HESLB Tanzania

HESLB Tanzania Official page for Higher Education Students' Loans Board (HESLB)

19/08/2026
Prof. Mkenda Afungua Rasmi Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Jijini TangaWaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia...
19/08/2026

Prof. Mkenda Afungua Rasmi Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Jijini Tanga

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda leo (Agosti 18, 2026) amefungua rasmi Maonesho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, Jijini Tanga.

Mhe. Prof. Mkenda amemwakilisha Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ambapo pia viongozi mbalimbali wamehudhuria hafla hiyo ya ufunguzi akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian ambaye amewakaribisha wageni kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo mkoani humo ukiutaja Tanga kuwa ni ‘lango la biashara la nchi za Afrika Mashariki na SADC’.

Maonesho hayo yanayolenga kuhamasisha na kuonesha mchango wa elimu, ujuzi na ubunifu katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa, yalianza Agosti 15, 2026 na yanatarajiwa kufikia tamati Agosti 24, 2026, yakiwa na kauli mbiu isemayo: “Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Njia ya Kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inashiriki kwa kutoa elimu na uelewa kwa wananchi na wadau mbalimbali kuhusu huduma inazotoa, hususan namna sahihi ya kuomba mikopo ya elimu ya juu pamoja na urejeshaji wa mikopo iliyoiva.

Ushiriki wa HESLB unalenga kuwafikia wanafunzi, wazazi, walezi na wananchi kwa ujumla ili kuwapatia taarifa sahihi kuhusu fursa za mikopo ya elimu ya juu, taratibu za maombi pamoja na wajibu wa wanufaika katika kurejesha mikopo yao kwa wakati.

Aidha, maonesho hayo yanatoa fursa kwa taasisi mbalimbali za elimu, wadau wa sekta ya elimu, wanafunzi na wananchi kukutana, kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu maendeleo ya elimu, ujuzi na ubunifu nchini.

HESLB inaendelea kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kutembelea banda lake katika maonesho hayo ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, ili kupata elimu na ufafanuzi kuhusu uombaji wa mikopo ya elimu ya juu na urejeshaji wa mikopo iliyoiva.

HESLB YASHIRIKI UAPISHO WA MAKAMU MKUU MPYA WA SAUTBodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Agosti 10, 20...
12/08/2026

HESLB YASHIRIKI UAPISHO WA MAKAMU MKUU MPYA WA SAUT

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Agosti 10, 2026 imeshiriki hafla ya uapisho wa Makamu Mkuu mpya wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Prof. Emmanuel Charles Wabanhu, iliyofanyika jijini Mwanza.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa HESLB Kanda ya Mwanza ameipongeza SAUT kwa mchango wake katika kutoa elimu ya juu na kuandaa wataalamu wanaochangia maendeleo ya Taifa.

Amesema HESLB itaendelea kushirikiana kwa karibu na uongozi wa SAUT kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji ya kifedha na wanaokidhi vigezo wanapata fursa ya kupata mikopo ya elimu ya juu na kuendelea na masomo bila vikwazo vya kifedha.

Aidha, HESLB imewahakikishia viongozi wa SAUT kuwa ipo tayari kuendelea kushirikiana nao katika kutatua changamoto zinazohusiana na mikopo ya wanafunzi, huku ikiwakaribisha kutembelea Ofisi za HESLB Kanda ya Mwanza zilizopo katika Jengo la PSSSF Plaza ghorofa ya pili kwa ajili ya mazungumzo na ushauri.

HESLB inampongeza na kumtakia Prof. Wabanhu kila la heri na mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yake mapya k**a Makamu Mkuu wa Chuo cha SAUT. HESLB inaamini kuwa uongozi wake utaleta chachu katika kuimarisha ubora wa elimu, pamoja na kuendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano mzuri uliopo kati ya SAUT na HESLB kwa manufaa ya wanafunzi na Taifa kwa ujumla.

06/08/2026

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wakitoa elimu na uhamasishaji kwa waombaji watarajiwa wa 'Ngorongoro Scholarship' ili kuwawezesha kuelewa vigezo vya scholarship na kujaza maombi yao kwa usahihi na kwa wakati.

Dirisha la maombi ya Ngorongoro Scholarship litafunguliwa Agosti 15, 2026. Wazazi, walezi, viongozi wa jamii na vijana wote kutoka ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wanahimizwa kusoma mwongozo wa 'Ngorongoro Scholarship' kwa mwaka 2026/2027 unaopatikana kwenye tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) ili kuelewa sifa, vigezo na taratibu za kuomba Scholarship hii.

HESLB NA NCAA WAZINDUA MWONGOZO WA NGORONGORO SCHOLARSHIP HESLB kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NC...
06/08/2026

HESLB NA NCAA WAZINDUA MWONGOZO WA NGORONGORO SCHOLARSHIP

HESLB kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) leo Agosti 04, 2026 imezindua Mwongozo wa Utoaji wa Ngorongoro Scholarship, inyowalenga wanafunzi wanaotoka katika jamii zinazoishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kuanzia mwaka wa masomo 2026/2027.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari katika Ofisi za HESLB Kanda ya Mashariki, Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, amesema uzinduzi huo ni utekelezaji wa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) yaliyosainiwa kati ya HESLB na NCAA tarehe 24 Oktoba, 2025, yenye lengo la kuongeza fursa za elimu ya juu kwa vijana wa Ngorongoro.

"Kuanzia mwaka wa masomo 2026/2027, HESLB kwa kushirikiana na NCAA itaanza kutoa ufadhili maalum wa elimu ya juu kwa wanafunzi wanaotoka katika jamii za Hifadhi ya Ngorongoro," amesema Dkt. Kiwia.
Alieleza kuwa katika awamu ya kwanza, wanafunzi 15 watanufaika na ufadhili huo, huku NCAA ikitenga shilingi milioni 99 kugharamia masomo yao. Aidha, alisema dirisha la maombi linatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 15 Agosti 2026 kupitia mfumo wa kidijitali wa HESLB.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi wa NCAA, Bi. Gloria Bideberi, amesema mpango huo unaonesha dhamira ya NCAA ya kuwekeza katika maendeleo ya jamii kupitia elimu sambamba na kuimarisha juhudi za uhifadhi.

"Ngorongoro Scholarship inaashiria dhamira ya NCAA ya kuwekeza katika rasilimali watu kupitia elimu. Tunaamini maendeleo ya uhifadhi hayawezi kutenganishwa na maendeleo ya watu, ndiyo maana tumeamua kushirikiana na HESLB kuhakikisha kila mwanafunzi anayekidhi vigezo anapata fursa ya kufadhiliwa," amesema Bi. Bideberi.

Alibainisha kuwa NCAA imekuwa ikiwezesha elimu kwa watoto wa jamii za Ngorongoro kwa zaidi ya miongo mitatu, ambapo hadi mwaka wa fedha 2025/2026 zaidi ya wananchi 15,000 walikuwa wamepatiwa ufadhili katika taaluma mbalimbali. Aidha, alisema kupitia Ngorongoro Fund yenye kaulimbiu "Elimu Endelevu kwa Maendeleo ya Jamii na Uhifadhi," ufadhili utaanza kwa wanafunzi wa fani zinazohusiana na uhifadhi wa wanyamapori, misitu, malikale na utalii, huku wigo ukitarajiwa kupanuliwa kadri mfuko utakavyoendelea kukua.

Address

P. O Box 76068
Dar Es Salaam

Opening Hours

Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00

Telephone

+255222864640

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HESLB Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to HESLB Tanzania:

Shortcuts

Share