Tarura Tanzania

Tarura Tanzania Ukurasa rasmi wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) "Barabara Bora kwa Maendeleo Ende

31/08/2026

HABARILEO..
KAGERA: MBIO za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026 zimepongeza ujenzi wa Barabara ya Marahala–MSD yenye urefu wa kilomita 0.49 iliyojengwa kwa kiwango cha lami wilayani Muleba, mkoani Kagera.

Barabara hiyo inatarajiwa kurahisisha mawasiliano na usafirishaji kati ya wananchi wa vijiji vya Magata, Nshamba, Muleba Mjini na Hospitali ya Wilaya ya Muleba, pamoja na kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi katika maeneo hayo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda, amepongeza ubunifu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Muleba wanaendelea kunufaika na miundombinu bora ya barabara.

Mwang’onda amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya barabara katika maeneo ya vijijini kwa lengo la kurahisisha mawasiliano, biashara na shughuli za kiuchumi, huku akiwataka wananchi kutumia fursa zinazotokana na miradi hiyo kuimarisha maisha na kuinua uchumi wao.

Kwa upande wake, Meneja wa TARURA Wilaya ya Muleba, Dativa Semforini, amesema barabara hiyo imekamilika kwa asilimia 100 na imewekewa taa za barabarani, hatua inayowawezesha wananchi kuendelea na shughuli zao za kibiashara hadi nyakati za usiku.

Amesema ujenzi wa barabara hiyo pia umerahisisha utoaji wa huduma katika Bohari ya Dawa (MSD), ambayo hapo awali ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kutokana na magari makubwa yanayofanya shughuli za usafirishaji katika bohari hiyo.

MWANG'ONDA APONGEZA UJENZI WA BARABARA YA MARAHALA - MSD MULEBAMuleba, KageraKiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2026 Waz...
31/08/2026

MWANG'ONDA APONGEZA UJENZI WA BARABARA YA MARAHALA - MSD MULEBA

Muleba, Kagera

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2026 Wazo Michael Mwang'onda amepongeza ubunifu wa wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa ubunifu na kuhakikisha wananchi wa wilaya ya Muleba wanaendelea kunufaika na miundombinu ya barabara

Pongezi hizo amezitoa wakati akizindua barabara ya Marahala - MSD yenye urefu wa Km. 0.49 kwa kiwango cha lami ambayo itarahisisha mawasiliano kati ya wananchi wa vijiji wa Magata Nshamba, Muleba mjini na Hospitali ya Wilaya ya Muleba.

Amesema serikali itaendelea kutekeleza miradi ya barabara kwa wanachi wavijiji ili kurahisisha mawasiliano biashara na uchumi huku akiwataka wananchi kutumia fursa zilizoko katika miradi ya barabara inayotelezwa kuinua uchumi wao.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilaya ya Muleba Dativa Semforini amesema kwa sasa barabara hiyo imekamilika kwa asilimia 100 na kuwekewa taa za barabarani na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kibiashara muda wote.

Amesema pia barabara hiyo imerahisisha huduma za Bohari ya Dawa (MSD) ambapo hapo awali barabara hiyo ilikuwa na changamoto kutokana na magari makubwa kufanya shughuli zake katika bohari hiyo.

Baadhi ya wananchi wanaotumia barabara hiyo kwa sasa akiwemo Seif Mzamiri amesema kuwa serikali imetatua changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa barabara kwa kiwango cha lami.

Amesema mara baada ya kuweka lami katika barabara hiyo wameshuhudia ujenzi wa hospital ukienda kwa kasi na sasa hospital imekamilika hivyo wanaamini
uwepo wa barabara hiyo itarahisha shughuli za afya masoko na mahitaji yote ya kijamii na kiuchumi.

30/08/2026
TARURA YAWAJENGEA UWEZO WATAALAMU KUIMARISHA USHIRIKISHWAJI WA JAMII KATIKA MATENGENEZO YA KAWAIDA YA BARABARA (CBRM)‎‎T...
28/08/2026

TARURA YAWAJENGEA UWEZO WATAALAMU KUIMARISHA USHIRIKISHWAJI WA JAMII KATIKA MATENGENEZO YA KAWAIDA YA BARABARA (CBRM)

‎Tabora

‎Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeendelea kuimarisha utekelezaji wa Mpango wa Matengenezo ya Barabara kwa kutumia vikundi vya kijamii (Community Based Routine Maintenance- CBRM) kwa kuwajengea uwezo wataalamu na wadau wanaohusika na ushirikishwaji wa jamii katika matengenezo ya kawaida ya barabara.

‎Mafunzo hayo yaliyofanyika Agosti 27, 2026 yamewashirikisha wataalamu kutoka TARURA mkoa wa Tabora, Mameneja wa wilaya zote mkoa wa Tabora pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Manispaa ya Tabora, Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Halmashauri ya Mji wa Nzega na Halmashauri ya Wilaya ya Uyui.

