The Open University of Tanzania

The Open University of Tanzania Tanzania’s Leading University in Open & Blended Learning. Affordable, Flexible and Accessible Nationally and Worldwide.

ELIMU, UJUZI, UBUNIFU & FURSA!OUT tupo Tanga katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026.Karibu Banda la OUT....
21/08/2026

ELIMU, UJUZI, UBUNIFU & FURSA!

OUT tupo Tanga katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026.

Karibu Banda la OUT.


Join Certified Data Protection Officer Programme (CDPOP) - Second Cohort and gain practical skills in data protection, p...
21/08/2026

Join Certified Data Protection Officer Programme (CDPOP) - Second Cohort and gain practical skills in data protection, privacy and compliance.

Registration: 14th Aug - 24th Sept 2026
Training: 28th Sept - 11th Oct 2026
Dodoma | Face-to-Face & Virtual.

Register today!


14/08/2026
Heri ya Sikukuu ya Nanenane.
08/08/2026

Heri ya Sikukuu ya Nanenane.


MoEST WATATHMINI MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA HEET, OUTWizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST) na Chuo Ki...
07/08/2026

MoEST WATATHMINI MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA HEET, OUT

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST) na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) wamefanya kikao kazi cha kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaotekelezwa na OUT, huku kwa pamoja wakisisitiza usimamizi madhubuti na kasi katika kukamilisha shughuli za mradi kwa viwango vinavyotarajiwa.

Kikao hicho kilichofanyika Agosti 3, 2026, makao makuu ya OUT, Kinondoni jijini Dar es Salaam, kiliongozwa na Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa HEET, Dkt. Kennedy Hosea na kuhudhuriwa na Naibu Makamu mkuu wa chuo anayesimamia Taaluma, Utafiti na Huduma za Kitaalam na Mratibu wa Mradi wa HEET kwa upande wa OUT, Prof. Saganga Kapaya, aidha kulihudhuriwa pia na wajumbe mbalimbali kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia na wajumbe wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Hosea alisisitiza umuhimu wa usimamizi wa karibu, uwajibikaji na ushirikiano kati ya Wizara na taasisi zinazotekeleza mradi huo ili kuhakikisha malengo yake yanafikiwa.
“Mradi wa HEET ni uwekezaji muhimu katika kuimarisha ubora na ushindani wa elimu ya juu nchini. Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa kila shughuli inayotekelezwa chini ya mradi inaleta matokeo yanayokusudiwa kwa kuzingatia muda, ubora na matumizi sahihi ya rasilimali,” alisema Dkt. Hosea.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa HEET kwa OUT, Prof. Saganga Kapaya, alisema kuwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kitaendelea kuhakikisha utekelezaji wa shughuli za mradi zinafanyika kwa ufanisi ili kuchangia katika kuboresha mazingira ya ufundishaji, ujifunzaji na utafiti pia kuimarisha utoaji wa elimu yenye ubora kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya kitaifa na kimataifa

Mradi wa HEET ni mpango wa Serikali unaolenga kuimarisha sekta ya elimu ya juu nchini kupitia uwekezaji katika miundombinu, teknolojia, utafiti, ubunifu na uendelezaji wa rasilimali watu, kwa lengo la kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.


06/08/2026

Kwanini uchague IMPTE?

Mkuu wa Kitivo cha Elimu, Dkt. Janet Kigobe, anakueleza kila unachohitaji kujua kuhusu Integrated Master of Primary Teacher Education (IMPTE).


Mradi wa ujenzi wa jengo la maabara za sayansi katika kituo cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) mkoa wa Mwanza umefi...
04/08/2026

Mradi wa ujenzi wa jengo la maabara za sayansi katika kituo cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) mkoa wa Mwanza umefikia asilimia 63 ya utekelezaji, ukiwa ni sehemu ya uwekezaji unaotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaolenga kuimarisha miundombinu ya kisasa ya kufundishia, kujifunzia na kufanya tafiti.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu (DVC-ARC), ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa HEET - OUT, Prof. Saganga Kapaya, alisema maendeleo yaliyofikiwa yanaonesha dhamira ya Chuo ya kuendelea kuwekeza katika miundombinu bora ya kufundishia na kujifunzia. Alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kazi zilizobaki zinakamilika kwa wakati, kwa ubora unaotakiwa na kuzingatia viwango vya usalama ili wanafunzi na wadau wengine waanze kunufaika na uwekezaji huo.

“Lengo letu ni kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati, kwa ubora unaokidhi viwango vinavyotakiwa na kuzingatia usalama katika kila hatua ya utekelezaji. Kukamilika kwake kutaiwezesha OUT kutoa mazingira bora zaidi ya kufundishia, kujifunzia na kufanya tafiti, huku wanafunzi na wadau wengine wakianza kunufaika na uwekezaji huu muhimu,” alisema Prof. Kapaya.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi wa Kituo cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kituo cha mkoa wa Mwanza, Dkt. Faustine Christopher, alisema ujenzi wa maabara hizo umekuja wakati muafaka kutokana na ongezeko la mahitaji ya mafunzo ya sayansi katika Kanda ya Ziwa, ambapo wanafunzi wamekuwa wakihitaji miundombinu ya kisasa inayowawezesha kujifunza kwa vitendo karibu na maeneo yao.

Mradi huu ni sehemu ya jitihada za Serikali kupitia Mradi wa HEET za kuimarisha elimu ya juu nchini kwa kuwekeza katika miundombinu ya kisasa ya kufundishia, kukufundishia, kujifunzia na kufanya tafiti, hatua inayolenga kujenga rasilimali watu wenye ujuzi, ubunifu na uwezo wa kuchangia maendeleo ya taifa.


Join the Bachelor of Arts in History and Cultural Heritage Management.One of the newly introduced programmes at the Open...
04/08/2026

Join the Bachelor of Arts in History and Cultural Heritage Management.

One of the newly introduced programmes at the Open University of Tanzania, gain the skills to protect, manage, and promote Tanzania's rich cultural and historical heritage for generations to come.


Join the Bachelor of Science in Accounting and Finance one of the newly introduced programmes at OUT.Build the expertise...
04/08/2026

Join the Bachelor of Science in Accounting and Finance one of the newly introduced programmes at OUT.

Build the expertise to lead in accounting, finance, auditing, investment, and business strategy.


Secure the Future. Shape the Digital World.Apply now.
04/08/2026

Secure the Future. Shape the Digital World.

Apply now.


Address

P. O. Box 23409, Off Kawawa Road, Kinondoni
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Open University of Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to The Open University of Tanzania:

Shortcuts

Share