21/08/2026
UNAPOPATA NAFASI YA KUKUTANA NA MTU ANAYEFANYA JAMBO K**A LAKO NA ANAKUZIDI UZOEFU AU MATOKEO
1. Usiende kumuona bila sehemu ya kuandika hekima kadhaa utakazopata kwake za kukupa hatua kwenye unachofanya au unachotaka kuwa
2. Ukifika muoneshe adabu, shuka, hata k**a atakusifia au kueleza unavyofanya vizuri, ili kuepuka kujiweka daraja moja na kumfanya asiseme mengi k**a mkubwa kwa mdogo
3. Sikiliza zaidi na ikiwezekana ongea tu mahali pa kushukuru, au kuuliza au kutaka ufafanuzi tu, Wewe sio mshirika mwenza wa hilo daraja, wewe ni mpokeaji wa hekima
4. Hakikisha umeandaa orodha ya maswali unayotaka kuuliza kabisa, na usiulize maswali ili uchangie unachojua, uliza ili yeye akupe siri na hekima
5. Uliza maswali yale tu ambayo akiyajibu kwa ufasaha ukapata nuru yatakupa hatua zaidi kwenye unachofanya
6. Usiongelee kabisa habari zako au mambo yako labda endapo amekuuliza, umekwenda kujifunza na si kuonesha mafanikio yako
7. Hata k**a huyu mtu ni mnyenyekevu, yuko simple mno, usilete mazoea k**a vile ni mtu wa daraja lako, mazoea yanakata flow ya moyo wa mtu mkuu kusema na kufunua mengi bali heshima na adabu ya waziwazi itakufungulia milango mikubwa kwa mhusika
8. Unapokwenda kwa mtu mkuu, usiende mikono mitupu, beba sadaka au zawadi iliyo kwenye ngazi au daraja lake, inaweza kuwa fedha ambayo hujawahi kuitoa kokote, kinaweza kuwa kitu ambacho kwako ni ghali (expensive, valuable)
Mioyo ya wakuu hufunguliwa na zawadi ya mtu!
9. Mruhusu akuambie mambo yapi kwako uyaondoe au uyaache ili uwe mtu bora
Usijitetee au kujieleza sana anapokuambia kuhusu makosa, madhaifu na yale ambayo hufanyi vizuri, maana kila mtu anapenda zaidi kuambiwa upande wake wa nguvu na hataki kuguswa upande wa marekebisho!
10. Uyazingatie hayo mambo tisa juu na yatakufanya uwe bora katika uyatendayo
Askofu Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI