01/09/2026
WAKAGUZI NAOT WASHIRIKI WARSHA YA KIKANDA YA AFRIKA MASHARIKI KUIMARISHA UBORA NA UKAGUZI
Wakaguzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) wanashiriki katika Warsha maalumu ya Kikanda ya Afrika Mashariki jijini Arusha, inayolenga kuimarisha Usimamizi wa Ubora na Ukaguzi wa Utendaji katika Taasisi Kuu za Ukaguzi (SAIs).
Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, Bw. Novati Mfalamagoha, amesema kuwa ushirikiano wa Ukaguzi Kikanda ni nguzo muhimu katika kukabiliana na changamoto zinazofanana zinazozikabili Taasisi Kuu za Ukaguzi ndani ya Afrika Mashariki na kwamba fursa hii ni muhimu kwa Wakaguzi kubadilishana ujuzi na uzoefu ili kuzidi kujenga mifumo imara ya usimamizi wa ubora wa Ukaguzi.
Warsha hiyo inawakutanisha Wakaguzi kutoka Mataifa ya Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda, pamoja na wawezeshaji kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ya Sweden inalenga pamoja na masuala mengine kubadilishana uzoefu ili kuzidi kuzijengea uwezo Taasisi Kuu za Ukaguzi za Afrika Mashariki katika maeneo mbalimbali k**a vile kuimarisha mifumo ya Ukaguzi.