TCRA CCC - Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano

TCRA CCC - Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano -
The Consumer Consultative Council of the Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA-CCC)

📍KUSINI UNGUJAK**ati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa  Kusini Unguja imeendesha mkutano wa elimu na uhamasi...
02/09/2026

📍KUSINI UNGUJA

K**ati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Kusini Unguja imeendesha mkutano wa elimu na uhamasishaji kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa watoto dhidi ya athari za matumizi mabaya ya huduma za mawasiliano.

K**ati imetoa elimu kwa wanafunzi wa Madrasa iliyopo katika Kijiji cha Bambi, Shehia ya Mitakawani, Jimbo la uzini, Wilaya ya Kati.

Mafunzo hayo yalihusu usalama wa mtoto mitandaoni, matumizi sahihi ya mtandao kwa watoto, pamoja na njia za kutoa taarifa pindi wanapobaini changamoto katika matumizi ya huduma za mawasiliano.

Katika hatua nyingine K**ati hiyo ilikutana na wajane katika Kijiji cha Mgeni Haji, Shehia ya Mgeni Haji, Jimbo la uzini, Wilaya ya Kati.

Akizungumza na wazazi hao, Mjumbe wa K**ati hiyo ndugu Mohamed Said alisema "watoto walioondokewa na wazazi wao ni wahanga zaidi wa matumizi mabaya ya mitandao, hivyo ni muhimu wazazi au walezi kuwa makini na kuwaelimisha mapema kabla ya athari kutokea".

Wazazi hao walielimishwa kuhusu matumizi sahihi ya mawasiliano na jinsi ya kuwalinda watoto wao dhidi ya athari zinazoweza kutokea kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya mawasiliano.

K**ati ya Watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Kusini Unguja inaendelea na jitihada za kuelimisha watumiaji ikiwa ni sehemu muhimu ya majukumu ya K**ati ya kuelimisha na kusambaza taarifa zenye maslahi ya watumiaji wa huduma za bidhaa za mawasiliano .

mtandaoni
wa mtoto mtandaoni
kwa uma

Tabora📍K**ati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Tabora imefanya mkutano wa kuelimisha na kuhamasisha vijana ...
31/08/2026

Tabora📍

K**ati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Tabora imefanya mkutano wa kuelimisha na kuhamasisha vijana wa Kanisa la FPCT-Ipuli mkoani Tabora tarehe 29 Agosti 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mafunzo hayo, mwakilishi wa K**ati hiyo alisema kuwa lengo kuu ni kuwaelimisha vijana kuhusu masuala muhimu yanayogusa maslahi ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano.

Masuala hayo ni pamoja na haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano, matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, pamoja na ulinzi wa taarifa binafsi ili kujikinga na utapeli na uhalifu wa kimtandao.

Katika mafunzo hayo jumla ya vijana 33 walishiriki, ambapo kati yao walikuwa wasichana 20 na wavulana 13. Vijana hao walionyesha kuridhishwa na elimu waliyoipata na kuahidi kuitumia katika maisha yao ya kila siku.

Naye mwenyekiti wa K**ati ya watumiaji ya Mkoa wa Tabora amesema kuwa k**ati hiyo itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini, shule na makundi mbalimbali ya kijamii kuhakikisha elimu ya ulinzi wa mtumiaji inafika kwa wananchi wote. Alisisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa kila mtumiaji anapata huduma bora na anafahamu haki zake

29/08/2026
MorogoroK**ati ya Watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Morogoro imefanya ziara na kutoa elimu kwa wananchi wakati ...
28/08/2026

Morogoro

K**ati ya Watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Morogoro imefanya ziara na kutoa elimu kwa wananchi wakati wa Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika Mkoani Morogoro.

Akizungumza na wananchi katika tamasha hilo, Mwenyekiti wa k**ati hiyo Ndug.Samweli Msuya amesema wamekuwa wakitoa elimu juu ya matumizi mazuri ya huduma za mawasiliano. Pia wametoa elimu kwa watumiaji kuhusu haki na wajibu wao pamoja na jinsi ya kutoa taarifa iwapo kuna viashiria vya utapeli mitandaoni.

Mbali na kutoa elimu, k**ati hiyo pia imetoa na kugawa vipeperushi mbalimbali kwa washiriki wa tamasha hilo ili kuwaongezea uelewa kuhusu masuala ya mawasiliano na ulinzi dhidi ya utapeli mtandaoni.

