25/01/2019
Tanzia: Nguli wa Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini Bi. Salome Nonge maarufu kwa jina la Mama Abduli amefariki dunia leo Tarehe 25 Januari, 2019 akiwa nyumbani kwake Mburahati jijini Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa ini.