‎Mratibu wa mafunzo kutoka TARURA Makao Makuu Mhandisi Laurent Kyombo ametoa wito kwa wasimamizi wa mpango wa CBRM mkoani Tabora kushirikisha viongozi wa serikali wa ngazi zote ili kuhakikisha mfumo huo unatekelezwa ipasavyo na kuleta tija kwa jamii.

‎Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Meneja wa TARURA mkoa wa Tabora Mhandisi Lusako Kilembe ameishukuru TARURA makao makuu kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yanakwenda kuwajengea uwezo wasimamizi wa CBRM mkoani Tabora na kwamba TARURA imejipanga kikamilifu kutekeleza mpango wa CBRM.

‎Kwa upande wake, Mratibu wa CBRM mkoa wa Tabora Mhandisi Baraka Mkuya amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa na uwezo wa wataalamu katika ushirikishwaji wa jamii katika matengenezo madogo madogo ya barabara na utunzaji wa miundombinu ya barabara.

‎Aidha, Afisa Ustawi wa Jamii TARURA Bw. Ramadhani Ally amefafanua kuwa baada ya mafunzo hayo TARURA mkoa wa Tabora utaandaa mpango kazi wa utekelezaji wa CBRM ambao utatumika k**a mwongozo katika kuratibu, kutekeleza na kufuatilia shughuli za CBRM katika maeneo yanayotekeleza mfumo huo.

‎Utekelezaji wa CBRM unalenga kuongeza ushiriki wa jamii katika kutunza barabara, kuimarisha uwajibikaji wa jamii na kuhakikisha barabara zinabaki katika hali nzuri na kupitika kwa usalama.

WANANCHI MKOANI SHINYANGA WATAKIWA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA BARABARA ShinyangaKiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ...
28/08/2026

WANANCHI MKOANI SHINYANGA WATAKIWA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Shinyanga

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Ndugu Wazo Mwang’onda amewataka wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kuhakikisha wanalinda na kutunza daraja la Dodoma linalowaunganisha wakazi wa Shinyanga mjini na mtaa wa Butengwa ili liendelee kuwa na manufaa kwa vizazi vijavyo.

Mwang’onda ametoa wito huo baada ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kupokea taarifa, kukagua na kuzindua daraja hilo huku akimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizowezesha ujenzi wa daraja hilo.

Amesema ujenzi wa daraja hilo ni hatua muhimu katika kurahisisha usafiri na usafirishaji kwa wananchi wanaotumia njia hiyo hivyo ni wajibu wa wananchi kuhakikisha linatunzwa na kutumika kwa kuzingatia taratibu.

Aidha, Mwang'onda amewapongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa madaraja mbalimbali katika mkoa wa Shinyanga.

Amesema uwekezaji katika miundombinu ya barabara na madaraja una mchango mkubwa katika kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kuwaunganisha wananchi na maeneo mbalimbali.

Mwang’onda amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kushirikiana na serikali katika kulinda miundombinu hiyo ili iweze kudumu na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.

26/08/2026

Wananchi wa vijiji vya Lendikinya, Lashaine, Arkatan, Arkaria na Mtimmoja wilayani Monduli mkoani Arusha wameanza kunufaika na utekelezaji wa mradi wa RISE baada ya TARURA kukamilisha ujenzi wa boksi kalavati katika barabara ya Monduli–Lendikinya–Mtimmoja yenye urefu wa Kilomita 23.

TARURA YALETA TABASAMU KWA WANANCHI MONDULI, VIJIJI VITANO VYANUFAIKA NA MATENGENEZO YA BARABARA ‎‎Monduli, Arusha‎‎Wana...
26/08/2026

TARURA YALETA TABASAMU KWA WANANCHI MONDULI, VIJIJI VITANO VYANUFAIKA NA MATENGENEZO YA BARABARA

‎Monduli, Arusha

‎Wananchi wa vijiji vya Lendikinya, Lashaine, Arkatan, Arkaria na Mtimmoja wilayani Monduli mkoani Arusha wameanza kunufaika na utekelezaji wa mradi wa RISE baada ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kukamilisha ujenzi wa boksi kalavati katika barabara ya Monduli–Lendikinya–Mtimmoja yenye urefu wa Kilomita 23.

‎Mradi huo uliogharimu shilingi milioni 203 umelenga kuondoa kikwazo kilichokuwa kikisababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi hususan wakati wa mvua ambapo maeneo mbalimbali ya barabara hiyo yalikuwa yamekatika na kutengeneza makorongo yaliyofanya usafiri kuwa mgumu.

‎Meneja wa TARURA Wilaya ya Monduli, Mhandisi Janeth Erasto amesema ujenzi huo umekamilika na kwa sasa upo katika hatua ya uangalizi huku ukitoa suluhisho la kudumu kwa changamoto iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.

