02/09/2026
Matukio mengi mabaya huwa ni marudio ya kile ambacho kimeshafanyika kwenye ulimwengu wa roho, na tunapoomba rehema tunamuomba Mungu atuepushe na hiyo adhabu.
Ndio maana kwenye;
📖 Kutoka 34:7
mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.
Wewe upo kizazi cha ngapi?
📖 Warumi 8:1
Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Ni kwa sababu kuna damu ya Yesu ambayo ilimwagika kwa ajili ya kuturehemu na ndio maana hakuna hukumu ya adhabu juu ya walio katika Kristo Yesu.
Pamoja na hayo yote, ni muhimu pia kujua ni adhabu gani ambayo iliachiliwa kwenye ulimwengu wa roho kutokana na kilichofanyika kutokana na matukio yaliyotokea.
Chochote ambacho kinakutesa au unajitahidi kukiacha na unashindwa ilhali unajua kabisa sio mapenzi ya Mungu, jua lazima kina connection ya damu ya unapotokea, kuna kilichofanyika na kikafanya adhabu ikaachiliwa...hapa hautoki kwa kukemea bali rehema.
📖 Kumbukumbu la Torati 23:2
Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa BWANA; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa BWANA.
Hapa kuna vizazi kumi ambavyo vimekataliwa, k**a mtu amezaliwa vizazi ndani ya hivi kumi anaweza kwenda kanisani, akatamkiwa baraka lakini hatoona matokeo yoyote. Huyu anaweza kuwa na bidii sana lakini akaishia kwenye umasikini, yaani hakuna kinachoenda kwake.
Hawa watu Mungu alikuwa ameachilia adhabu kwao, wewe kwenu kuna adhabu gani iliyoachiliwa? na ni nini kilifanyika kikapelekea adhabu hiyo kuachiwa?
Leo katika siku hii ya tatu ya mfungo tulikuwa na maombi ya rehema tukimuamini Mungu kuturehemu na kuondoa adhabu na madhara ya adhabu yaliyokuwa yameachiliwa kwetu na kwenye koo zetu.