19/08/2026
DKT. BATILDA : WIKI YA ELIMU YAING'ARISHA TANGA, LANGO LA UCHUMI AFRIKA MASHARIKI
Tanga.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Dkt. Batilda Buriani wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, iliyobeba Kauli mbiu " Elimu , Ujuzi na Ubunifu, njia ya kufikia Dira 2050" , Tarehe 18 Agosti 2026 - Uwanja wa Usagara - Jijini Tanga.
Amesema kuwa Uwekezaji unaofanywa na Serikali kwa Sekta ya Elimu - Tanga ni utekelezaji wa maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresho mitaala, Ujenzi wa miundombinu ya elimu na utekelezaji wavsera ya elimu ni nyenzo ya kuimarisha ujuzi, sayansi, teknolojia na bunifu kutumia rasilimali adhimu za Mkoa huo ili kutumia uchumi-maarifa kwa lengo la kuongeza tija ya uzalishaji wa viwanda vya ndani, biashara, kilimo, utalii na uwekezaji mkao wa Tanga.
" Tunajenga refinery na viwanda, hivyo tunahitaji kuwaandaa zaidi vijana wetu ili wawe tayari kutumia fursa hizi, Tanga imekuwa Kitovu cha viwanda, madini na uwekezaji wa kiuchumi hivyo kuimarisha utaoji huduma kwa sekta za viwanda, ujenzi, madini, nishati, biashara na gesi miongoni mwa maeneo yenye fursa kubwa " alisisitiza
Dkt. Batilda amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa uwekezaji huo mkubwa na kuendelea kuchagua kuadhimisha Wiki hiyo mkoani humo kwa mara ya tatu mfululizo, na kutambua mchango wa viongozi wa dini kudumisha amani, mshik**ano na utulivu nchini Tanzania.
Aidha, Uwekezaji wa Elimu umeanza kuonekana kupitia ujenzi wa shule, madarasa, mabweni kutoka shule 46 mpaka shule 94 na ongezeko la ufaulu kutoka Asilimia 84% mpaka kufikia Asilimia 90% vikienda sambamba na ongezeko la ajira za walimu na upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya elimu ya amali na ufundi Jijini Tanga. Ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo, Elimu bila ada, kuimarika kwa ongezeko la fedha hivyo kusaidia Serikali kukabiliana na changamoto za miundombinu na mazingira ya kujifunzia.
" Kwa Mwaka wa Fedha wa 2026/27, Mkoa wa Tanga imekuwa mwenyeji wa Ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe ikiwa ni fursa ya uwekezaji wa elimu ya juu, tafiti, ubunifu na uzalishaji wa wataalamu ili kuongeza mwingiliano kati ya vyuo, viwanda, sekta binafsi na jamii, na kutumika kwa uchumi maarifa kutatua changamoto za jamii na kuzalisha ajira." Amelisema.
Aidha, amebainisha kuwa Mkoa huo umekuwa kitovu cha uzalishaji wa bidhaa kwa kutumia rasilimali za ndani k**a vile madini ya graphite, saruji (cement), vifaa vya ujenzi na gesi zinazoongeza thamani ya mkoa, mazingira ya vijana kujifunza elimu ya vitendo, badala ya kubaki watazamaji wa maendeleo pekee bali kuchangia matumzi ya uchumi maarifa.
Dkt. Burian alisema kufanyika kwa Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu mkoani Tanga kumetoa faraja na umuhimu wa kipekee kuonesha mafanikio, kubaini changamoto na kujadili namna bora amali inavyoweza kutatua changamoto za jamii na kuchochea ujenzi wa uchumi maarifa sayansi, teknolojia na ubunifu. Pia, Utalii na uchumi wa buluu nao wachangia fursa za ukuzaji na mazingira ya ujifunzi wa vitendo kupitia viwanda vya Tanga vilivyo na utajiri mkubwa wa vivutio vya utalii k**a Mapango ya Amboni na Magoroto vinavyochangia uchumi wa mkoa na Taifa.