Embassy of Denmark in Tanzania

Embassy of Denmark in Tanzania Welcome to the page of the Embassy of Denmark in Tanzania.

Our mission:
Development cooperation is a cornerstone in the relationship between Denmark and Tanzania, along with multifaceted relations involving trade and investments, culture and political cooperation . A main task for the Embassy is responsibility for development cooperation with Tanzania but we also provide various other services to Danish and Tanzanian citizens. Link to the MFA code of con

duct for social media: https://um.dk/en/about-us/organisation/mfa-on-social-media/social-media-guide

Kiswahili:

Katika ukurasa huu utapata

- Taarifa kuhusu Tanzania k**a kivutio cha utalii

- Habari za kabiashara kuhusu Afrika Mashariki.

- Ushirikiano wa kitamaduni kati ya Denmark na Tanzania

- Habari kutoka Ubalozi wa Denmark

-Mengine yo! Ushirika wa kimaendelio ni msingi katika uhusiano kati ya Denmark na Tanzania, pamoja na mahusiano ya kushirikisha biashara na vitega uchumi, utamaduni na ushirikiano wa kisiasa. Kazi kuu Ubalozi ni kusimania ushirikiano wa kimaendelio na Tanzania lakini pia kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wa Denmark na Tanzania.

Wanawake katika vyuo na taasisi za utafiti bado wanakabiliwa na changamoto zinazowazuia kupiga hatua katika utafiti na n...
24/08/2026

Wanawake katika vyuo na taasisi za utafiti bado wanakabiliwa na changamoto zinazowazuia kupiga hatua katika utafiti na nafasi za uongozi.

Hivi karibuni, Chuo Kikuu cha Mzumbe kiliwakutanisha watafiti wanawake, wahadhiri, Wanachama wa Danida Fellows na wanafunzi wa uzamili mjini Morogoro kujadili changamoto hizi na namna ya kuzitatua.

Ubalozi wa Denmark ulishiriki katika warsha hiyo, iliyofadhiliwa kupitia mpango wa Danida Fellowship Centre wa mwaka 2026.

Majadiliano yalijikita katika ushauri, kujenga mitandao, ushirikiano katika utafiti na uongozi.

_______________

Women in academia continue to face barriers to advancing in research and leadership.

Recently, Mzumbe University brought together women researchers, academics, Danida Fellows and postgraduate students in Morogoro to discuss how to break these barriers.

The Embassy of Denmark attended the workshop, supported through the Danida Fellowship Centre’s 2026 grant.

The discussions focused on mentorship, networking, research collaboration and leadership.

21/08/2026

Just two coworkers with the exact same fashion sense. 😂

Happy Weekend 🎉

Tunamkaribisha Kamilla Borre Jørgensen, Mshauri wetu mpya wa Sekta Ubalozini.Kamilla atashughulikia ushirikiano wa kodi ...
20/08/2026

Tunamkaribisha Kamilla Borre Jørgensen, Mshauri wetu mpya wa Sekta Ubalozini.

Kamilla atashughulikia ushirikiano wa kodi kati ya Denmark na Tanzania.

Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mamlaka ya Kodi ya Denmark, atasaidia kuendeleza ushirikiano huu mpya wa kodi kati ya nchi hizi mbili.

Kabla ya kujiunga na Ubalozi, Kamilla alifanya kazi katika Mamlaka ya Kodi ya Denmark, ambako alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Kampeni na Chapa.

Nje ya kazi, anafurahia muda na familia yake, shughuli mbalimbali za sanaa na utamaduni na kusafiri.

_____________

Meet Kamilla Borre Jørgensen, our new Sector Advisor at the Embassy of Denmark in Tanzania.

Kamilla will support our work on tax cooperation between Denmark and Tanzania.

Together with the Tanzania Revenue Authority and the Danish Tax Agency, she will help drive the new bilateral tax cooperation.

Before joining us, Kamilla worked at the Danish Tax Agency as Head of Division for Campaigns and Branding.

Outside work, she enjoys family time, cultural events and, of course, travelling.

19/08/2026

Hongera kwa John Petro Maganga kwa kupata ufadhili wa masomo kupitia Erasmus Mundus.

Atasomea Shahada ya Uzamili katika Uandishi wa Habari na Utandawazi katika Chuo Kikuu cha Aarhus nchini 🇩🇰Denmark.

Erasmus Mundus ni programu za kimataifa zinazoendeshwa kwa pamoja na vyuo vikuu mbalimbali barani Ulaya, huku ufadhili kamili wa masomo ukitolewa kwa wanafunzi waliochaguliwa kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Ikiwa unafikiria kusoma 🇪🇺Ulaya, tembelea tovuti ya Erasmus Mundus kuona fursa zilizopo na kutuma maombi.
___________

Congratulations to John Petro Maganga on being awarded an Erasmus Mundus scholarship.

He will pursue a Master’s in Journalism and Globalisation at Aarhus University in 🇩🇰Denmark.

Erasmus Mundus Joint Masters are international programmes jointly delivered by universities across Europe, with full scholarships available to selected students from around the world.

If you’re thinking about studying in 🇪🇺Europe, explore the Erasmus Mundus opportunities and apply through the Erasmus website.

Mchezaji wa soka kutoka Denmark, Elliot Bachelor, alitumia muda akiwa Tanzania akiwafundisha vijana katika Young Boys Ac...
18/08/2026

Mchezaji wa soka kutoka Denmark, Elliot Bachelor, alitumia muda akiwa Tanzania akiwafundisha vijana katika Young Boys Academy, TZ.

