwa na alie takiwa kukufariji.
Kupigiwa simu na wanaokudai kuliko unaowadai.
3. Hakuna ongezeko la watu wapya wenye msaada au faida kwenye maisha yako.
Zaidi wakiongezeka niwatu ambao inabidi wewe uwasaidie.
Watu wengi wanao kutafuta ni wale wazamani ambao na wao hawajapiga hatua yoyote kimaisha,
na story mnazopiga nikukumbushana historia za nyuma za mambo dhaifu mliyo pitia ambayo hayajengi chochote kwenye maisha yako.
Marafiki walio fanikiwa hata ukiwatafuta huoni wakijali sana kuhusu wewe,
hata k**a ulikuwa wa maana sana kwao
wanakuwa k**a hawana kumbu kumbu yoyote ya maana na wewe.
4. Kila kitu chako unakipata kwa kutumia nguvu nyingi na usumbufu isivyo kawaida.
Hata ikitokea umepata mtaji unataka kufanya biashara yoyote unapata hasara,
au unaambiwa umechelewa ungeifanya mwaka jana ilikuwa inalipa sana.
5. Unakosa kibali na heshima unapingwa na mazingira yako mwenyewe,
MFANO
Waliotakiwa kukuheshim wanakudharau,
hata ukiongea wanakuonyesha mapungufu yako,
Hata mke mume au watoto uliowazaa wanakosa kukuheshim,
Hata ukitoa maagizo hakuna anae tekeleza.
6. Ahadi za mambo mazuri kwako hazitimii
MFANO
Mtu anaweza kuku ahidi pesa ikifika ile siku ukimpigia cm anakuambia nilikuwa nayo pesa lakini kunajambo nimeifanyia,
au akasema nilisahau kabisa k**a nilitakiwa kukupa nimeitumia jana subili wakati mwingine.
Unaweza ukaahidiwa kupewa kazi na CV yako ninzuri hata kuliko hiyo kazi lakini ukashangaa anachukuliwa mtu unae mzidi kwa kila kitu.
Unaweza uka ahidiwa kuolewa au kuoana na mtu, lakini ukashangaa amebadili mawazo mwishoni na kumuoa mtu mwingine ambae hakuwa amemkusudia kabisa
MWANZO 29: 25 💥
7. Hali ya kukata tamaa na kuona kila jambo haliwezekani.
Uwezo ndani yako unafunga kila kitu kwako kinakuwa ni kigumu hata mambo uliyo kuwa unayaweza kirahisi yanageuka mzigo.
Kuna kuwa na vita ya ndani inayokuwa inakuambia usijaribu utashindwa utaanguka uta aibika,
Maana wewe huwezi, k**a alishindwa yule mwenye uwezo kuliko wewe wewe huwezi.
Una kuwa na mifano mingi ya watu walio shindwa, wenye uwezo kuliko wewe,
pia inakukumbusha ulipo anguka zaidi kuliko ulipo simama.🙏
Dalili hizi nimbaya sana kuna watu zimekaa kwenye maisha yao mpaka wame amini ndiyo hali yao na maisha waliyo pangiwa na Mungu,
Mpendwa hayo siyo maisha yako bali nishetani amevamia maisha yako,
na akitoka hapo nikukuua kabisa maana hana huruma.
UKIONA UNA HIZI DALILI KWENYE MAISHA YAKO CHUKUA HATUA YA KUINGIA KWENYE MAOMBI YA TOBA NA KUITIA DAMU YA YESU YA UKOMBOZI NA UPATANISHO,
ILI UKOMBOLEWE KUTOKA KWENYE MIKONO YA ADUI NA NGUVU ZA GIZA.
✍️By Mtumishi Fahim 0716 822126 💥
Niandikie ujumbe Messenger majina yako mahali unapoishi namba yako ya cm na mahitaji yako nikuombee 👏