Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania

Ofisi  ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini husimamia utekelezaji wa Sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka1992 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010

01/07/2026
UMOJA WA KITAIFA NI MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050 - WAZIRI DEUS SANGUSerikali imeviasa vyama vya siasa kuendela...
17/06/2026

UMOJA WA KITAIFA NI MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050 - WAZIRI DEUS SANGU

Serikali imeviasa vyama vya siasa kuendela kuimarisha mazungumzo, ushirikiano na umoja wa kitaifa wakati Tanzania ikijiandaa kuanza kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 mwezi Julai mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, wakati akifungua warsha ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa mjini Morogoro tarehe 17 Juni 2026. Warsha hiyo yenye lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu jukumu jipya la Mahusiano ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa siasa.

Kwenye hotuba yake Waziri Sangu amesema vyama vya siasa ni wadau muhimu katika kukuza amani, umoja na ustawi wa jamii. Ameongeza kuwa, utayari wao wa kushirikiana na Serikali ni muhimu katika kuimarisha mahusiano kati ya Serikali na makundi mbalimbali ya kijamii, ikiwemo vyama vya siasa vyenyewe.

Amewapongeza na kuwaasa viongozi wa kisiasa kuendelea kuwa mabalozi wa amani na kutokubali kutumiwa na watu wachache wenye maslahi binafsi wanaoweza kuligawa taifa au kuhatarisha utulivu na amani ya nchi.

“Leo tunapozungumzia mahusiano kati ya Serikali na vyama vya siasa, niwahakikishie kuwa dhana hii inaendelea kutekelezwa kupitia falsafa maarufu ya 4R iliyoasisiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kujenga taifa lenye amani na umoja,” alisisitiza Waziri Sangu.

Amesema falsafa hiyo ya Rais Samia ya 4R, ambayo ni Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko na Ujenzi Upya, inaendelea kuongoza jitihada za Serikali katika kukuza mazungumzo, kuimarisha kuaminiana na kujenga taifa lenye umoja kupitia ushirikishwaji mpana.

Waziri Sangu amelipongeza Baraza la Vyama vya Siasa kwa kuendelea kushirikiana na Serikali, ikiwemo kutoa ushauri katika masuala mbalimbali ya kitaifa. Amesema ushirikiano huo ni muhimu wakati nchi ikielekea katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ambayo inahitaji mshik**ano na malengo ya pamoja bila kujali tofauti za kisiasa.

Akiunga mkono ujumbe huo, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Mhe. Juma Ali Khatibu, amesema vyama vya siasa vina nafasi kubwa katika jamii ya Watanzania na vinaweza kusaidia kuimarisha mahusiano, amani na maelewano ndani ya jamii.

Khatibu ameongeza kuwa Baraza hilo linatambua dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza siasa za ushirikishwaji. Ametolea mfano uteuzi wa mmoja wa wajumbe wa Baraza hilo, Dkt. Eveline Wilbard Munisi kutoka NCCR-Mageuzi, kuwa Mbunge na Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano. Amesema uteuzi huo unaonesha kuaminiana, ushirikishwaji na ushirikiano katika siasa za ushindani nchini.

Akieleza zaidi kuhusu lengo la kikao hicho, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mstaafu Francis Mutungi, amesema warsha hiyo ni matokeo ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya Baraza la Vyama vya Siasa kilichofanyika tarehe 21 Mei mwaka huu. Amesema katika kikao hicho ilikubalika kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu itoe mada ya kujenga uelewa kuhusu jukumu jipya la Mahusiano kwa ustawi wa Tanzania.

Warsha hiyo imehudhuriwa na viongozi wa kitaifa kutoka vyama vya siasa 18 kati ya 19 vyenye usajili kamili. Kikao hicho kinaonesha dhamira ya Serikali ya kuviona vyama vya siasa si tu k**a washindani wa uchaguzi, bali pia k**a washirika muhimu katika ujenzi wa amani, mshik**ano wa jamii na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

01/06/2026

CCM imetekeleza maelekezo ya Msajili. Habari za mitandaoni ni upotoshaji.

29/05/2026

Madai ya kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inadharau Mahak**a ni upotoshaji wa dhahiri. Msajili Msaidizi Sisty Nyahoza, anaeleza ukweli kuhusu zuio hilo la Mahak**a.

