ortamisemi

ortamisemi Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from ortamisemi, Government Organization, Dodoma.

RAIS SAMIA ATAKA MIKOA, HALMASHAURI KUIMARISHA UKUSANYAJI WA MAPATONa OWM - TAMISEMI, ZanzibarRais wa Jamhuri ya Muungan...
02/09/2026

RAIS SAMIA ATAKA MIKOA, HALMASHAURI KUIMARISHA UKUSANYAJI WA MAPATO

Na OWM - TAMISEMI, Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka Viongozi wa Mikoa na Wilaya kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kudhibiti matumizi na kuelekeza rasilimali katika vipaumbele vya maendeleo, hususan sekta za elimu na afya.

Rais Dkt. Samia ametoa maagizo hayo leo Septemba 2, 2026, wakati wa hafla ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa na Katibu Tawala wa Mkoa iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar.

“Kila mwenye eneo lake la utawala ajitahidi kuhakikisha mambo yanaenda katika eneo lake; si kila kitu kitoke kwenye Hazina ya Serikali,” amesema Rais Dkt. Samia.

Aidha, amezitaka Halmashauri kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuimarisha utoaji na urejeshaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, huku mikopo hiyo ikielekezwa katika miradi inayozalisha.

Pia, ameelekeza mapato ya ndani yatumike kupanua na kujenga masoko, kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara wadogo na kugharamia miradi ya maendeleo. Amesisitiza kuwa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2025 na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 unahitaji viongozi kuwajibika na kusimamia matokeo.

Walioapishwa kuwa Wakuu wa Mikoa ni Mhe. Jumanne Abdallah Sagini wa Mbeya, Mhe. Alexander Pastory Mnyeti wa Geita, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo wa Pwani na Mhe. CP Salum Rashid Hamduni wa Mwanza. Bw. Richard Marcellino Kayombo ameapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.

02/09/2026
SERIKALI YAWEKA MKAKATI KUKAMILISHA MIUNDOMBINU YA VITUO 364 – DKT. SEIFNa: OWM - TAMISEMINaibu Waziri Ofisi ya Waziri M...
01/09/2026

SERIKALI YAWEKA MKAKATI KUKAMILISHA MIUNDOMBINU YA VITUO 364 – DKT. SEIF

Na: OWM - TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Dkt. Jafar Seif amesema Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa awamu kwa ajili ya kukamilisha miundombinu muhimu katika vituo vya afya 364 nchini, ikiwemo Kituo cha Afya Myangayanga kilichopo kata ya Myangayanga, Jimbo la Mbinga Mjini, ili vituo hivyo viweze kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.

Dkt. Seif ameyasema hayo leo, Septemba 1, 2026, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu Swali la Mbunge wa Mbinga Mjini, Mhe. Jonas Mbunda, aliyetaka kujua ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Myangayanga, ambapo amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 23.37 katika mwaka wa fedha 2026/27 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika vituo vya afya 111, kikiwemo Kituo cha Afya Myangayanga.

Aidha, Dkt. Seif amesema Kituo cha Afya Myangayanga ni miongoni mwa vituo 364 vyenye upungufu wa miundombinu muhimu, ambapo Serikali itaendelea kutekeleza ujenzi kwa awamu, ikiwemo ujenzi wa jengo la upasuaji, wodi na jengo la kufulia, hatua inayolenga kuimarisha uwezo wa vituo hivyo kutoa huduma bora za afya.

Amesema katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali ilitoa Shilingi Milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Myangayanga, ambapo fedha hizo zilitumika kujenga jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD) pamoja na jengo la maabara.

Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuendelea kuimarisha miundombinu ya afya nchini kwa kuwekeza katika ujenzi na ukamilishaji wa majengo muhimu katika vituo vya afya, lengo likiwa ni kuongeza uwezo wa vituo hivyo kutoa huduma za afya zilizo bora, salama na zinazokidhi mahitaji ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

01/09/2026

SERIKALI YAAHIDI FEDHA KUKAMILISHA UKARABATI WA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA KUELEKEA JUBILEE YA MIAKA 100

SERIKALI imeahidi kupeleka fedha mapema kwa ajili ya kuendelea na ukarabati wa miundombinu iliyobaki katika Shule ya Sekondari Tosamaganga, Iringa, kuelekea maadhimisho ya miaka 100 ya shule hiyo yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 2026.

Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu–Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange, kwa Niaba ya Waziri wa Nchi, OWM-TAMISEMI, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kalenga, Jackson Gideon Kiswaga, leo Septemba 01, 2026, Bungeni jijini Dodoma, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kupeleka fedha kwa haraka ili kukamilisha ukarabati wa shule hiyo kabla ya maadhimisho hayo.

Dkt. Dugange amesema Serikali tayari imepeleka Shilingi Milioni 867 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya shule hiyo, ikiwemo vyumba 20 vya madarasa, ofisi tatu za walimu, karakana, majengo mawili ya utawala, mabweni mawili, maktaba, kumbi mbili, bwalo, stoo ya chakula pamoja na matundu sita ya vyoo.

"Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali imeona umuhimu wa kupeleka fedha mapema ili angalau tuendelee kukarabati miundombinu iliyobaki. Lakini pia Serikali inaendelea kuhamasisha wadau kuiga mfano wa mpango wa Tosamaganga Sekondari katika kuchangia nguvu katika ukarabati wa shule hizo," amesema Dkt. Dugange.

Amesema pamoja na hatua zilizochukuliwa, bado shule hiyo ina mabweni sita, vyumba viwili vya madarasa na nyumba 28 za walimu ambazo hazijafanyiwa ukarabati, hivyo Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa miundombinu hiyo.

Amesema Shule ya Sekondari Tosamaganga, ambayo ni miongoni mwa shule kongwe nchini, inatarajiwa kutimiza miaka 100 ifikapo Oktoba 10, 2026, huku akitoa wito kwa wadau na wahitimu wa shule hiyo kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu. Aidha, amesema katika kipindi cha mwaka 2015/16 hadi 2022/23, Serikali imetumia Shilongi Bilioni 97.92 kukarabati shule kongwe 89 nchini.

PROF. SHEMDOE APONGEZA MPANGO WA M***I BIMA FOUNDATION KUWASAIDIA WANANCHI WASIO NA UWEZOWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri...
01/09/2026

PROF. SHEMDOE APONGEZA MPANGO WA M***I BIMA FOUNDATION KUWASAIDIA WANANCHI WASIO NA UWEZO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amekutana na Naibu M***i na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa na Mkurugenzi wa M***i Bima Foundation, Sheikh Ally Hamis Ngeruko na kujadiliana kuhusu mpango ya M***i Bima Foundation wa kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kugharamia bima ya afya kwa kuwalipia huduma hiyo.

Majadiliano hayo yamefanyika Agosti 31 katika ofisi ndogo ya Prof. Shemdoe jijini Dar es Salaam, ambapo Sheikh Ngeruko ameeleza kuwa mpango huo ni sehemu ya jitihada za taasisi hiyo iliyo chini ya M***i Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakary Zubeiry bin Ally katika kuunga mkono azma ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za afya kupitia utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.

Kwa upande wake, Prof. Shemdoe amepongeza uamuzi wa M***i Mkuu na uongozi wa M***i Bima Foundation kuanzisha mpango huo wenye lengo la kuwasaidia wananchi wenye uhitaji, hususan wale ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za bima ya afya, na kuongeza kuwa OWM - TAMISEMI ipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo pindi itakapohitajika.

Ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada hizo, Prof. Shemdoe amechangia kiasi cha Shilingi Milioni 1.5 ili zitumike kuwachangia wanufaika kumi wa M***i Bima Foundation.

Aidha, Prof. Shemdoe amewataka viongozi wa M***i Bima Foundation kushirikiana kwa karibu na taasisi binafsi na wadau mbalimbali katika Halmashauri ili kupata uwezeshaji na kuimarisha utekelezaji wa mpango huo.

Address

Dodoma

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ortamisemi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to ortamisemi:

Shortcuts

Share