‎"Barabara hii inaunganisha kata ya Monduli Mjini na Sepeko kipindi cha mvua maeneo mengi yalikuwa hayapitiki kutokana na makorongo na maji mengi. Kupitia mradi wa RISE tumeondoa kikwazo hiki na sasa wananchi wanaweza kufikia huduma za kijamii kwa urahisi ikiwemo shule, zahanati, hospitali na masoko", amesema Mhandisi Janeth.

‎Kwa upande wake, mkazi wa kijiji cha Lendikinya Bi. Maria Alais amesema kabla ya ujenzi boksi kalavati kipindi cha mvua wananchi walilazimika kuvuka kwa miguu huku watoto wakikosa masomo kutokana na kushindwa kuvuka maeneo yaliyokuwa yakijaa maji.

‎"Wakati wa mvua tulikuwa tukivuka kwa miguu watoto walikuwa wakikosa masomo kwa sababu maji yalikuwa mengi hata akina mama wajawazito walikuwa wakipata changamoto ya kuvuka wakati mwingine kujifungulia njiani", amesema Maria.

‎Naye, Bw. Alais Esoto, Mjumbe wa Kamati ya Siasa wilayani Monduli amesema awali barabara hiyo ilikuwa ikikwamisha shughuli za kiuchumi na kijamii lakini baada ya kukamilika kwa ujenzi wa boksi kalavati kumerejesha matumaini kwa wananchi kwani sasa hata mvua ikinyesha wananchi wanavuka bila hofu wala usumbufu.

"Wakati wa mvua wananchi walikuwa wakikwama kwenda sokoni Monduli. Wanafunzi nao walipata changamoto kufika shuleni. Magari na hata

DARAJA LA IKINDA LAONDOA KERO YA USAFIRI KWA WANANCHI KAHAMA   watakiwa kulitunza daraja‎‎Kahama, Shinyanga‎‎Wananchi wa...
26/08/2026

DARAJA LA IKINDA LAONDOA KERO YA USAFIRI KWA WANANCHI KAHAMA

watakiwa kulitunza daraja

‎Kahama, Shinyanga

‎Wananchi wa kata za Ikinda na Bugarama halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameondokana na changamoto ya kukatika kwa mawasiliano wakati wa mvua baada ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja la Ikinda lenye urefu wa mita 11 katika barabara ya Ikinda–Buyange.

‎Daraja hilo limejengwa na TARURA kupitia mradi wa RISE unaotekelezwa kwa fedha za mkopo nafuu toka Benki ya Dunia ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha miundombinu ya barabara na kuondoa vikwazo vinavyokwamisha usafiri na shughuli za kiuchumi.

‎Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wameeleza kuwa kabla ya ujenzi wa daraja wakati wa msimu wa mvua barabara hiyo ilikuwa ikikatika na kufanya usafiri kuwa mgumu na kuhatarisha usalama wa wananchi na mali zao lakini kukamilika kwa daraja hilo changamoto hiyo sasa imekuwa historia.

‎Kwa upande wake, Meneja wa TARURA wilaya ya Kahama Mhandisi Joseph Mkwizu amesema ujenzi wa daraja hilo umegharimu shilingi milioni 410.02 ambapo mradi umekamilika kwa asilimia 100 kwa sasa upo katika kipindi cha matazamio.

‎Ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo umejumuisha ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 11 na upana wa mita 8, kalavati 3, uchongaji wa barabara urefu wa kilomita 4, kunyanyua tuta na kuweka changarawe kilomita 1 pamoja na uwekaji wa alama za barabarani chini ya Mhandisi Mshauri NOR-PLAN Tanzania Ltd huku kazi za ujenzi zikifanywa na M/S Mashilanga Construction Company Ltd.

‎Amesema kuwa zaidi ya kurahisisha usafiri daraja hilo linatarajiwa kuchochea shughuli za kiuchumi kwa kurahisisha usafirishaji wa mazao ya kilimo na bidhaa za biashara kwenda kwenye masoko huku wananchi wakipata fursa ya kusafiri kwa uhakika bila hofu ya barabara kukatika wakati wa mvua.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Ndugu Wazo Mwangonda baada ya kufungua daraja hilo la Ikinda amewataka wananchi kulitunza na kulinda daraja hilo kwa kuepuka kufanya shughuli zozote za kibinadamu pembezoni mwa daraja zinazowez

26/08/2026

TARURA kupitia mradi wa RISE umekamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha wananchi wa kata za Oloipiri, Soitsambu na Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha baada ya kuondoa changamoto ya kuvuka mto wakati wa msimu wa mvua na kurahisisha shughuli za kijamii na kiuchumi.

Address

Dodoma
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tarura Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share