06/03/2026
Mafunzo ya Mfumo wa NIIMS mkoani Morogoro
Mafunzo ya Mfumo wa Taarifa za Viwanda Tanzania (NIIMS) yanayotolewa na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO) yaliyofanyika tarehe 24 Februari 2026 kwa maafisa Biashara na TEHAMA wa mkoa wa Morogoro.
Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo maafisa Tehama na Biashara wa Halmashauri za Mkoa huo juu ya Mfumo ambao utasaidia kuhifadhi taarifa sahihi za viwanda vyote ndani ya Mkoa na hali yake.