APRM Tanzania

APRM Tanzania African Peer Review Mechanism Tanzania is a specialized agency of the African Union.

APRM Tanzania imempongeza na kumshukuru Mhe. Badria Masoud, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, kufuatia uteuzi w...
19/07/2026

APRM Tanzania imempongeza na kumshukuru Mhe. Badria Masoud, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, kufuatia uteuzi wake kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Zanzibar.

Katika kipindi chake cha utumishi , Mhe. Badria alitoa mchango mkubwa katika kuimarisha mawasiliano ya taasisi na kusaidia utekelezaji wa majukumu yake kwa weledi.

Tunampongeza kwa kuaminiwa kulitumikia Taifa katika nafasi yake mpya na tunamtakia mafanikio, hekima na utumishi wenye tija katika majukumu yake mapya.

15/07/2026

Maridhiano ni uwekezaji katika utawala bora, amani na mshik**ano wa kimataifa. APRM Tanzania inaamini kuwa mazungumzo ya...
10/07/2026

Maridhiano ni uwekezaji katika utawala bora, amani na mshik**ano wa kimataifa. APRM Tanzania inaamini kuwa mazungumzo ya kujenga maridhiano, ushirikishwaji wa wadau na utekelezaji wa makubaliano ni miongoni mwa misingi muhimu ya utawala bora, amani na maendeleo endelevu. Maridhiano k**a haya ni msingi wa kujenga Tanzania imara, uchumi imara na mustakabali wenye matumaini zaidi kwa vizazi vijavyo.

Pichani ni matukio ya utiaji saini wa ajenda zilizokubaliwa na pande zote mbili kwa ajili ya kufanyiwa kazi kufuatia Tamko la Pamoja la Muafaka wa Kisiasa Zanzibar kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo.

Heri ya Siku ya Sabasaba
07/07/2026

Heri ya Siku ya Sabasaba

APRM Tanzania yashirikiana na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana na Wadau kufanikisha Vijana Uchumi Challenge 2026Taasi...
06/07/2026

APRM Tanzania yashirikiana na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana na Wadau kufanikisha Vijana Uchumi Challenge 2026
Taasisi ya African Peer Review Mechanism (APRM) Tanzania imeshirikiana na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, National Social Security Fund (NSSF), UTT Asset Management and Investor Services (UTT AMIS), Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), WCF, Save the Children Tanzania, African Leadership Initiatives for Impact, CRDB Bank Foundation, NMB Bank na iMbeju kufanikisha Vijana Uchumi Challenge 2026 kupitia udhamini na ushiriki katika mchakato mzima wa mashindano kuanzia hatua za awali hadi fainali. Mashindano hayo yalilenga kuibua na kukuza bunifu za vijana zenye uwezo wa kutoa suluhisho kwa changamoto za maendeleo, kuchochea ubunifu na kuimarisha ukuaji wa uchumi nchini.
Vijana Uchumi Challenge imeendelea kujidhihirisha k**a shindano linalowapa vijana nafasi ya kuwasilisha mawazo bunifu yanayoweza kutoa suluhisho kwa changamoto za maendeleo katika sekta mbalimbali za uchumi. Mashindano hayo yalivutia maelfu ya vijana kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ambapo zaidi ya waombaji 7,800 waliwasilisha bunifu zao, huku washiriki 100 bora wakichaguliwa kuendelea katika hatua za juu za mashindano. Hatimaye, katika fainali za mashindano hayo, Geofrey Samuel Sanga aliibuka mshindi wa kwanza.
Kwa kushiriki katika ufadhili wa shindano hilo, APRM Tanzania imeonesha kwa vitendo umuhimu wa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kujenga mazingira yanayowawezesha vijana kutumia maarifa, ubunifu na teknolojia k**a nyenzo za maendeleo. Ushiriki huo ulihusisha mchakato mzima wa mashindano pamoja na kutoa udhamini wa kufanikisha utekelezaji wa programu hiyo.
‘Tunaamini vijana si wanufaika wa maendeleo pekee, bali ni washiriki wakuu wa kuyabuni na kuyaendesha. Ndiyo maana APRM Tanzania inaendelea kuunga mkono majukwaa yanayowawezesha vijana kuonesha uwezo wao na kutoa suluhisho kwa changamoto za maendeleo.’ Katibu Mtendaji - APRM Tanzania
Akizungumza wakati wa kufunga rasmi Vijana Uchumi Challenge 2026, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliwataka vijana kuendelea kutumia ubunifu, maarifa na teknolojia kutatua changamoto za maendeleo na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa. Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayowasaidia vijana kuendeleza bunifu zao, kuzigeuza kuwa biashara zenye tija na kuongeza fursa za ajira nchini. Aidha, aliwataka vijana kuthubutu kutumia fursa zilizopo na kuendelea kubuni suluhisho zitakazoongeza thamani katika uchumi wa Tanzania.
Katika fainali hizo, Geofrey Samuel Sanga aliibuka mshindi wa kwanza, Jacob Fabian Lugwisha akashika nafasi ya pili, huku Robert Malonga akimaliza katika nafasi ya tatu. Mbali na kutambuliwa kwa ubunifu wao, washindi hao walitunukiwa zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuhamasisha vijana kuendelea kubuni suluhisho zenye mchango katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

Karibu kwenye Banda letu katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam. U...
02/07/2026

Karibu kwenye Banda letu katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Upate fursa ya kujifunza na kufahamu kwa kina masuala mbalimbali, hususan shughuli tunazozitekeleza katika kuhamasisha Utawala Bora.

   On  , APRM salutes the vibrancy and resilience of young Africans who are championing good governance, democracy, and ...
12/08/2024


On , APRM salutes the vibrancy and resilience of young Africans who are championing good governance, democracy, and sustainable development. We recognize the critical role youth play in shaping the continent's future and call for their active participation in decision-making processes.

Let's harness the energy and creativity of young people to drive positive change and build a more inclusive and prosperous Africa.




n









Uongozi mpya wa Taasisi ya Mpango wa hiyari wa Tathmini ya Utawala Bora Barani Afrika (APRM Tanzania) iliyochini ya Wiza...
20/06/2023

Uongozi mpya wa Taasisi ya Mpango wa hiyari wa Tathmini ya Utawala Bora Barani Afrika (APRM Tanzania) iliyochini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki umetambulishwa rasmi leo tarehe 20-06-2023 kwa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF)

Zoezi hilo limefanywa na Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo ya Mpango wa hiyari wa Tathmini ya Utawala Bora Barani Afrika (APRM Tanzania) Bw. Lamau Mpolo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) Bw. Raphael Maganga katika mkutano mfupi uliofanyika katika ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, taasisi hizo zimekubaliana mambo mbalimbali ikiwemo Kuimarisha mahusiano, kubadilishana uzoefu na kuhamasisha ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika Utawala Bora hususani katika kipindi hiki wanapoelekea kutengeneza ripoti ya pili ya tathmini ya utawala bora wa serikali hapa nchini.

16/06/2023
06/06/2023

Address

Shaaban Robert Street
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when APRM Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to APRM Tanzania:

Shortcuts

Share