28/05/2026
Issue siyo urembo, pesa, shepu, elimu au umaarufu, kinachotazamwa ni maadili ya mwanamke sawasawa na maandiko na pia asili ya mwanamke katika kuuk**ata moyo wa mumewe. Biblia inaagiza wanawake wawe watii (Efeso 5:22), na pia kichwani waonyeshe dalili ya kumilikiwa (1 Wakorintho 11:10). Ambapo zamani dalili hiyo ilikuwa ni kilemba, baadaye ikaja kuwa pete ya ndoa, ila kwa sasa inapaswa kuwa akili pevu (A mature mind) ya kumstahi mume k**a mamlaka inayokumiliki. Zile mambo za haki sawa au hamsini kwa hamsini huwa zinaishia kwenye mgawanyo wa majukumu huko ofisini kwenu, ndani ya vyama, au kwenye makampuni na kadhalika, ila ukivileta ndani ya nyumba huwa vinavunja ndoa, maana kwenye ndoa wewe mwanamke unatambuliwa k**a kitu kinachotakiwa kumilikiwa, kupendwa na kutunzwa kwa heshima. Kwenye Mithali 18:22 imeandikwa, "Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA." Pigia mstari hapo kwenye "KITU CHEMA" kwa kiingereza ni good thing.... Mwanamke wewe ni kitu yaani propert ya mumeo k**a vile nyumba yake, gari yake, simu yake, tv yake, nakadhalika, ila tofauti yako na hivyo vitu vingine ni kwamba una uwezo wa kujua jema na baya na pia umeunganishwa na roho yake,tendo linalokufanya uwe sehemu ya mwili wake.
Kwenye amri za Mungu sheria ya mke imeenda sambamba na sheria ya vitu na watumwa, ukisoma kitabu cha Kutoka 20:17 imeaandikwa, "Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako."
Nahitimisha kwa kukuambia mwanamke kuwa mwanaume ni mamlaka kubwa sana juu yako ambayo ili ikupe unachotaka ki hisia inabidi ujitengeneze kisaikolojia kuwa kitu chema kinachomilikika, ukija na Yes no nyiiingi utaishia kuwa super woman, mara mwanamke wa mithali na vile vimisemo vya what man can do even woman can do lakini ndoa itaota mbawa na kukukimbia you know....