16/10/2025
MIAKA 10 YA TBPL 🔥🔥🔥🔥.
Katika kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Tanzania Biotech Products Limited (TBPL), hafla maalum imefanyika ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, kwa pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Dkt. Nicolas Shombe, wameongoza zoezi la kukata keki ya kumbukizi k**a ishara ya furaha, mafanikio, na ukuaji endelevu wa kiwanda hicho.
Tukio hilo limeudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa sekta ya viwanda, watafiti, na wafanyakazi wa TBPL na NDC.Limeakisi safari ya mafanikio ya kiwanda hicho katika kipindi cha miaka kumi, safari iliyojengwa juu ya misingi ya ubunifu wa teknolojia za kibaiolojia, uzalishaji wa bidhaa bora, na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa viwanda nchini.