Viongozi wa Siasa Tayari Kuwa Vinara wa MajadilianoViongozi wa vyama vya siasa wameeleza utayari wao wa kuunga mkono maj...
21/05/2026

Viongozi wa Siasa Tayari Kuwa Vinara wa Majadiliano

Viongozi wa vyama vya siasa wameeleza utayari wao wa kuunga mkono majadiliano ya pamoja kati ya Serikali na makundi mbalimbali ya kijamii, ikiwa ni hatua inayotarajiwa kuimarisha amani, ushirikiano, utulivu wa kijamii na mshik**ano wa kitaifa.

Utayari huo umebainishwa mjini Morogoro wakati wa kikao kilichowakutanisha Ofisi ya Waziri Mkuu inayosimamia Kazi, Ajira na Mahusiano na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa.

Kikao hicho kilitoa fursa kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kutambulisha majukumu ya Idara ya Mahusiano na kueleza nafasi yake katika kuimarisha mahusiano kati ya Serikali na wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, makundi ya kijamii na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Mauhusiano, Bi. Zuhura Yunus, amesema kikao hicho ni sehemu ya jitihada zinazoendelea za kuimarisha mahusiano kati ya Serikali na wadau wake kupitia majadiliano, ushirikiano na uelewa wa pamoja.

Amesema vyama vya siasa ni wadau muhimu katika kujenga uaminifu, kuimarisha mawasiliano na kuendeleza umoja wa kitaifa, hasa kutokana na ukaribu wao na wananchi katika ngazi mbalimbali za jamii.

Akiendeleza ujumbe huo, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mstaafu Francis Mutungi, amesisitiza kuwa vyama vya siasa ni washirika muhimu katika kulinda amani na utulivu nchini. Amesema mahusiano mazuri kati ya Serikali na wadau wa siasa hujenga ushirikiano, na ushirikiano huo hufungua nafasi ya majadiliano na upatikanaji wa suluhu za changamoto mbalimbali za kijamii na kitaifa.

Jaji Mutungi ameongeza kuwa viongozi wa siasa wana nafasi kubwa ya kulinda tunu ya amani ya Tanzania kwa kuhamasisha umoja, uvumilivu na ushiriki wa wananchi kwa njia ya staha na uwajibikaji.

Kauli ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na vyama vya siasa
pia imeungwa mkono na Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma, CHAUMMA, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Baraza la Vyama vya Siasa, Bw. Salum Mwalimu. Amepongeza kikao hicho akisema ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano, huku akisisitiza kuwa mahusiano mazuri kati ya Serikali na wadau wa siasa ni muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa vipaumbele vya kitaifa, ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.

Zaidi ya kubadilishana mawazo, kikao hicho kinatarajiwa kuboresha mawasiliano kati ya Serikali na wadau, kuimarisha imani kati ya taasisi za umma na viongozi wa siasa, pamoja na kujenga mazingira mazuri ya ushirikiano katika kushughulikia masuala ya maendeleo ya taifa. Kikao hicho cha siku moja kiliandaliwa kufuatia ombi la Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kukutana na wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa ikiwa na lengo kutoa elimu kuhusu majukumu ya Idara hiyo mpya ya Mahusiano.

Bofya link kupata orodha na mawasiliano rasmi ya vyama vyenye usajili kamili 👇https://www.orpp.go.tz/uploads/documents/s...
15/04/2026

Bofya link kupata orodha na mawasiliano rasmi ya vyama vyenye usajili kamili �https://www.orpp.go.tz/uploads/documents/sw-1776159118-ORODHA%20YA%20VYAMA%20VYA%20SIASA%20CURRENT%20AS%20AT%20JANUARI%2020_260414_121940.pdf

Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. Jaji Mstaafu Francis Mutungi amekutana na  kufanya mazungumzo na Mhe. Lazarus Chakwera,...
10/04/2026

Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. Jaji Mstaafu Francis Mutungi amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Lazarus Chakwera, Rais wa Zamani wa Malawi na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola. Kikao hicho ni sehemu ya ziara ya Mhe. Chakwera nchini ambapo anakutana na makundi mbalimbali ya wanasiasa, taasisi na viongozi wa Serikali. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 10 Aprili 2026 katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa zilizopo Mtaa wa Shaban Robert Jijini Dar es Salaam.

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania:

Shortcuts

Share