04/09/2026
Zaidi ya Kukimbia Pamoja!
Ushirikiano mzuri haujengwi katika kumbi za mikutano.
Unajengwa kupitia mafunzo, kazi ya pamoja na uzoefu wa pamoja.
Wataalamu wa kijeshi wa Marekani na Tanzania wameanza mafunzo ya kwanza barani Afrika yaitwayo Psychological Operations Joint Combined Exchange Training, yakileta pamoja wataalamu kutoka nchi zote mbili kujifunza kutoka kwa wenzao na kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu wa kiusalama kati ya Marekani na Tanzania.
Mazoezi hayo ya pamoja yanalenga kuwezesha kila upande kujifunza kutokana na uzoefu wa mwenzake katika kuzuia migogoro, kujenga imani na jamii za kiraia, pamoja na kutekeleza shughuli za uokoaji na kampeni za mawasiliano wakati wa majanga ya asili.
—————————————————————————
More Than Just a Run!
Good partnerships are rarely built in conference rooms.
They’re built through training, teamwork, and shared experiences.
U.S. and Tanzanian military professionals kicked off the first Psychological Operations Joint Combined Exchange Training conducted in Africa, bringing together experts from both countries to learn from one another and strengthen our long-standing U.S.-Tanzanian security partnership.
The joint exercise is aimed at each force learning from the experience of the other on conflict prevention, building trust with civilian populations, and conducting rescue operations and communication campaigns during natural disasters.