Tamasha la Kitaifa la Utamaduni linaloendelea Mkoani Morogoro limekuwa jukwaa la kuwafikia wananchi wengi na kuwapa uelewa juu ya masuala mbalimbali ikiwemo matumizi salama ya teknolojia na mawasiliano

Tunawatakia Waislamu na Watanzania Wote, Sikukuu Njema.
25/08/2026

Tunawatakia Waislamu na Watanzania Wote, Sikukuu Njema.

24/08/2026


Ni jukumu letu sote kuhakikisha watoto wanakuwa salama pindi watumiapo mitandao. Tuwaelimishe watoto kuhusu matumizi sah...
22/08/2026

Ni jukumu letu sote kuhakikisha watoto wanakuwa salama pindi watumiapo mitandao. Tuwaelimishe watoto kuhusu matumizi sahihi ya mitandao.


📍Kusini UngujaK**ati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Kusini Unguja imefanya mkutano na waratibu wa masuala...
19/08/2026

📍Kusini Unguja

K**ati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Kusini Unguja imefanya mkutano na waratibu wa masuala ya jinsia, wazee na watoto katika Shehia za Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

K**ati imetumia fursa hiyo kufahamiana na kujengea uwezo washiriki kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi kwa watumiaji ikiwemo fursa zilizoko katika sekta ya mawasiliano.

K**ati imesisitiza umuhimu wa ushirikiano ili kuweza kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuhakikisha watumiaji wanapata uelewa wa masuala ya sekta ya mawasiliano.

K**ati ilipokea maoni na maswali kutoka kwa washiriki na kuyatolea ufafanuzi.

Aidha; washiriki wameahidi kutoa ushirikiano kwa K**ati katika utekelezaji wa shughuli zake ili kusaidia kupunguza changamoto zinazowakabili watumiaji katika Mkoa wa Kusini Unguja.

KAMATI YA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO YATOA ELIMU SHULE YA MSINGI KAGERA KIGOMAK**ati ya Watumiaji wa Huduma za M...
17/08/2026

KAMATI YA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO YATOA ELIMU SHULE YA MSINGI KAGERA KIGOMA

K**ati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano imefanya kampeni ya kutoa elimu kwa wanafunzi katika Shule ya Msingi Kagera iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Mada kuu ililenga kuelimisha kuhusu matumizi sahihi na salama ya huduma za mawasiliano na Kufahamu haki zao K**a watumiaji Wa huduma za mawasiliano.

Aidha; K**ati imewataka wanafunzi hao kusambaza elimu hiyo kwa wazazi na walezi wao ili kuepuka changamoto mbalimbali zitokanazo na matumizi yasiyo sahihi ya huduma za mawasiliano.

Akizungumza na wanafunzi hao, katibu wa K**ati bi. Bertha mshana alisema "Wanafunzi k**a walivyo watumiaji wengine wanaweza kukumbwa na changamoto k**a vile udhalilishaji, utapeli au kuibiwa taarifa binafsi na kutumika vibaya na watu wasio na nia njema, hivyo ni muhimu kwa elimu hii kuwafikia" alisisitiza bi. Mshana.

Baraza kupitia K**ati za watumiaji za Mikoa limekuwa likiendesha kampeni ya elimu na usambazaji wa taarifa muhimu zenye maslahi watumiaji kwa lengo la kuongeza uelewa wa watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini.

10/08/2026

Dar es Salaam📍

Waziri wa mawasiliano na Teknolojia ya habari Angela Kairuki amewataka wananchi kutoa taarifa dhidi ya watoa huduma za mawasiliano ambao hawatumii namba rasmi ya kampuni za mawasiliano ( 100) kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia namba 15040 mara tu utakapopigiwa au kupokea ujumbe kutoka kwa mtu anayedai kuwa ni mtoa huduma wa kampuni fulani ya mawasiliano.

Akizungumza leo, Agosti 10, 2026, wakati wa uwasilishaji wa Ripoti ya Utendaji ya Robo ya Nne ya mwaka wa Fedha 2025/26 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), amesema "....Ukiona umepigiwa simu au umefanyiwa mawasiliano na kampuni ya mtoa huduma za simu kupitia namba ambayo ni nje na siyo namba 100 wala usihangaike nae wew tuma ujumbe kwetu kwenye namba 15040 tuwekee ile namba ambayo ilikupigia...."

Hata hivyo Amewahakikishia wananchi kuwa Wizara inaendelea na jitihada za kukabiliana na vitendo vya ulaghai kupitia huduma za mawasiliano , kwani bado haijafikia kiwango cha kutokomeza tatizo hili kabisa.

Address

14 Jamhuri Street
Dar Es Salaam
11470DARESSALAAM,

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Telephone

+255652966633

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TCRA CCC - Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to TCRA CCC - Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano:

Shortcuts

Share