19/08/2026
Karibu Tanzania 🇧🇪 🇹🇿
Tunayo furaha kumkaribisha Bi. Lot Debruyne, Balozi mteule wa Ubelgiji nchini Tanzania, aliyewasili jijini Dar es Salaam. Ataanza rasmi majukumu yake baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho, na baadaye atafanya vivyo hivyo nchini Komoro, Malawi, Mauritius na Zambia, ambazo pia zinahudumiwa na Ubalozi huu.
Ni mwanadiplomasia wa kitaaluma mwenye uzoefu wa takribani miongo miwili katika mahusiano ya kimataifa, masuala ya kisiasa na haki za binadamu. Anatujia kutoka Kinshasa, alikohudumu k**a Naibu Mkuu wa Ubalozi. Amewahi pia kuhudumu Thailand, Misri, na katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ubelgiji katika Umoja wa Ulaya, na kuwa Mshauri wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Ubelgiji.
Amewasili na familia yake — pamoja na paka wake kutoka Congo 🐈. Nje ya ofisi anapenda kupika, mazoezi ya Pilates na kitesurfing, na tayari ameanza kuuliza wapi kuna upepo mzuri zaidi.
💬 Ulizeni Balozi. Andika swali lako katika maoni, na atajibu baadhi ya maswali kwa njia ya video.
Karibu Tanzania, Balozi.
——
Welcome to Tanzania 🇧🇪 🇹🇿
We are pleased to welcome Mrs Lot Debruyne, Belgium's Ambassador-designate to the United Republic of Tanzania, who has arrived in Dar es Salaam. She will formally take up her functions upon presentation of her Letters of Credence, and will subsequently present credentials in Comoros, Malawi, Mauritius and Zambia, also covered by the Embassy.
A career diplomat with nearly two decades in international relations, political affairs and human rights, she joins us from Kinshasa, where she was Deputy Head of Mission. She has also served in Thailand, Egypt and at Belgium's Permanent Representation to the EU, and advised the Belgian Minister of Foreign Affairs and Defence.
She arrives with her family — and with a Congolese cat 🐈. Outside the office she cooks, practises Pilates and kitesurfs, and has already started asking where to find the best wind.
💬 Ulizeni Balozi — ask the Ambassador. Leave your question in the comments and she will answer a selection of them on video. Karibu Tanzania, Balozi.