Tanzania Agricultural Development Bank

Tanzania Agricultural Development Bank TADB is established to be an apex agricultural development bank, and catalyze other banks and FIs to finance agriculture value chains.

28/08/2026
Tunawatakia Heri na Baraka za Sikukuu ya Maulid! Tudumishe upendo, amani, umoja na furaha, na tuendelee kuishi kwa wema ...
25/08/2026

Tunawatakia Heri na Baraka za Sikukuu ya Maulid! Tudumishe upendo, amani, umoja na furaha, na tuendelee kuishi kwa wema na mshikamano.

Happy Mawlid al-Nabi!

24 Agosti 2026 Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) zi...
24/08/2026

24 Agosti 2026 Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) zimesaini Hati ya Makubaliano yenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa fedha katika sekta ya kilimo, kuongeza uzalishaji na usalama wa chakula, kuimarisha minyororo ya thamani na kufungua fursa zaidi za kiuchumi kwa wananchi wa Zanzibar.

Makubaliano hayo yanalenga kuunganisha upatikanaji wa fedha na mahitaji halisi ya mnyororo wa thamani wa kilimo, kuanzia uzalishaji, ukusanyaji na uchakataji hadi usafirishaji na masoko, ili kuongeza tija, thamani ya mazao na kujenga masoko ya uhakika kwa wazalishaji wa ndani.

Hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo imefanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, Mbweni Zanzibar, na kuhudhuriwa na Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Shaaban Ali Othman, Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na viongozi na watendaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, TADB, ZEEA, BPRA washirika wa maendeleo, sekta binafsi, wakulima na wajasiriamali.


17/08/2026



 Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Mhe. Suleiman Masoud Makame, ameipongeza Benki ya Maendele...
16/08/2026



Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Mhe. Suleiman Masoud Makame, ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa mchango wake katika kuchochea mageuzi ya sekta ya kilimo Zanzibar.

Mhe. Makame alitoa pongezi hizo wakati akifunga Maonesho ya Nanenane Zanzibar yaliyofanyika Agosti 1 hadi 16 katika Viwanja vya Dole Kizimbani, ambapo TADB ilikuwa miongoni mwa wadhamini.

Amesema ushiriki wa TADB unaonesha umuhimu wa taasisi za fedha katika kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kupata mitaji na huduma za kifedha.

Waziri Makame pia ametoa wito kwa taasisi nyingine za fedha kuongeza ushirikiano na Serikali katika kuwekeza kwenye kilimo, ili kuongeza uzalishaji, tija na kipato cha wananchi.

Amesisitiza kuwa maendeleo ya kilimo yanahitaji ushirikiano wa Serikali, taasisi za fedha, sekta binafsi na wadau wengine.



  Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amewataka wananchi, hususan wakulima, wafuga...
16/08/2026

Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amewataka wananchi, hususan wakulima, wafugaji, wavuvi, vijana na wanawake, kuchangamkia fursa za kifedha zinazotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuongeza mitaji, uzalishaji na kipato.

Mhe. Hemed ametoa wito huo baada ya kutembelea banda la TADB katika Maonesho ya Nanenane Viwanja vya Dole Kizimbani, na baadaye kuwaalika viongozi wa benki ya TADB - Zanzibar ofisini kwake Vuga kwa mazungumzo.

Katika mazungumzo hayo, walijadili namna TADB inavyowawezesha wananchi kupitia mikopo na fursa mbalimbali katika sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Mhe. Hemed ameitaka TADB kuongeza elimu kwa wananchi ili waweze kuzifahamu na kuzitumia fursa hizo, akisisitiza kuwa Zanzibar ina fursa kubwa ya kuendeleza kilimo na kuongeza uzalishaji.

Kwa upande wake, Meneja wa TADB Kanda ya Zanzibar, Ally Jamal, ameshukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano na mazingira wezeshi inayoiwekea TADB katika kutekeleza majukumu yake na kuwafikia wananchi.

Jamal amesema TADB itaendelea kutumia mazingira hayo kushirikiana na Serikali katika kuwawezesha wananchi, huku akieleza kuwa tayari benki hiyo imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 15 kwa wananchi wa Zanzibar.



16/08/2026




14/08/2026


Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeshiriki Kongamano la Uchumi wa Buluu lililofanyika Kizimkazi, Zanzibar, ...
13/08/2026

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeshiriki Kongamano la Uchumi wa Buluu lililofanyika Kizimkazi, Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya Tamasha la Kizimkazi la Biashara na Utamaduni.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, likiwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya uvuvi kutoka katika mnyororo mzima wa thamani, kujadili fursa, changamoto na namna ya kuendeleza sekta hiyo.

TADB iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Mipango na Ushauri wa Kitaasisi, Bw. Mkani Waziri, akiambatana na Meneja wa Kanda ya Zanzibar, Bw. Ally Jamal. Bw. Waziri alikuwa miongoni mwa wazungumzaji, akieleza namna TADB inavyochagiza maendeleo ya Uchumi wa Buluu kupitia uwezeshaji wa sekta ndogo ya uvuvi na shughuli zinazohusiana na mnyororo wa thamani.

Alisisitiza utayari wa TADB kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kuwezesha upatikanaji wa fedha na uwekezaji kwa ajili ya kuongeza tija, thamani na ushindani wa sekta ya uvuvi.

Kongamano hilo lilikuwa na kaulimbiu isemayo “Hifadhi Bahari, Changamkia Fursa za Uchumi wa Buluu.”




13/08/2026

Ahsante mama



Address

Kinondoni Road
Dar Es Salaam
255

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Telephone

+255222923500

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Agricultural Development Bank posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tanzania Agricultural Development Bank:

Shortcuts

Share