06/09/2026
๐ต๐ธ GAZA 1989: Historia ya Ukandamizaji na Kizazi Kisichotaka Tena Kusubiri ๐ฅ๐๏ธ
โHuu ni ukweli wa kihistoria unaoonyesha wazi kuwa mateso, dhuluma, na kupokwa kwa haki za Wapalestina si mambo ya leo wala ya jana, ni mfumo uliopandwa miongo mingi iliyopita.
โKwenye video hii ya mwaka 1989, inaelezwa wazi jinsi Ukanda wa Gaza ulivyogeuzwa kuwa mojawazi ya maeneo yenye msongamano mkubwa zaidi duniani kutokana na kuwepo kwa kambi 26 za wakimbizi ndani ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu. Watu zaidi ya 650,000 walilundikwa kwenye eneo dogo sana la maili 5 upana na maili 28 urefu, huku wakizungukwa na makazi mapya ya Waisraeli na jeshi kubwa la ukandamizaji ambalo idadi yake ilikuwa mara tatu zaidi ya wanajeshi waliotumwa kuliteka eneo hilo mwaka 1967.
โNdani ya kambi hizi kuna simulizi za kusikitisha za tabaka tatu za watu:
1๏ธโฃ Wale waliokimbia mwaka 1948 wakidhani wangerudi nyumbani baada ya miezi michache.
2๏ธโฃ Wale waliokuja mwaka 1967 wakiamini huo ungekuwa ukimbizi wa muda mfupi.
3๏ธโฃ Kizazi kipya kilichozaliwa kambini, kilichotazama wazazi na babu zao wakiishi na kufia kwenye ukimbizi huo, na sasa hakiko tayari tena kusubiri!
โVita hii si ya kidini; ni vita dhidi ya dhuluma, ukoloni wa kibaguzi (Apartheid), na unyang'anyi wa ardhi. Utu wa binadamu unavunjwa mchana kweupe, na sauti za wanyonge haziwezi kunyamamazishwa milele.
โFREE PALESTINA ๐ต๐ธ๐ต๐ธ๐ต๐ธ
โTafadhali fuatilia (Follow), shiriki (Share) na Like kurasa zetu ili kusaidia kuongeza uelewa na kusimama pamoja katika kudai haki dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi (Apartheid). ๐ข๐
โKila mmoja wetu ana nafasi ya kuwa sauti ya wasio na sauti. ๐โจ
โ