Kipa wa timu ya U19 ya alifanya kazi na timu za U11 na U13, akiwafundisha vijana na kushirikiana nao ndani na nje ya uwanja.

Hii inaonyesha jinsi Denmark na Tanzania zinavyoweza kujenga uhusiano imara zaidi kupitia michezo. 🇩🇰🇹🇿⚽

_____________

Danish footballer Elliot Bachelor spent his summer in Tanzania coaching young players at Young Boys Academy, TZ

The U19 goalkeeper worked with the U11 and U13 teams, sharing his skills and experience both on and off the pitch.

It’s a great example of how people-to-people connections between Denmark and Tanzania can grow through sport. 🇩🇰🇹🇿⚽

📸: Young Boys Academy, TZ | Elliot Bachelor |

Hongera kwa Watanzania watatu waliochaguliwa kupata ufadhili wa masomo ya Shahada ya Uzamili katika Immunolojia na Infla...
17/08/2026

Hongera kwa Watanzania watatu waliochaguliwa kupata ufadhili wa masomo ya Shahada ya Uzamili katika Immunolojia na Inflamesheni katika Chuo Kikuu cha Copenhagen! 🇹🇿🇩🇰

Walichaguliwa kati ya waombaji 120 na watakwenda Denmark mwezi huu kusoma kwa muda wa miaka miwili.

Ufadhili huu ni sehemu ya ushirikiano wa utafiti kati ya KCMC, Chuo Kikuu cha Ghana na Chuo Kikuu cha Copenhagen, unaofadhiliwa na Denmark kupitia Danida Fellowship Centre.

Leo, tumekutana nao na kusikia kuhusu matarajio yao wanapojiandaa kuanza masomo yao nchini Denmark.

______________

Congratulations to three Tanzanians selected for a Master’s scholarship in Immunology and Inflammation at the University of Copenhagen! 🇹🇿🇩🇰
 
Selected from 120 applicants, they will travel to Denmark this month for two-year Master’s degrees.

The scholarship is part of a research partnership between KCMC University, the University of Copenhagen and the University of Ghana, funded by Denmark through the Danida Fellowship Centre.

Today, we heard about their expectations and hopes for bringing their experience back home.

14/08/2026

We are just here for the teamwork... and aparently the fun too 😉

Happy Weekend 🎉

Wiki hii mjini Moshi, watafiti, wasomi, wanafunzi na wataalamu kutoka Tanzania, Ghana na Denmark wanashiriki katika Kozi...
13/08/2026

Wiki hii mjini Moshi, watafiti, wasomi, wanafunzi na wataalamu kutoka Tanzania, Ghana na Denmark wanashiriki katika Kozi ya Ubunifu ya UPIVAC Africa.

Kozi hii ni sehemu ya ushirikiano kati ya Vyuo Vikuu vya KCMC, Copenhagen na Ghana, unaofadhiliwa na serikali ya Denmark.

Lengo ni kuimarisha maarifa na ushirikiano katika tafiti za kinga ya mwili na chanjo.

Wanafunzi watatu Watanzania waliopata ufadhili kupitia mpango huu hivi karibuni watakwenda Denmark kuendelea na masomo yao katika Chuo Kikuu cha Copenhagen. 🇹🇿🇩🇰
__________

This week in Moshi, researchers, academics, students and experts from Tanzania, Ghana and Denmark are taking part in the UPIVAC Africa Innovation Course.

The course is part of a partnership between KCMC University, the University of Copenhagen and the University of Ghana, supported by Denmark.

It strengthens knowledge and collaboration in immunology and vaccinology.

Three Tanzanian scholarship recipients taking part in the programme will soon travel to Denmark to continue their studies at the University of Copenhagen. 🇹🇿🇩🇰

12/08/2026

Happy International Youth Day

 ilishiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vijana 2026 jijini Dodoma! Wawakilishi wa DFC Fellows na European...
11/08/2026

ilishiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vijana 2026 jijini Dodoma!

Wawakilishi wa DFC Fellows na European Union Youth Sounding Board in Tanzania walishiriki katika mjadala kuhusu nafasi ya vijana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, pamoja na fursa zilizopo katika Uchumi wa Kijani na Uchumi wa Buluu.

Mjadala ulionyesha kuwa vijana:

✅ Wana mawazo mapya na wanaweza kuleta mabadiliko
✅ Wana nafasi muhimu katika mijadala ya sera na maamuzi
✅ Wana mchango mkubwa katika kutafuta na kutekeleza suluhisho za changamoto za tabianchi

Denmark inaendelea kuunga mkono vijana wa Tanzania kwa kuwapatia fursa ya kupata taarifa, kutoa mawazo yao, kushirikiana na wadau mbalimbali na kuchukua hatua katika masuala yanayowahusu. 🇩🇰🇹🇿

__________

KEYJana Impact took the stage at International Youth Day 2026 in Dodoma! 🎉

DFC Fellows and members of the EU Youth Sounding Board for Tanzania joined a panel on youth participation in climate action and opportunities in the Green and Blue Economy, showing that young people are:

✅Innovators and problem-solvers
✅Policy actors and decision-makers
✅Contributors to real climate solutions

Denmark is proud to support young Tanzanians turning policy information into understanding, participation, innovation and action. 🇩🇰🇹🇿

Address

Ghana Avenue 1
Dar Es Salaam
P.O.BOX9171

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 13:00

Telephone

+255222165200

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Embassy of Denmark in Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Embassy of Denmark in Tanzania:

Shortcuts

Share