14/04/2026
KIWOHEDE kwa Kushirikiana na UNFPA Wawawezesha Mabinti Vijana Kigoma
KIWOHEDE kwa kushirikiana na UNFPA katika mkoa wa Kigoma Region, wamebaini na kusajili mabinti 50 waliozaa katika umri mdogo (First Time Young Mothers) katika Chuo cha Ufundi cha Maendeleo ya Wananchi cha Kihinga FDC.
Lengo la mpango huu ni kuwawezesha mabinti hao kupata ujuzi wa kujitegemea katika fani mbalimbali ikiwemo ushonaji, ufundi magari, kilimo, uchomeleaji na nyinginezo. Kupitia mafunzo haya, wanatarajiwa kujiajiri na kujikwamua kiuchumi, pamoja na kuboresha maisha yao na familia zao.
Washiriki hawa wanatoka katika halmashauri nne za mkoa wa Kigoma ambazo ni Kakonko District, Kibondo District, Kasulu Town Council na Kasulu District Council.
Mafunzo haya yamefunguliwa rasmi na Afisa Maendeleo wa Mkoa wa Kigoma, Msafiri Nzunuri, ambaye alisisitiza umuhimu wa kuwajengea uwezo mabinti vijana ili waweze kuwa na maisha bora na yenye kujitegemea. UNFPA Tanzania