Tanesco

Tanesco Ukurasa rasmi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)

04/09/2026

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME

📌 Kukamilika kwa njia mpya kutatoa fursa kwa njia ya awali kuendelea kunufaisha wananchi wa mkoa wa Geita na kuchochea shughuli za kiuchumi.

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME📌 Kukam...
04/09/2026

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME

📌 Kukamilika kwa njia mpya kutatoa fursa kwa njia ya awali kuendelea kunufaisha wananchi wa mkoa wa Geita na kuchochea shughuli za kiuchumi.

📌 Serikali yawekeza takribani Shilingi bilioni 63.19 kuutekeleza

Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inaendelea kuimarisha miundombinu ya umeme nchini kupitia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Mpomvu hadi kituo cha kupokea na kupoza umeme cha GGM, wenye urefu wa takribani kilomita 6.7.

Akizungumza Septemba 3, 2026, jijini Dodoma, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema kukamilika kwa mradi huo kutaimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuchochea shughuli za kiuchumi, ikiwemo uzalishaji, ajira, ongezeko la mapato na uwekezaji.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na TANESCO na wadau wa sekta ya nishati kuhakikisha miundombinu ya umeme inaendana na kasi ya ukuaji wa mahitaji.

“Serikali itaendelea kushirikiana na TANESCO na wadau wote wa sekta ya nishati kuhakikisha miundombinu ya umeme inaendana na kasi ya ukuaji wa mahitaji. Tunataka kuona umeme unaozalishwa nchini ukitumika kikamilifu kuchochea uzalishaji, kuongeza ajira, kuongeza mapato na kuvutia uwekezaji zaidi. Mradi huu ni kielelezo cha falsafa hiyo,” amesema Mhe. Salome.

03/09/2026

UMEME KUBADILISHA MAISHA YA WAKQZI WA KISIWA CHA JIBONDO MAFIA.

📍Wananchi zaidi ya 3,000 kunufaika na Mradi.

📍Waeleza Umeme utachochea Maendeleo, Waipongeza TANESCO kuwapelekea Umeme.

UMEME KUBADILISHA MAISHA YA WAKAZI WA KISIWA CHA JIBONDO MAFIA.📍Wananchi zaidi ya 3,000 kunufaika na Mradi.📍Waeleza Umem...
03/09/2026

UMEME KUBADILISHA MAISHA YA WAKAZI WA KISIWA CHA JIBONDO MAFIA.

📍Wananchi zaidi ya 3,000 kunufaika na Mradi.

📍Waeleza Umeme utachochea Maendeleo, Waipongeza TANESCO kuwapelekea Umeme.

Na MwandishinWetu, Mafia – Pwani

Zaidi ya wananchi 3,000 wa Kisiwa cha Jibondo, Wilaya ya Mafia, Mkoa wa Pwani, wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya umeme baada ya Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutekeleza mradi wa kusambaza umeme katika kisiwa hicho wenye thamani ya Sh bilioni 8.4.

Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Septemba 2026, ambapo kwa sasa umefikia asilimia 82 ya utekelezaji na unatarajiwa kubadilisha maisha ya wananchi kwa kufungua fursa mpya za kiuchumi, kuongeza shughuli za uzalishaji na kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii.

Wananchi hai wameeleza kuwa kwa muda mrefu, wakazi wa Jibondo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme, hali iliyokuwa ikiathiri shughuli zao za kiuchumi, hususani zinazohusisha uvuvi, uchakataji na uhifadhi wa mazao ya bahari.

Wananchi wanasema kukosekana kwa umeme kuliwafanya kushindwa kutumia fursa mbalimbali za kuongeza thamani ya mazao yao na kuanzisha viwanda vidogo vya kuchakata samaki na bidhaa nyingine za baharini.

Hata hiyo wamesema uwepo wa umeme sasa unakwenda kuleta matumaini mapya, huku wakitarajia kuanzisha biashara na shughuli za uzalishaji zitakazowaongezea kipato, kuunda ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa eneo hilo.

“Kabla ya umeme wananchi wa Kata ya Jibondo na kisiwa hiki walikuwa katika mazingira magumu sana kwani walikosa baadhi ya fursa za kiuchumi kwa sababu hawakuwa na umeme. Tunaipongeza TANESCO kwa kutuletea umeme; fursa mbalimbali zinafunguka na uchumi utazidi kukua,” amesema Hassan Mohamed, Diwani wa Kata ya Jibondo.

03/09/2026
Taarifa Kwa Wateja wa Mkoa wa Kinondoni
03/09/2026

Taarifa Kwa Wateja wa Mkoa wa Kinondoni

02/09/2026

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI

📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo halali ya umeme eneo la Visiwani, Mwananyamala na Mivumoni

📌 TANESCO yawataka wananchi kutoa taarifa za vitendo vya wizi wa umeme

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limebaini matukio ya wizi wa umeme katika eneo la Visiwani, Mwananyamala na Mivumoni, zilizo Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, wakati wa operesheni ya ukaguzi wa mita na miundombinu ya umeme inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

Operesheni hiyo inalenga kudhibiti matumizi yasiyo halali ya umeme, kulinda miundombinu ya Shirika na kuhakikisha huduma ya umeme inaendelea kutolewa kwa usalama na ufanisi kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa operesheni hiyo, Afisa Usalama wa TANESCO, Bi. Lilian Nizim, amewataka wananchi kuzingatia sheria na taratibu za matumizi ya umeme na kuepuka vitendo vya kuingilia au kuchezea mita za umeme.

“Mteja anapobaini changamoto yoyote inayohusiana na mita yake, anapaswa kutoa taarifa TANESCO ili ipatiwe ufumbuzi. Ni muhimu wananchi waepuke kabisa kuingilia mita kwa njia yoyote, kwani ni kinyume cha sheria na kunaweza kuhatarisha usalama wa maisha na mali,” amesema Bi. Nizim.

Kwa upande wake, Mhandisi wa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kaskazini, Mha. Underson Manyika, amesema wakati wa ukaguzi katika eneo la Visiwani, timu ya wataalamu ilibaini baadhi ya wateja wakiwa wamechepusha nyaya za umeme, hali iliyosababisha mita kutosoma matumizi halisi ya umeme.

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo hala...

TAARIFA KWA UMMA; UTEKELEZAJI WA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA
30/08/2026

TAARIFA KWA UMMA; UTEKELEZAJI WA ZOEZI LA UKAGUZI WA MITA

Address

Jamatini Street
Dodoma Outlying
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanesco posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tanesco:

Shortcuts

Share