The Fair Competition Commission - FCC

The Fair Competition Commission - FCC Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. For details visit us at www.competition.or.tz

Imepewa dhamana ya kumlinda mlaji, kukuza na kulinda ushindani (FCA No 8, 2003, as amended) na kudhibiti bidhaa bandia (MMA, 1963, as amended). Government Market Support Institution (Commission) established by the Fair Competition Act No. 8 of 2003. it is under the Ministry of Industry and Trade and is, responsible for protection and promotion of Effective Competition in Trade and Commerce and pr

otecting Consumers against unfair and misleading market conducts. According to the Merchsndise Marks Act (1963), as amended, FCC is responsible for curtailing and counteracting counterfeit products in Tanzania Mainland. As a market support institurion, FCC is particularly responsible for setting and ensuring a level playing field in the Tanzania Mainland Market, by ensuring that market participants observe competition principles and adhere to globally and legally acknowledged and accepted consumer rights and principles. These include the UN acxepted principles against restrictive trade practices (The UN Set),, and consumer rights provided under the UN Guidelines for Consumer Protection, Revised Edition of December 22, 2015 and the Consumers' International (CI) Consumer Rights. FCC has quasi-judicial powers, and exercises them inquisitorially on violations of icompetition and consumer law vide the FCA. On this front it serves as a Tribunal of first instance, with its decisions being appelable at the Fair Competition Tribunal (FCT). All matters relating to approvals of mergers and acqusitions, exemptions to mergers and agreements, registration of Business to Consumer Standard Form (Consumer) Contracts used in trade as well as protection of legitimate brands and trade marks are handled by FCC.

Wizara ya Viwanda na Biashara Yaomba Bilioni 137.8 Kuimarisha Uchumi wa Viwanda.Wizara ya Viwanda na Biashara imeliomba ...
22/05/2026

Wizara ya Viwanda na Biashara Yaomba Bilioni 137.8 Kuimarisha Uchumi wa Viwanda.

Wizara ya Viwanda na Biashara imeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla ya Sh. Bilioni 137.8 kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 kwa ajili ya kutekeleza mipango ya kuendeleza Sekta ya Viwanda na Biashara nchini ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukuza uchumi wa viwanda na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Mei 22, 2026 bungeni jijini Dodoma, Mhe. Judith Kapinga (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara amesema kati ya fedha hizo Sh. Bilioni 104.1 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Serikali.

Waziri amesema kuwa kati ya fedha hizo, za matumizi ya kawaida, Sh. Bilioni 78 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi wa Wizara, Sh. Bilioni 26 zimetengwa kwa ajili ya matumizi mengine ya uendeshaji wa shughuli za kila siku.

Aidha, Waziri amebainisha kuwa Sh. Bilioni 33.6 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo yote ikiwa ni fedha za ndani ya Serikali, hatua inayoonesha dhamira ya kuongeza Uwekezaji katika Sekta ya Viwanda na Biashara.

Waziri ameongeza kuwa Bajeti hiyo inalenga kuimarisha mazingira ya uwekezaji, kuongeza uzalishaji wa viwanda vya ndani, kukuza biashara na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na kimataifa.

"FCC Kwa utendaji wa haki katika uchumi wa soko".

22/05/2026

Viwanda vipya 25 vimetoa ajira zaidi ya 39,000.

Serikali imesema viwanda vipya, vikubwa na vya kati 25 vilivyoanzishwa nchini katika mwaka 2025/2026 vimetoa ajira zaidi ya 39,000 kwa watanzania huku vikichochea ukuaji wa uchumi na kuongeza matumizi ya malighafi za ndani.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027, Mhe. Judith Kapinga, Waziri wa Viwanda na Biashara amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali katika kujenga uchumi wa viwanda wenye ushindani na uwezo wa kuongeza thamani ya rasilimali zinazozalishwa nchini.

Aidha, Waziri amesema viwanda vimetoa jumla ya ajira 39,250 ambapo ajira za moja kwa moja ni 7,635 na zisizo za moja kwa moja ni 31,615 hali ambayo imeendelea kufungua fursa za kipato kwa wananchi.

Waziri ameeleza kuwa kupitia juhudi hizo, viwanda vipya vimejengwa huku vingine vikifanyiwa upanuzi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa bidhaa muhimu zinazotumika kwa wingi nchini na kuongeza mauzo ya bidhaa nje ya nchi.

22/05/2026

Mhe. Judith Kapinga (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara akiwa pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara hiyo na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwasili bungeni jijini Dodoma kwa ajili ya ratiba ya uwasilishaji wa bajeti ya Wizara hiyo.

"FCC Kwa utendaji wa haki katika uchumi wa soko"

Mhe. Judith Kapinga (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Ba...
22/05/2026

Mhe. Judith Kapinga (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Aristides Mbwasi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Needpeace Wambuya, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara leo asubuhi amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

"FCC Kwa utendaji wa haki katika uchumi wa soko".

Mhe. Judith Kapinga (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara alipowasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma ambapo leo Me...
22/05/2026

Mhe. Judith Kapinga (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara alipowasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma ambapo leo Mei 22, 2026 amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

"FCC Kwa utendaji wa haki katika uchumi wa soko"

"FCC Kwa utendaji wa haki katika uchumi wa soko"
22/05/2026

"FCC Kwa utendaji wa haki katika uchumi wa soko"

"FCC For fair play in the economy"
22/05/2026

"FCC For fair play in the economy"

Address

HQ PSSSF Makole Road, P. O. Box 2351, Dodoma, , , Dar Es Salaam Office, 2nd Floor, PSSSF Victoria (GEPF) House Bagamoyo Road
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Fair Competition Commission - FCC posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to The Fair Competition Commission - FCC:

Share