ACT Wazalendo

ACT Wazalendo ACT Wazalendo ni chama cha siasa kilichoundwa kwa kufuata misingi ya Ujamaa wa Kidemokrasia na chenye shabaha kuu ya kusimamia Mabadiliko na Uwazi nchini.

Official page ya Chama cha ACT-Tanzania

MTUTURA:  SERIKALI ISITISHE VIBALI VYA BANDARI KAVUWaziri Kivuli wa Ujenzi, Uchukuzi na Miundombinu wa ACT Wazalendo, Mt...
30/08/2026

MTUTURA: SERIKALI ISITISHE VIBALI VYA BANDARI KAVU

Waziri Kivuli wa Ujenzi, Uchukuzi na Miundombinu wa ACT Wazalendo, Mtutura Abdallah Mtutura, ameitaka Serikali kusitisha mara moja utoaji wa vibali vipya vya Bandari Kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam, huku bandari kavu zilizopo zipatiwe muda wa miezi sita kusitisha huduma zinazofanyika katikati ya jiji, pembezoni mwa barabara na maeneo yanayosababisha usumbufu kwa wananchi.

Akizungumza leo tarehe 30 Agosti 2026 na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo, Mtutura amesema ongezeko la Bandari Kavu katika maeneo ya makazi na pembezoni mwa barabara limekuwa likisababisha madhila kwa wananchi, ikiwemo msongamano wa magari, uharibifu wa miundombinu na changamoto za usalama, huku likidhoofisha uchumi wa Dar es Salaam.

Mtutura amesema Bandari Kavu (ICDs) zimekuwa na uhusiano na wafadhili wa CCM pamoja na baadhi ya vigogo wa Serikali, akidai kuwa mfumo huo umetengeneza mwanya wa watu wenye maslahi binafsi kuunganisha biashara za bandari na kampuni zao za usafirishaji wa mizigo kwa lengo la kujipatia faida.

“Bandari kavu (ICDs) zina mizizi ya wafadhili wa CCM na vigogo wa Serikali ambao wametengeneza mwanya wa Bandari na makampuni yao ya usafirishaji wa mizigo ili kujipatia faida huku wakiacha madhila makubwa kwa wananchi na kudhoofisha uchumi wa Dar es Salaam,” amesema Mtutura.

Mtutura ameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kwa kusitisha utoaji wa vibali vipya vya Bandari Kavu, kufanya mapitio ya maeneo yote yenye ICDs na kuwapa waliopo muda wa miezi sita kuondoa shughuli hizo katika maeneo ya katikati ya jiji, pembezoni mwa barabara na maeneo yasiyokidhi vigezo vya mipango miji.

TAARIFA KWA UMMA"Mfumo wa Bima ya Afya chini ya CCM haufai, ni wa kibaguzi na matabaka: Tathmini ya ACT kuhusu Utekeleza...
27/08/2026

TAARIFA KWA UMMA

"Mfumo wa Bima ya Afya chini ya CCM haufai, ni wa kibaguzi na matabaka: Tathmini ya ACT kuhusu Utekelezaji Ahadi ya Siku 100 za Rais Samia katika Afya,Bima ya Afya kwa Wote". Dkt. Elizabeth Benedict Sanga
Waziri Kivuli Afya na Ustawi wa Jamii
27 Agosti, 2026.

22/08/2026

"Tunataka Katiba itakayoimarisha na kurejesha mamlaka ya maamuzi kwa Wananchi. Tunataka Katiba ya Wote kwa Maslahi ya Wote."

Kiongozi wa ACT Wazalendo
Dorothy Semu

Mwenyekiti wa  Taifa, Ndugu  akiambatana Makamu Mwenyekiti .jussa atafanya ziara maalum Unguja kuanzia Agosti 24, 2026 h...
20/08/2026

Mwenyekiti wa Taifa, Ndugu akiambatana Makamu Mwenyekiti .jussa atafanya ziara maalum Unguja kuanzia Agosti 24, 2026 hadi Agosti 29, 2026.

Chama cha ACT Wazalendo  kupitia Waziri Kivuli wa Habari, Shangwe Ayo  tumelaani kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi kwa...
20/08/2026

Chama cha ACT Wazalendo kupitia Waziri Kivuli wa Habari, Shangwe Ayo tumelaani kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi kwa kipindi cha miezi sita.

Wito wetu
Tumeitaka Serikali isimamishe mara moja adhabu hiyo kwa Mwanahalisi na irudishe leseni yake.

TAARIFA KWA UMMA "Tunalaani Kusitishwa kwa Leseni ya Gazeti la Mwanahalisi. Tunaitaka Serikali isimamishe mara moja adha...
19/08/2026

TAARIFA KWA UMMA

"Tunalaani Kusitishwa kwa Leseni ya Gazeti la Mwanahalisi. Tunaitaka Serikali isimamishe mara moja adhabu dhidi ya MwanaHALISI na kurejesha leseni yake."

Waziri Kivuli wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa ACT Wazalendo.



19/08/2026

"Hatutaki Katiba itakayoibeba CCM, tunataka Katiba ya wote kwa maslahi ya wote."

Kiongozi wa ACTwazalendo
Dorothy Semu

18/08/2026

"Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea kulaani mauaji yaliyotokea Oktoba 2025 na kinataka wafungwa wote wa kisiasa waachiwe huru."

Kiongozi wa ACT Wazalendo
Dorothy Semu

Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ndugu Ismail Jussa. Sote tunamtakia heri na b...
18/08/2026

Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ndugu Ismail Jussa. Sote tunamtakia heri na baraka anapoadhimisha siku hii adhimu kwake.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ACT Wazalendo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share